Tetesi: Rais Magufuli 'kuutumbua' Mwenge wa Uhuru

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Baada ya Rais John P. Magufuli kubadili na kuokoa fedha kwenye sherehe za Uhuru na Muungano,sasa Mwenge wa Uhuru uko njiani kutumbuliwa. Taarifa za kishushushu zinaonesha kuwa tayari Rais Magufuli ameitisha faili la Mwenge huo na kupata maelezo ya kutosha na kutisha kuhusu Mwenge huo.

Taarifa zinaonesha kuwa Rais Magufuli ameguswa na kutikiswa na matumizi makubwa yanayofanyika wakati wa mbio za Mwenge nchi nzima. Rais anapanga kutumbua Mwenge huo ambao sasa ni kero badala ya kuwa hero hapa nchini.

Wangapi wanaafiki bila unafiki?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Baada ya Rais John P. Magufuli kubadili na kuokoa fedha kwenye sherehe za Uhuru na Muungano,sasa Mwenge wa Uhuru uko njiani kutumbuliwa. Taarifa za kishushushu zinaonesha kuwa tayari Rais Magufuli ameitisha faili la mwenge huo na kupata maelezo ya kutosha na kutisha kuhusu mwenge huo.

Taarifa zinaonesha kuwa Rais Magufuli ameguswa na kutikiswa na matumizi makubwa yanayofanyika wakati wa mbio za mwenge nchi nzima. Rais anapanga kutumbua mwenge huo ambao sasa ni kero badala ya kuwa hero hapa nchini.

Wangapi wanaafiki bila unafiki?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Atumbue hakuna namna lakin mauchawi ya nchi sijajua waasisi wata lipokeaje
 
Kwa kuzingatia aina ya majipu alokwisha kuyatumbua, kimantiki, itashangaza sana kama hata tumbua hizo mbio za mwenge.
 
hilo jini linaloitwa mwenge litumbuliwe tu.chadema walitoa wazo wa kuliweka makumbusho tu.
 
Baada ya Rais John P. Magufuli kubadili na kuokoa fedha kwenye sherehe za Uhuru na Muungano,sasa Mwenge wa Uhuru uko njiani kutumbuliwa. Taarifa za kishushushu zinaonesha kuwa tayari Rais Magufuli ameitisha faili la Mwenge huo na kupata maelezo ya kutosha na kutisha kuhusu Mwenge huo.

Taarifa zinaonesha kuwa Rais Magufuli ameguswa na kutikiswa na matumizi makubwa yanayofanyika wakati wa mbio za Mwenge nchi nzima. Rais anapanga kutumbua Mwenge huo ambao sasa ni kero badala ya kuwa hero hapa nchini.

Wangapi wanaafiki bila unafiki?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Bora uchawi wa CCM ufike mwisho tumechoka nao.Kwanza ni kichocheo cha UKIMWI tu hakuna kingine.Mwenge umekuwa soko la ngono kwa vijana na watoto
 
Uwekwe makumbusho ya taifa maana umeongeza idadi ya waathirika wa ukimwi kuliko wazalendo
 
Kwa kifupi hauna mantiki yoyote, miradi ambayo hao watembeza mwenge uzindizu niya kulia fedha mf. Choo cha shule shs 10,000,000/- garama za maandalizi ya uzinduzi ni mara mbili ya hizo za ujenzi, sasa kuna faida gani hapo?
 
Na autumbue kwa namna ambayo utakufa moja kwa moja. Kusiwe na wa kuuibua tena.
 
mbona nasikia unaanza tar 18 mwezi huu huko morogoro? kumbuka hata kwenye kampeni alitumia hiyo alama!!!
 
Ndugu wana bodi,
Ningependa wale wote waliokunywa mvinyo wa vyama vyao au hawapo kuwasilisha mawazo na mitazamo yao huru na binafsi nawaomba kwa heshima na taadhima wapite hivi thread zipo nyingi humu JF, huu ni wakati sasa tunajenga Taifa tuko serious.

Nikirudi kwenye hoja ambayo ipo muda mrefu kidogo kuhusu mbio za mwenge kuna mawazo mchanganyiko hapa, kuna wale wanaotaka mwenge uwekwe jumba la makumbusho ubaki kuwa historia tu na kuna ambao wanaona mwenge uendelee lakini uwe kama kifimbo cha malkia ambacho kinakimbizwa kila baada ya miaka minne minne ila sisi tunaweza kuweka miaka sita sita au kumi.

Pia kuna kundi hili la tatu na bila kumung'unya maneno ni kundi la wanufaika wa mchezo huu wa mwenge, ukiwasikiliza hoja yao kuu ambayo ni dhaifu kabisa wanakwambia Mwenge unazindiwa miradi mingi ya maendeleo kana kwamba vile pesa za mwenge ndio zinagaramia ile miradi. Insanity.

Binafsi mimi mara ya mwisho kuchangia mwenge ni utawala wa Mwinyi kwa sababu ilikuwa shuleni ni lazima tuchangie mwenge, lakini kwa sasa kama afisa mtendaji hajipendi basi aje kwangu kunieleza habari za kuchangia mwenge kitakachopata atakuwa sample ya Taifa.

Kwahiyo mwenge umebaki kuwa mradi wa kuwakandamiza walimu kuwachangisha kinguvu (nipo tayari kukosolewa kama wameacha kuwalazimisha kuchangia mwenge) pili kuwandamiza wafanyabiashara hasa mabar maguest , mahotel hasa mikoani maana Dar watu wamepinda hata OCD anaweza kuliwa mitama.

Hivyo basi kwa maoni yangu binafsi kati ya mwenge na muungano mimi naona muungani ni zaidi ya mwenge, sasa najenga hoja kama Rais ameona umuhimu wa kuokoa pesa za kufanya sherehe za muungano kwa mwaka huu ili ziende moja kwa moja kwenye shughuli za maendeleo, je wadau huu si ni wakati muhafaka wa wa Rais kutumia option one kusitisha kwa miaka kadhaa au kuupeleka moja kwa moja jumba la makumbusho for good.

Naomba wadau tuweke mihemko ya vyama pembeni mimi chama changu ni Rais Magufuli, karibuni tuchangie kwa weledi na kwa mdau anayejuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni kiasi gani atuwekee hapa hili Rais apelekewe taarifa sahihi mchwa bado wengi wamemzunguka kila upande. Wale wanaohubiri uzalendo hebu onesheni uzalendo wenu hapa. Ni wakati sasa kila mtu ale kwa jasho lake tu.

Hapa kazi tu.

Cc: Pasco Manyerere Jackton Nyani Ngabu Kiranga
 
Ifike wakati tuanze kuulizana vyeti vya kuzaliwa maana wenzetu wengine uraia wenu unatia mashaka sana haya mwenge nao umekukosea nini; hivi umewahi kujiuliza sababu zake kwanza za kuanzisha mbio za mwenge au unadhani akina nyerere walikuwa hawana akili timamu. Watu tu wanaacha kuweka symbolism muhimu katika hizi ritual ndio maana wengine mnaleta madharau.
 
Huuu mwenge ni alama ya ushirikina unapaswa utupwa kati kati ya bahari for ever tena utupwe ukiwa unawaka
 
Back
Top Bottom