Rais Magufuli, mpe Zitto Wizara ya Nishati na Madini..

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Nitaandika kwa kifupi sana.

Kwa ninavyomsoma Rais wetu, si mtu wa kuyumbishwa na maneno ya kisiasa. Ameshayazoea, anayajua vyema.

Hasira yake ni pale mtu anapoifanya siasa ktk maeneo hatarishi hasa ya kitaifa. Mifano inajulikana.

Bezo, chuki na mayowe hazijawahi kumtoa kwenye focus mzee wetu. Badala yake amekuwa akitumia nafasi yake kama Baba na Amir wa taifa hili kudhibiti masuala mbalimbali. Hapo tutamwelewa baadae.

Ninachotaka kusema, ni kwa miezi kadhaa sasa nafasi ya Muhongo pale wizarani haijapewa mtu. Pengine ni ktk mwendelezo wa umakini na unyeti wa eneo husika Rais wetu alionao, au ni tafakari inayoendelea kumkagua yupi wa kumpa jukumu hilo.

Vyovyote iwavyo, uamuzi sahihi ambao kwa maoni yangu nadhani anayestahili nafasi hiyo ni aidha yeye mwenyewe Magufuli au Mbunge wa Kigoma Mjini, Bwana Zitto Kabwe.

Kwanini Magufuli?

Unyeti wa Wizara hii ya Madini unahitaji mtu jasiri hususani kipindi hiki ambacho tumedhamiria kulinda rasilimali zetu. Hiki chuma kikikaa mwenyewe pale hakuna wa kuleta ujanja ujanja, hivyo mambo yataenda. Kule bandarini Mzee wetu Mbarawa anafanya vyema.

Kwanini Zitto?

Sababu ni fupi sana. ELIMU. Bwana ZZK pamoja na kuwa ni mwanasiasa controversial sana, lakini ana uelewa mpana sana na masuala ya nishati na madini kwa ujumla wake. Pia ana advantage ya masuala ya uchumi hivyo atalifaa taifa kama akisimamiwa vizuri.

Najua Rais anapita hapa. Naomba asiwaze kisiasa kwenye hili. Kama anasimamia anachokiamini kutoka kwa aina ya viongozi anaowateua awamu hii (usomi) basi namuomba aliangalie hili kwa ukaribu.

Hata hivyo nitahadharishe tu. Akimpa nafasi hii Zitto, ajitahidi kumsimamia vizuri.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Ujinga ,hii nchi ili tuendelee tunahitaji kuondoa fikra finyu kama hizi ulizonazo.Toka lini mtu ndumila kuwili akaaminika ?
 
Back
Top Bottom