Rais Magufuli na Libya

Gadafi hajawahi kuwa roll model ya utawala mzuri si kwa africa tu hata huko Libya kwenyewe, mambo yanayofanyika chini ya carpet kwa viongozi kama hao usipime, of course kuna watu wanafaidika na tawala kama hizo na watazisifia sana. Watu wanashindwa kuelewa kwamba aliyesababisha kutoweka kwa amani Libya ni Gadafi mwenyewe wala hakuna mtu mwingine, hata kufa alijisababishia yeye. Bila udikteta wake Gadafi angeweza kuifanya Libya ikawa nchi ya amani na utulivu daima na yeye akaishi kama Farther of the Nation hata baada ya kutoka madarakani.
 
Tangu Mobutu ameondoka madarakani ni miaka 20 sasa. Wamefanya nini cha maana zaidi ya migogoro ambayo haiishi. Natarajia utaniambia machafuko Zaire yameanzishwa na Wazungu pia maana wao kila mahali wanaanzisha machafuko as if sisi waafrika hatuna akili timamu.
 
Nchi ili iweze kuendelea pasipo shaka lazima udikteta utumike ,,mfn Libya,U.S,Uk,Russia,Israel,Egypt,Cuba,Venezuela na nyingine nyingi tu,udikteta ulitumika.Hivyo basi JPM ana malengo mazuri na Nchi yake
 
Watanzania wenzetu wanatushambulia na kutuita tusiojua as if wao ni waLibya.
 
Ila maandamano ya kusifia yanakubalika kufanyika kwa maana yanatoa pongezi na wanaoandamana si watu ila visiki. Yake maandamano ya kukosoa baadhi ya mambo si sahihi.
 
Bado hatujafikia huko ila Magufuli ndiyo anataka tuelekee huko
 
Marekani nchi ina uhura na ina maendeleo
Uk, France, Germany, canada huwezi kusikia radio imefungiwa kwasababu ya kumkosoa raisi au serekali lakini kuna amani na maendeleo. Sasa Mtukufu raisi ameona libya tu ndio mfano wa amani na utawala bora, na kama libya ya gadafii ilikua ina amani sana ile vita ilitoka wapi? Kama kila mtu ambae anaikosoa serekali anatupwa jela hio sio amani huo ni udikteta. Tanzania hatuna cha kujifunza kutoka kwa libya. Tuna mfumo wa utawala ambao ni bora sana kuliko libya japo magu anataka kuuharibu. Sisi tunatakiwa kuziangalia nchi kama marekani au UK ili siku moja tuwe kama wao sio libya.
 
Nchi ili iweze kuendelea pasipo shaka lazima udikteta utumike ,,mfn Libya,U.S,Uk,Russia,Israel,Egypt,Cuba,Venezuela na nyingine nyingi tu,udikteta ulitumika.Hivyo basi JPM ana malengo mazuri na Nchi yake

Cuba imeendelea?
 
% alizopata Magufuli hadi tunafika 2020 atabakiza 20% tu !!
 
Kama namwelewa Mtukufu Rais, anamlaumu Ghadafi kwa kutochukua hatua kuzima chokochoko kutoka nje. Kwamba hakuwaadhibu watu waliokuwa wamepewa ahadi za uongo. Matokeo yake aliangamia. Kwa kutumia mfano huo, hatovumilia chokochoko yoyote kutoka nje. Na anasema huko Zanzibar kuna chokochoko. Anawajua wanaofanya chokochoko na ameagiza waadhibiwe kwa kuwa wasipoadhibiwa yatampata yaliyompata Ghadafi.

Na sijui Mtukufu Rais alijuaje kuwa Libya kuna raha kwa ziara ya siku chache tu.
 
We Nyani acha uchochezi
 
Ndugu yangu kesi ya libya na tanzania ni tofauti....kule serikali ya familia ya gadafi na watu hawakuridhika ...nchi ni ya watu wote.
Hapa kwetu kuna mfumo tofauti. Tuna katiba na hatuna ufalme.
Tunafanya uchaguzi anayeshinda anatuongoza ...ndo katiba yetu inavo sema .
Hatuna ugomvi na hilo na raia wote wanali elewa ...ila ccm wao hawako huko wao mawazo yao kumbe ni ya ki gadafi gadafi...kuwa uchaguzi ni geresha tu lakini tukishindwa sisi hatutoi hii nchi ni mali yetu...wamefanya zanzibar. Sasa ndo hii mifano ya gadafi inapo tolewa.
Maana yake nini ? Maana yake hata kama ikitokea watanzania wameichoka ccm ..hawaitaki tena ..basi wao waendelee tu kututawala.... na hata kwa nguvu watatutawala...sasa wao ndo watatuchafulia ..ukaidi wao ndo utatuharibia...
Hivyo hiivi vya libya mfano tumtake mtawala wetu tukimkataa tutageuka libya.
Hii sio sahihi...ni wazi ccm bara bado wana mbavu za kuendelea kuchaguliwa..lakini ushawishi unapungua. Wakishinda sawa sawa hamna tabu...tujenge nchi
Wakushundwa sawa wakae pembeni...hapo tutafika hakutakua na gadafi wala syria...tutakua ma tanzania imara yenye umoja na upendo
 
tatizo la gadafi nikukaakatika cheokwamudamrefu miyaka 40 simchezo
Hao wanaokaa miaka kumi kumi wanaleta maendeleo ya nchi na wanawajali wananchi wao? mimi nadhani tatizo si kukaa muda mrefu, muhimu ni maendeleo yapatikane na wananchi wasisote, japokuwa hao wanaotetea "demokrasia" hawalikubali hilo. Ila kama kiongozi anakaa miaka mingi halafu hakuna maendeleo, njaa tupu, elimu ni shida, mahospitali hakuna dawa nk. basi hafai na hata kama atakaa miaka kumi tu halafu hamna kitu (kama hapa kwetu wameshabadilisha maraisi mara ngapi?) basi pia huyo kiongozi hafai.
 
Aaaa kumbe mawaazo yangu kwako yamepatwa poa
 
Nakubaliana nawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…