Harrison Justine
JF-Expert Member
- Jun 19, 2015
- 1,136
- 559
Rais wangu mpendwa angalau pitia hapa na nikuombe jambo moja tu, nalo ni kulipa madeni ya walimu. Katika hotuba zako ulisema unatambua kuwepo kwa madeni ya walimu na tayari umeandaa utaratibu wa kuyalipa. Ushauri wangu ni kuwa kwenye hayo madeni kuna aina kama tano za madai, 1. madeni yanayotokana na malimbikizo ya mishahara ambayo pia ina sehemu mbili a) wale waliorekebishiwa madaraja na kusubiri malimbikizo yao tu na b) walipanda daraja na bado hawajarekebishwa na kusubiri nyongeza na malimbikizo. 2. Pesa za likizo 3. Pesa za masomo 4. 5. Pesa za uhamisho na matibabu.
Ushauri wangu ni kulipa mapema kabla deni halijakua. Mfano kuna baadhi waliisharekebishiwa lakini baadaye wakarudishwa kwenye kwango walichokuwa wakipata awali kv kupandishwa toka E kwenda F na baadaye kutolewa F kurudi tena E. Wa aina hii ni wengi na malimbikizo yao huzidi kuongezeka mwezi hadi mwezi. Kwa sasa hivi kuna tofauti ya walimu kupanda kwa wakati mmoja na wengine kuendelea na mishahara katika ngazi ya F, E, G nk na wengine kuwa na mishahara ya madaraja ya chini ya hapo ilhali barua zao zinasomeka kupanda tarehe sawa.
Nadhani wewe ni mtu makini na jambo hili utalitolea tamko, Mungu akubariki.