Rais Magufuli: Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako ndio mji wenye nyumba na Makazi bora Tanzania

Leo tarehe 11 April 2019,Akiwa mji wa Makambako mheshimiwa Rais amekiri wazi kuwa hajawahi ona mji Tanzania uliopangwa na kuwa na nyumba bora za Makazi kama Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Ameomba mawaziri wakawaelimisha maeneo wanayotoka sehemu ya kujifunza nyumba bora ni Njombe

Yeye binafsi amekiri mkoa wake na mikoa mingi Tanzania hawaufikii mji wa Makambako

Ameshauri watu wakajifunze mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Hongereni Makambako
Kweli dude la Njombe linakuondoa haya unakuwa unajisemea semea tuuu. Mbarawa emb kapige pafu kadhaa tukusikie na wewe!
 
Anaongelea nyumba bora, Dodoma kuna nyumba za nyasi na tembe,
Mkuu tukisema Dar kuna Makazi hovyo hatuongelei ofisi na magorofa ya Posta na kariakoo

Angalia Makazi ya sinza, buguruni, magomeni ni kama taka taka ambazo hazikupaswa watu kuishi,
Kabisa mkuu ,yaani sinza unaruka maji ya kinyesi ndio unaingia nyumbani kwako na ni maeneo mengi tu dar makazi ni duni mnooo
 
Vijana wanasema sinza Makazi bora, Wakati ni slum na hovyo
Kabisa mkuu ,yaani sinza unaruka maji ya kinyesi ndio unaingia nyumbani kwako na ni maeneo mengi tu dar makazi ni duni mnooo
 
Hata mimi kuna wakati nilishangaa viwango vya nyumba za Makambako. Ukiwa barabarani, na hasa maeneo jirani na soko, utaona vibanda barabarani lakini ukitoka barabarani, ukaenda kwenye nyumba za makazi, kuna nyumba nyingi ambazo ni kufuru.

Kwanza nyumba nyingi zina maeneo makubwa. Halafu nilshangaa kuona nyumba kadhaa ambazo fence zake zimetengenezwa au kwa marumaru au kupambwa kwa vigae ambavyo maeneo mengine inakuwa ni nyumba chache kuona vimewekwa ndani ya nyumba lakini kule unakuta vimewekwa kwenye ukuta wa fence unaozunguka eneo la karibia nusu ekari.

Hata hivyo, kuna tofauti ya desturi kati ya watu wa Njombe na watu kama wa mikoa ya pwani na mikoa ya katikati ya Tanzania. Watu wa Njombe, wanathamini sana nyumba kuliko mavazi. Ukioneshwa nyumba na huyo anayeimiliki, kuna tofauti kubwa sana. Pale Morogoro, hoteli kubwa mpya zilizoko Morogoro, nyingi zinamilikiwa na watu wa Njombe. Siku moja nilishangaa kumwona fundi akitengeneza pavements za hotel lakini anayemchanganyia cement ya kujengea na mmiliki wa hotel.

Lakini pia miaka ya karibuni, ni watu wa Njombe ambao wamekuwa wakinunua sana majengo ya Kariakoo, na kuyavunja ili kuyajenga upya. Uchumi wa Njombe, tofauti na mikoa mingine umetawanyika kwa watu wengi, siyo kama mikoa mingine ambako unawakuta labda matajiri wawili wakubwa sana. Njombe hakuna. Ukiangalia hata mabasi yatokayo Njombe kwenda mikoa mbalimbali, hakuna hata moja la mwarabu au mhindi bali ni ya wananchi wa kawaida ambao wengi wao hawamiliki zaidi ya mabasi manne.

Biashara ya mbao na mazao ya mashambani, na moyo wa kujituma sana, vimewasaidia watu wengi wa Njombe kuwa na uchumi mzuri ukilinganisha na baadhi ya mikoa. Mkoa wa Mwanza, kwa mfano, ni Mwanza mjini ndiyo penye shughuli nyingi za kiuchumi, na ni mji mkubwa lakini vijiji vya mkoa wa Mwanza, vingi vina umaskini wa kupindukia. Shinyanga na Simiu ndiyo usiseme. Vijijini watu wanashindwa kuwa na uhakika hata wa chakula.

Hata ukienda vijiji vya mkoa wa Njombe, vingi hutakutana na nyumba hata moja ya tope. Nyingi ni nyumba za matofali ya kuchoma, japo nyingi hazina sakafu nzuri. Lakini watu wa kule wanafanya kazi sana, na wana moyo wa kujituma sana. Na wengi wao ni waaminifu kwenye masuala ya fedha.
Sasa hivi watu wa Njombe tayari wameshaingia Moshi kitambo wananunua majengo ya Wachaga
 
Hajapita Mafinga weweeeew!!!!!

Mafinga ndo mji ambao kwa sasa upo on the peak!!


Mafinga hoyeeeeeee!!!!!!!
Jidanganye uje kunitafuta hapo
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Mkuu nipo mafinga hapa Jumatatu narudi Dsm
 
Mji pekee East Africa ulioku na plani nzuri ni Tanga, japokuwa huo Mji ulitelekezwa na Nyerere, lakini umekaa vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuweni wakweli TANGA ilitelekezwa na nani? Kwasababu wakati wa nyerere (1961-1985) Tanga ilijengwa viwanda vingi sana kuliko wakati wowote ule wa uongozi nchi hii. Sasa Nyerere aliitelekeza Tanga lini? Na ni kipindi hicho Tanga ilikuwa ni ya pili kwa uzalishaji mali na ukubwa wa miji ikitanguliwa na Dar. Palikwa na viwanda wa Chuma, Cement, Sabuni, Usindikaji wa vyakula, Mkonge n.k. Isitoshe shughuli za usafirishaji wa bidhaa kupitia bandari ya Tanga na usafirishaji wa reli ulifanyika kipindi cha Mwl Nyerere. Sasa baada ya hapo hivyo vyote vilitoweka. Unamlaumuje Nyerere???
 
Mkoa wenye makazi Bora vijijin Ni Kilimanjaro ndio inaongoza
Kilimanjaro nzima Hakuna nyumba za nyasi tangu 1980's
Kwamba makambako ina nyumba bora kimpangilio kuliko moshi? Hahaha
FB_IMG_15020060897734219.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za mkoa wa Njombe hasa Wilaya za Njombe na Wanging'ombe ni bora kuliko maeneo mengine ya nchi. Tangu miaka ya 1980 vijijini vya Njombe nilikuwa havigawa ardhi ya kujenga kabla mwombaji hajaonyesha tanuri la matofali ya kuchoma. Ndiyo maana hakuna tembe huko. Shida yao ni sakafu na bati tu.
Hakuna mkoa unaoifikia kilimanjaro kwa makazi Bora vijijin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom