Rais Magufuli, madeni ya walimu yanazidi kuongezeka

Harrison Justine

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,136
559
Rais wangu mpendwa angalau pitia hapa na nikuombe jambo moja tu, nalo ni kulipa madeni ya walimu. Katika hotuba zako ulisema unatambua kuwepo kwa madeni ya walimu na tayari umeandaa utaratibu wa kuyalipa. Ushauri wangu ni kuwa kwenye hayo madeni kuna aina kama tano za madai, 1. madeni yanayotokana na malimbikizo ya mishahara ambayo pia ina sehemu mbili a) wale waliorekebishiwa madaraja na kusubiri malimbikizo yao tu na b) walipanda daraja na bado hawajarekebishwa na kusubiri nyongeza na malimbikizo. 2. Pesa za likizo 3. Pesa za masomo 4. 5. Pesa za uhamisho na matibabu.
Ushauri wangu ni kulipa mapema kabla deni halijakua. Mfano kuna baadhi waliisharekebishiwa lakini baadaye wakarudishwa kwenye kwango walichokuwa wakipata awali kv kupandishwa toka E kwenda F na baadaye kutolewa F kurudi tena E. Wa aina hii ni wengi na malimbikizo yao huzidi kuongezeka mwezi hadi mwezi. Kwa sasa hivi kuna tofauti ya walimu kupanda kwa wakati mmoja na wengine kuendelea na mishahara katika ngazi ya F, E, G nk na wengine kuwa na mishahara ya madaraja ya chini ya hapo ilhali barua zao zinasomeka kupanda tarehe sawa.
Nadhani wewe ni mtu makini na jambo hili utalitolea tamko, Mungu akubariki.
 
Anaedai anaomba kwa huruma alipwe heeee heee anaedaiwa ndio mbabe hapa duh vitu vinaenda kasi ila kinyume nyume nilitegemea serikali ndio ingeandika haya maombi kua hawana hela wavumiliwe
 
Kweli anapaswa kuhakiki mpaka kwenye ngazi za mishahara kwani wako watumishi wengi has a walimu wameanza kazi pamoja lakini kuna utofauti wa mishahara.
 
Si waalimu peke yao wenye kuidai serikali wapo watumishi wa umma wengi tu wanaoidai serikali na wengine hadi wamestaafu hawajalipwa
 
swala hili la madaraja Mimi linaniuma sana kwani Mimi binafsi nilipenda daraja mwaka 2010 nikaja kurekebishiwa mshahara mwaka 2012 lakini mpaka Leo sijalipwa zaidi ya miezi 18,ila sasa toka nipande daraja 2010,sijapanda tena mpaka hii 2016 inaisha,yaani nafanya kazi sana ila moyo wangu hauna furaha kabisa,wenzangu nilioanza nao kazi wameshapanda hadi walioanza kazi mbele yangu wamenipita mshahara,yaani nahudhunika kweli,kosa langu naambiwa ni kwenda kusoma na kubadirisha muundo,nipo najiuliza hivi ukijiendeleza ukiwa kazini ni kosa?,kwa maana wale wasiojiendeleza ambao nilianza nao kazi wanamshahara mkubwa zaidi yangu,Inaniuma sana
 
alafu kuna watu wanashabikia sisiemu, Mimi kabla ya mambo ya uhakiki nilimshauri Mdogo wangu apige mikopo kwenye banks then asepe sasahv anasukuma biashara zake pasipo presha
 
Kwahili la mapunjo na kupanda madaraja,Mkuu aangalie sana.
Wanaomshauri watakuwa wanamdanganya,hali ni mbaya
 
Anaedai anaomba kwa huruma alipwe heeee heee anaedaiwa ndio mbabe hapa duh vitu vinaenda kasi ila kinyume nyume nilitegemea serikali ndio ingeandika haya maombi kua hawana hela wavumiliwe
Nchi hii ni Shida sana hasa hiyo taaluma ya waalimu
 
Mleta mada hajakosea kuomba kulipwa madeni..naona kuna wadau wanataka angekuja kudai humu kwa povu wakati hawawezi kwenda mahakaman kumsaidia kulipa fine....kama ujumbe umefika inatosha
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom