Rais Magufuli mpe kazi Makongoro Nyerere

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Hata Makongoro Nyerere hana sifa za kuwa hata naibu waziri?

Hivi Magufuli anathamini kweli mchango wa baba wa Taifa hili kweli? Watoto na ndugu Wa baba Wa Taifa hili wamewakosea nini? Mnasubiri msiba utokee mwende kuongea unafiki?.

Yule mwingine mlimyanganya ubunge Kwa nguvu watu wa Musoma wanakiri hivyo. Huyu naye baada ya kuenguliwa kwenye urais yaani mmeamua kuimaliza familia na kizazi cha Baba wa Taifa?

Hata uwaziri? Kweli jamaa hafai kiukweli. Mimi inaniuma sana ndugu zake na Baba Wa taifa kutokuwa kwenye system hata sehemu yeyote muhimu.

Siamini kama Makonda au Nape wana vyeo vikubwa lakini Makongoro hana cheo.

Laana ya kuitelekeza hii familia itafatafuna Ccm. Yaani hata hamjiuliz kwanini hamfanikiwi kwa mambo mengi mnayoyafanya.
 
Wewe jamaa uwe unafanya utafiti hata kidogo kabla ya kuangusha thread hapa Jamiiforums. Thread zako nyingi zimejaa mihemko, zimepitwa na wakati au zilizofirisika kihoja.

Makongoro Nyerere ni Mbunge wa EAC na kama hiyo haitoshi, kwa sasa ni Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Hata kama angekuwa sio Mbunge, hakuna utaratibu au sheria inayotaka mtoto wa Rais apewe cheo kwa sababu ni mtoto wa Rais.

Samahani kama nimekukwaza lakini kumbuka ukweli ni mchungu lakini ni dawa ya kukupa uelewa!
 
Duh!

Yaani fikra zingine bana...mtu unashindwa hata uziweke kwenye fungu gani!

Kisa yeye ni mtoto wa rais wa kwanza wa Tanganyika/ Tanzania ndo apewe kazi?

Na kwanza kwanini apewe kazi serikalini?

Hawezi kuomba kazi kwingineko kama ambavyo wengine hufanya?

Wahshi kabisa!
 
Mbona makongoro anapiga maisha EAC sema wengine wamesahaulika hata wangekua wawili kwenye system siyo mbaya.
 
Wewe jamaa uwe unafanya utafiti hata kidogo kabla ya kuangusha thread hapa Jamiiforums. Thread zako nyingi zimejaa mihemko, zimepitwa na wakati au zilizofirisika kihoja.

Makongoro Nyerere ni Mbunge wa EAC na kama hiyo haitoshi, kwa sasa ni Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Samahani kama nimekukwaza lakini kumbuka ukweli ni mchungu lakini ni dawa ya kukupa uelewa!
.
Eac kitu gani ni apewe Kazi kwenye system
 
Duh!

Yaani fikra zingine bana...mtu unashindwa hata uziweke kwenye fungu gani!

Kisa yeye ni mtoto wa rais wa kwanza wa Tanganyika/ Tanzania ndo apewe kazi?

Na kwanza kwa nini apewe kazi serikalini?

Hawezi kuomba kazi kwingineko kama ambavyo wengine hufanya?

Wahshi kabisa!
Kwani wanaopewa wana nini cha ziada?

Mtoto wa baba Wa taifa ni tunu ya taifa pia.
 
Wewe jamaa uwe unafanya utafiti hata kidogo kabla ya kuangusha thread hapa Jamiiforums. Thread zako nyingi zimejaa mihemko, zimepitwa na wakati au zilizofirisika kihoja.

Makongoro Nyerere ni Mbunge wa EAC na kama hiyo haitoshi, kwa sasa ni Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Hata kama angekuwa sio Mbunge, hakuna utaratibu au sheria inayotaka mtoto wa Rais apewe cheo kwa sababu ni mtoto wa Rais.

Samahani kama nimekukwaza lakini kumbuka ukweli ni mchungu lakini ni dawa ya kukupa uelewa!
Acheni kuwa wanafiki Siku msiba ukitokea tutasikiamatamko ya kinafiki na ahadi kibao.....
 
Mkuu;
Unashangaa nini kuona unafiki kwenye misiba?

Kuanzia wachungaji, Maaskofu mpaka Masheikh na Imam huwa ni wanafiki kwenye msiba na bila kusahau wanasiasa.

Wewe unayeshangaa unafiki inabidi tukushangae.

Ulisikia wabunge wa upinzani wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Samuel Sitta walivyokuwa wanampamba kwa maneno na mapambio?
 
Hata Makongoro Nyerere ana sifa za kuwa hata naibu waziri?
Jamani bado nasisitiza tujifunze kuandika kiswahili chetu. Sentensi hii ina maana tofauti kabisa na ulichotaka kuuliza! Ukisema ana tayari umekubali anayo. Badala yake ungeuliza ......hana....
 
Duh!

Yaani fikra zingine bana...mtu unashindwa hata uziweke kwenye fungu gani!

Kisa yeye ni mtoto wa rais wa kwanza wa Tanganyika/ Tanzania ndo apewe kazi?

Na kwanza kwa nini apewe kazi serikalini?

Hawezi kuomba kazi kwingineko kama ambavyo wengine hufanya?

Wahshi kabisa!

Yaani mradi ni watoto wa Nyerere basi wapewe kazi hata kama ni wendawazimu? Mkapa alijitahidi sana kuwabeba hata akamtunukia mtoto wake wa kike Rosemary ubunge wa viti maalum lakini ukweli ni kwamba hawabebeki!! Wameshindwa hata kumiliki mali za mama yao vikiwemo viwanja huko Mbezi beach ambavyo sasa vimekuwa mapango ya majambazi!!
 
Back
Top Bottom