Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo.
Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali kama SGR na Stieglers Gorge(Bwawa la Nyerere).
Tunajua Bunge linamaliza muda wake na kuvunjwa June hii,2020. Kwa uhakika Wabunge na Mawaziri wote watalipwa mamia ya mamilioni ya Shilingi baada ya kulitumikia Bunge kwa miaka 5 tu!
Kinachosikitisha kuna wazee Wastaafu wamelitumikia Taifa hili kwa uaminifu na kwa miaka mingi kati ya 25~40 lakini mpaka sasa wengi wao hawajalipwa mafao yao tangu Wastaafu.
Wengine wana miaka 3,2,1 na wengine wana miezi kadhaa. Wazee hawa wanapofika PSSSF hupewa Majibu yaliyojaa visingizio vya uchelewesho wa malipo ya michango toka kwa Waajiriwa au makosa ya ujazaji wa fomu, majina au tarehe za kuzaliwa ilhali Ukweli ni kwamba Mifuko haina Fedha ya kuwalipa wazee hao.
Kama Hali itaendelea kuwa hivo Rais Magufuli ajue kuwa hatopata kura hata moja toka kwa hao wazee Wastaafu pamoja na familia zinazowategemea.
Wazee hao wamepigika sana hasa kipindi hiki cha Covic-19 maana hawana kipato chochote, hawana mishahara, hawana malipo ya pensheni na hawawezi kukopesheka popote.
Chondechonde Rais Magufuli toa maelekezo kwa Hazina ilipe Deni Hilo la PSSSF ili mfuko uwalipe Wastaafu hao wanyonge.