Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Ananyoosha kwanza nchi. Mbona raisi was Burundi hajawai kutoka nje ya nchi yake ,huu mwaka wa tano sasa.toka 2014 mpaka sasa,
 
Inasikitisha kwakweli, hii mikutano ndio fursa ya kukutana na wenzanko wakuambie wanafanya nini, sasa wewe kila siku umejifungia ndani kwako, ukienda mbali sana ni chattle......itabidi tuandamane kushinikiza rais awe anasafiri kuhudhuria mikutano ya maana kama hii
Mmmmmh peleka uzumbukuku huko, eti kukutana na wenzako wakuambie ufanye nini, 😂😂😏😂😂 mbona nyumbu mna akili finyu hivi?? 😂😂😂 Kuna siri duniani hapa karne ya mwisho hii eti kuna ambacho hakijulikani?

Yeye alivyokua akiomba kura alitumwa na hao ambao unataka akachukue ushauri kwao? Matatizo ya Tanzania atayajua mjapan ambae hata ileje Hajui ipo upande upi?

Funga bakuli chafu hilo
 
Anapata hasira akikaa na Mabeberu meza moja akiyaona anatamani ayatumbue tu
 
Inauma sana hasa kama tunataka maendeleo. Maendeleo hayaji kwa kujifungia Ikulu. Lazima ukapate new ideas na kubadilishana mawazo na wenzako hasa waliokuzidi ili upate maufundi.
Rais Lazima atambue kuna umuhimu wa kuhudhuria mikutano kama hii ya maendeleo.
Kikwete alipewa jina la utani la Vasco Da Gama kwa sababu ya mikutano kama hiyo ya Japan.

Wabongo huwa hatuna jema, kikiwa kizuri ni malalamiko kikiwa kibaya ni malalamiko pia.
 
Kikwete alipewa jina la utani la Vasco Da Gama kwa sababu ya mikutano kama hiyo ya Japan.

Wabongo huwa hatuna jema, kikiwa kizuri ni malalamiko kikiwa kibaya ni malalamiko pia.
Hapana Kikwete alizidi. Kuna mikutano muhimu sana. Huu wa Japan Rais alitakiwa aende. Maana huu unahusu maendeleo na yeye anataka maendeleo.
 
Kwani Mapinduzi wanafanyaga Wakuu wa Majeshi,hujawahi ona Rais anapinduliwa hapo hapo Mkuu wa Majeshi anapigwa shaba?
Mapinduzi mengi yaliyofanikiwa niliona wakuu wa majeshi wameunga mkono mapinduzi.
 
Raise anafanya vizuri kuliko marais wengi wa Africa, hana cha kujikomba......
Japan ni wadau wakubwa wa Maendeleo hapa nchini. Angetumia fursa hii kwenda kuonana ana kwa ana na PM wa Japan na kumpiga sound kuhusu maendeleo.
 
Alianza kukifahamu hicho kizungu pengine kabla mzazi wako wa kiume hajamfahamu yule wa kike.

Punguzeni utoto, unakuwa unawapunguzia sifa za kuitwa great thinkers.
Arafu dogo kuwa na adabu huyo jiwe ni mdogo sana kwa baba yangu. Kujuwa kizungu cha kuandika na kujibia mtihani ni tofauti na kujuwa kizungu cha kuongea na fahamu anajuwa kizungu cha kujibia mtihani ila sio cha kuongee kuwa na akili dogo
 
Kule Japan kuna mkutano unaohusu Maendeleo ya Africa. Najua Rais Magufuli ni muumini wa maendeleo.

Japan ni mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini kwetu.

Rais Magufuli najua umemtuma Waziri Mkuu, ila kumbuka tulikuchagua wewe na siyo Waziri Mkuu.

Unajua mkutano kuhudhuriwa na Rais kuna uzito wake?

Pia unakutana na ideas mpya. Sasa wewe umejifungia tu Ikulu huku marais wenzako wa Africa wanajadili maendeleo.

Tena hapa ungetumia uchu ulionao kwa maendeleo kuongea na waziri mkuu wa Japan.
Angalia Rais wa Rwanda juzi alikuwa France kwenye G7. Leo yupo Japan.

Rais wa South Africa pia ilikuwepo kwenye SADC, akawepo kwenye G7 leo yupo Japan.

Kama mpenda maendeleo ulitakiwa usikose huu mkutano.

View attachment 1192348View attachment 1192349View attachment 1192350
Ajui kijapani ndio maana. Kumbuka NI muchimi hasa. Akienda JPM watu wasio zidi 55 watakwenda. Walinza. Dakitari. Watu wa usalama. Watu ikulu mkewe. Batman (mtu wa usafi wa Rais, nguo anazo vaa)
 
Kikao kina umuhimu sana. Ukizingatia yeye anapenda maendeleo.

Mwanzo watetezi walisema anaweka mambo vizuri nchini. Huu ni mwaka wa 4, je tuendelee kuamini kwamba nchi bado haijakaa sawa? Kuna tatizo la msingi, time will tell.
 
Nampangia kwa sababu nilimpa kura Yangu. Kikao kama hiki tena Wajapan kabisa anamtuma waziri mkuu? Ona waziri mkuu hata front page haonekani.Rais ana uzito wake jamani.
Nani wewe CHADEMA mkampigia kura JPM? Lowassa alikuwa wapi wakati huo?
 
Mwanzo watetezi walisema anaweka mambo vizuri nchini. Huu ni mwaka wa 4, je tuendelee kuamini kwamba nchi bado haijakaa sawa? Kuna tatizo la msingi, time will tell.
Na kweli kuna kitu hakipo sawa kabisa. Hii siyo normal.
 
Ajui kijapani ndio maana. Kumbuka NI muchimi hasa. Akienda JPM watu wasio zidi 55 watakwenda. Walinza. Dakitari. Watu wa usalama. Watu ikulu mkewe. Batman (mtu wa usafi wa Rais, nguo anazo vaa)
Majaliwa anajua kijapan ? Maana Majaliwa ndo katumwa kumuwakilisha Rais. Hana impact yeyote huko. Hata kuongea na PM wa Japan hajaongea nae. Uhuru Kenyata kishaongea na PM wa Japan. Na Kaambiwa Japan itashiriki kikamilifu katika mifuko ya afya Kenya.
 
Ningekuwa raisi hata mimi nisingeenda. Yaani maraisi wote Africa mnajazana pale na vibakuli vyenu kweli?

Nadhani anasimamia maneno yake kuwa Tanzania ni Tajiri, bado tunahitaji misaada na uwekezaji ila kuna uombaji mwingine wakujishushia heshima kama nchi.

Japan moja inawaita maraisi wote Africa mumfuate awaambie atawavushaje. Wacha nife na umasikini wangu.

Masikini Jeuri
 
Back
Top Bottom