Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,230
- 10,201
Kinachotuponza watanzania ni kukosoa jambo bila kuchunguza uhalisia wake. Uhuru mnaoutaka nyinyi haupo dunia kote. Kila nchi ina sheria na taratibu zake ambazo huwezi kuziepuka.
Kuhusu Libya ni suala ambalo linatakiwa kufundishwa hata mashuleni ili wanaokuwa waelewe kile kilichotokea Libya kabla historia haijaanza kupotoshwa. Jamaa kweli alikuwa dikteka, dikteka ambaye aliandaliwa na Uingereza kuja kuitawala Libya kwa kufanya mapinduzi lakini ni kiongozi aliyependa watu wake. Na waliompinga aliwapoteza. Aliuwa mapandikizi kama 2000, lakini baada ya kutoka madarakani ni watu wangapi wamekufa huko Libya?
Dunia leo inashuhudia idadi ya wakimbizi wengi kuwahi kutokea tangu dunia ianze Huko Syria! Hivi vitu huwezi kuvielewa kama hujaamua kuvielewa...
Gaddafi alitoa skolashipu bure kwa wanafunzi kutoka afrika, na alisaidia afrika katika tozo ya satelaiti tunayotumia leo kwenye mitandao. Pia hiyo Libya ya Gaddafi ilikuwa na maisha bora kwa kila raia kuliko nchi zote za mashariki ya kati. Sasa shida ya Gaddafi iko wapi hapo? Aliowaua ni kawaida kwa wahaini katika nchi yoyote ile, hata Tanzania Nyerere alikuwa anawapoteza watu waliokuwa wanahatarisha usalama wa serikali yake.
Uhuru mnaotaka nyinyi haupo dunia kote! Serikali lazima isimamie sema ni kwa namna tofauti. Kuna nchi zingine hata uchaguzi hautakiwi kuwepo, sababu za kiusalama na kuepusha vurugu. Ni nafuu kiongozi yule yule aendelee kutawala ili kuepusha machafuko, hii inatokea sana nchi za uarabuni.
Umesema vyema sana.
Sasa maswali ya kujiuliza
1. Tanzania tunatoa Scholarship ?
2. Tanzania tunasaida Africa kulipia Matumizi ya Sattelite ?
3. Raia wa Tanzania tuna Maisha bora kuwazidi watu wengine wote barani Africa ?
Ukijbu haya Maswali utajua kuwa hatupaswi kujifananisha na Libya ya enzi za Gadafi,hatufanani nayo hata Chembe...