Rais Magufuli: Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako ndio mji wenye nyumba na Makazi bora Tanzania

Leo tarehe 11 April 2019,Akiwa mji wa Makambako mheshimiwa Rais amekiri wazi kuwa hajawahi ona mji Tanzania uliopangwa na kuwa na nyumba bora za Makazi kama Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Ameomba mawaziri wakawaelimisha maeneo wanayotoka sehemu ya kujifunza nyumba bora ni Njombe

Yeye binafsi amekiri mkoa wake na mikoa mingi Tanzania hawaufikii mji wa Makambako

Ameshauri watu wakajifunze mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Hongereni Makambako


Mwambie aende Kitisi
 
Leo tarehe 11 April 2019,Akiwa mji wa Makambako mheshimiwa Rais amekiri wazi kuwa hajawahi ona mji Tanzania uliopangwa na kuwa na nyumba bora za Makazi kama Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Ameomba mawaziri wakawaelimisha maeneo wanayotoka sehemu ya kujifunza nyumba bora ni Njombe

Yeye binafsi amekiri mkoa wake na mikoa mingi Tanzania hawaufikii mji wa Makambako

Ameshauri watu wakajifunze mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Hongereni Makambako
JPM analipa fadhila kwa huyu jamaa aliyemtukuza.... fungua link hii hapa chini!

https://www.jamiiforums.com/threads...ndekeza-rais-magufuli-aongoze-milele.1505433/
 
Ukweli ni huu wiki 2 zilizopita nilikuwa huko makambako.... Ni kuzuri mno
 
Ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za mkoa wa Njombe hasa Wilaya za Njombe na Wanging'ombe ni bora kuliko maeneo mengine ya nchi. Tangu miaka ya 1980 vijijini vya Njombe nilikuwa havigawa ardhi ya kujenga kabla mwombaji hajaonyesha tanuri la matofali ya kuchoma. Ndiyo maana hakuna tembe huko. Shida yao ni sakafu na bati tu.
Mie naona Moshi kuna nyumba bora na kumepangwa vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninapafahamu Makambako vizuri. Kuna vibanda vya Mpesa, Mabanda ya mbao, gesti bubu, vibanda vya walevi, na maduka.
Nyumba za makazi zipo ila siyo bora kushinda za Buguruni wala Manzese, DSM.
Acheni kulinganisha Buguruni na mtaa wa Makambako

Hata mimi kuna wakati nilishangaa viwango vya nyumba za Makambako. Ukiwa barabarani, na hasa maeneo jirani na soko, utaona vibanda barabarani lakini ukitoka barabarani, ukaenda kwenye nyumba za makazi, kuna nyumba nyingi ambazo ni kufuru.

Kwanza nyumba nyingi zina maeneo makubwa. Halafu nilshangaa kuona nyumba kadhaa ambazo fence zake zimetengenezwa au kwa marumaru au kupambwa kwa vigae ambavyo maeneo mengine inakuwa ni nyumba chache kuona vimewekwa ndani ya nyumba lakini kule unakuta vimewekwa kwenye ukuta wa fence unaozunguka eneo la karibia nusu ekari.

Hata hivyo, kuna tofauti ya desturi kati ya watu wa Njombe na watu kama wa mikoa ya pwani na mikoa ya katikati ya Tanzania. Watu wa Njombe, wanathamini sana nyumba kuliko mavazi. Ukioneshwa nyumba na huyo anayeimiliki, kuna tofauti kubwa sana. Pale Morogoro, hoteli kubwa mpya zilizoko Morogoro, nyingi zinamilikiwa na watu wa Njombe. Siku moja nilishangaa kumwona fundi akitengeneza pavements za hotel lakini anayemchanganyia cement ya kujengea na mmiliki wa hotel.

Lakini pia miaka ya karibuni, ni watu wa Njombe ambao wamekuwa wakinunua sana majengo ya Kariakoo, na kuyavunja ili kuyajenga upya. Uchumi wa Njombe, tofauti na mikoa mingine umetawanyika kwa watu wengi, siyo kama mikoa mingine ambako unawakuta labda matajiri wawili wakubwa sana. Njombe hakuna. Ukiangalia hata mabasi yatokayo Njombe kwenda mikoa mbalimbali, hakuna hata moja la mwarabu au mhindi bali ni ya wananchi wa kawaida ambao wengi wao hawamiliki zaidi ya mabasi manne.

Biashara ya mbao na mazao ya mashambani, na moyo wa kujituma sana, vimewasaidia watu wengi wa Njombe kuwa na uchumi mzuri ukilinganisha na baadhi ya mikoa. Mkoa wa Mwanza, kwa mfano, ni Mwanza mjini ndiyo penye shughuli nyingi za kiuchumi, na ni mji mkubwa lakini vijiji vya mkoa wa Mwanza, vingi vina umaskini wa kupindukia. Shinyanga na Simiu ndiyo usiseme. Vijijini watu wanashindwa kuwa na uhakika hata wa chakula.

Hata ukienda vijiji vya mkoa wa Njombe, vingi hutakutana na nyumba hata moja ya tope. Nyingi ni nyumba za matofali ya kuchoma, japo nyingi hazina sakafu nzuri. Lakini watu wa kule wanafanya kazi sana, na wana moyo wa kujituma sana. Na wengi wao ni waaminifu kwenye masuala ya fedha.
 
Back
Top Bottom