Rais Magufuli na karata ya machinga kuelekea 2020

Kuna uwezekano kuwa watapaswa kuvilipia kila mwaka.
Hii ni tax base nyingine kama leseni tu.
Cha mwaka sasa sijui kama wanacount kuanzia mwezi uliochukua au vipi
IMG-20181211-WA0073.jpeg
 
Mzee huyu kaona hapa njia pekee ya kuwarubuni machinga ni kuwaambia eti anawapa vitambulisho,

Kwanini visiwe vitambulisho vya kawaida, mfano kama vya kumtambulisha mkazi au aina nyingine mpaka viwe connected na TRA? Kwanini visitolewe na halmashauri au wizara ya viwanda na biashara ila atoe Magufuli kuputia mlango wa TRA?

Kwa sasa kitambulisho mmekipata kwa 20,000 hiyo ni Invitation to treat ,

Hivo mtavilipia mpaka 200,000 ,kwa Muda unaokuja hasa mwakani, na imeshatambulika kuwa huwa una kitambulisho, na kina mama lishe woote mtalipa

Nanukuu "Hakuna kumsumbua machinga au mama lishe mwenye kitambulisho hiki"

Alafu wakashangilia, yaan kwa logic ya kawaida ni kwamba wasiokuwa navyo wasumbuliwe, hivo ipo siku kitauzwa laki 4 lazima awe nacho kuepuka kusumbuliwa na mgambo, haya

Shangilieni
Nilisikia huu mfumo ulianza Rwanda miaka kadhaa iliyopita, na sas unakuja bongo.
 
Magufuli kaukazia upinzani mpaka hauwezi kufurukuta kwa hoja za msingi wamebaki na vihoja tu
Vioja ni RAISI wa nchi kuhangaika na KUORODHESHA majina ya wamachinga.
Baada ya kuwaziba pumzi 'wanasiasa', kujaza watu na vikundi vya mapambio, kuhakikisha vyombo vya habari vinamtajataja na kumsifu yeye muda wote, vyombo vya dola kuwanyanyasa na hata kutishia maisha ya 'wasiomwabudu', ukweli umemuingia kuwa bado hana MVUTO kama TWAWEZA walivyowahi eleza.
Maigizo hayo, kama ilivyokuwa kwenye makinikia, ukuta wa Mererani, viwanda (hewa), kununua watu, Korosho etc yataishi kwa mwezi mmoja tu halafu YATACHINA.
 
Bado tunasafari ndefu sana hapa.. Serikali ilitakiwa kuwa na mipango Endelevu juu ya vijana wake,Njia bora ya hizi ID ilikuwa pia hawa Machinga wawe conected na micro pension scheme and Health Insurance .....ili pia wapate huduma staiki wanapokuwa wagonywa na pale wanapozeeka wawe na tuela twa kuwasaidia kusukuma siku wakifikia muda wa kutembea na mkongojo!! Vinginevyo Serikali yetu kupitia idara ya kulea wazee itaingia garama nyingi mno miaka ya mbeleni kuwahudumia hawa today machingaz!
 
Wakuu huu mpango wa kuwathamini Machinga sio wa bahati mbaya.Hii ni karata kubwa kisiasa hasa kwa chama kilichochokwa na wananchi.

Watu wanajiuliza WHY Machinga?

(1) Population ya vijana wengi hasa mijini ni Machinga.

(2)HII NDIO POINT KUU

Watu wanasema Watanzania ni waoga,hasa katika mambo ya kudai haki tena hikihusisha MAANDAMANO.Na huo ndio ukweli

Kwanini watu ni waoga kuandamana kudai haki?.Wengi watakujibu kuwa "Tuache kutafuta ugali wa watoto tukaandamane,wapi".

Apa Tanzania watu wenye uthubutu wa kuandamana na kujitoa kwa 100% kudai haki ni MACHINGA pekee.

Machinga haogopi mabomu wala Segerea kwa sababu tayari kaishakosa haki yake ya kutafuta ridhiki,kwahiyo anajitoa muhanga kwa ajili ya familia yake.

Hii ni tofauti na sekta nyingine,mtu aandamane wakati ana uhakika na mwisho wa mwezi.

Magufuri anaitumia hii kete vizuri ili mwaka 2020 baada ya kujitangazia USHINDI,atawambia Machinga waendelee kuchapa kazi wasisikilize porojo za wapinzani.

Eti waandamane,wakati wameshapewa uhuru wa kufanya biashara,NEVER.

Narudia hakuna mtu wa kuingia road zaidi ya machinga,hata kule Mwanza na Arusha enzi za Slaa Machinga ndio waliokua wanaongoza zile harakati za maandamano.

2020 twende na......
Mtu asipokuwa makini kwenye Uzi wako,anaweza akaamini mawazo yako. Aliye makini atajua umepotoka, makusudi ama kwa bahati mbaya. Kama lengo lingekuwa kura za 2020 walengwa wazingekuwa connected na Tra. Subiri vilio vyao kabla ya 2020.
 
Wakuu huu mpango wa kuwathamini Machinga sio wa bahati mbaya.Hii ni karata kubwa kisiasa hasa kwa chama kilichochokwa na wananchi.

Watu wanajiuliza WHY Machinga?

(1) Population ya vijana wengi hasa mijini ni Machinga.

(2)HII NDIO POINT KUU

Watu wanasema Watanzania ni waoga,hasa katika mambo ya kudai haki tena hikihusisha MAANDAMANO.Na huo ndio ukweli

Kwanini watu ni waoga kuandamana kudai haki?.Wengi watakujibu kuwa "Tuache kutafuta ugali wa watoto tukaandamane,wapi".

Apa Tanzania watu wenye uthubutu wa kuandamana na kujitoa kwa 100% kudai haki ni MACHINGA pekee.

Machinga haogopi mabomu wala Segerea kwa sababu tayari kaishakosa haki yake ya kutafuta ridhiki,kwahiyo anajitoa muhanga kwa ajili ya familia yake.

Hii ni tofauti na sekta nyingine,mtu aandamane wakati ana uhakika na mwisho wa mwezi.

Magufuri anaitumia hii kete vizuri ili mwaka 2020 baada ya kujitangazia USHINDI,atawambia Machinga waendelee kuchapa kazi wasisikilize porojo za wapinzani.

Eti waandamane,wakati wameshapewa uhuru wa kufanya biashara,NEVER.

Narudia hakuna mtu wa kuingia road zaidi ya machinga,hata kule Mwanza na Arusha enzi za Slaa Machinga ndio waliokua wanaongoza zile harakati za maandamano.

2020 twende na......
Pembe
 
Back
Top Bottom