Rais Magufuli kutembelea China

Kwamba akienda huko thamani ya dola vs shillingi itashuka sio?
What is the impact asipoenda?

BTW asipoenda hilo unalotarajia litatokea ama!!!

Sometimes https://jamii.app/JFUserGuide your mind prior speaking otherwise people gonna https://jamii.app/JFUserGuide it.
 
Kwamba akienda huko thamani ya dola vs shillingi itashuka sio?

Ndivyo anaenda kwa madikteta wenzake. Makatili wasio kuwa refined kama yeye.
Hawezi kwenda na Washington na London kwa vile kule wanathamini utu na haki za binadamu.
Aende akawasalimu pia manyambuda wenzake akina Putin, Rohani, Kim un na ampe hi Duterte!!!
 
Hivi wewe ulikuwa unaijua nguvu ya makaburu na kina Ian Smith au unaongea tuu. Ukanda wote huo ulikuwa na mafisi, kuanzia Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia mpaka Afrika ya kusini.

Nyerere alichokifanya ni kuondoa vizingiti vya maendele kwa kusaidia kuondoa wakoloni wote ili baadae (siyo lazina iwe leo) iwe rahisi kufanya maendelea kwa kufanya biashara baina yetu bila bugdha.

Mfano ni pale Ian Smith (Southern Rhodesia - Zimbabwe) alipojitwalia madaraka alizuia Wazambia kutumia reli yao ya cape gauge iliyotumika kupitishia shaba ndipo Kaunda akamwomba Nyerere kutumia badari yetu lakini kwa kuwa hatukuwa na miundo mbinu, tukaomba mkopo WB ili tujenge reli. Jamaa wakakataa kutupatia mkopo kwa sababu chungu mzima zisizo na kichwa wala miguu, ndipo ikabidi tuombe Wachina watusaidie.

Sasa fikiria hizo fitna za kina Ian Smith ambazo ziliendelezwa mpaka WB, kama tungewaacha hao jamaa waendelee kutawala ukanda huu sasa hivi si wangekuwa wameota mapembe?

Wenzetu wazungu wameweka NATO, IMF na WB ili kulinda mazingira ya uwepo wao na kufanya biashara kwa faida ya nchi zao, nyinyi waswahili mnapata mtu mwenye akili anaeujua mchezo wa wakubwa, anawafundisha ujanja mnamuona hafai. kweli tuna safari ndefu.

Tatizo sisi waafrika ni kuwa na upeo mdogo sana wa kifikiri, wewe teyari umeshaleta ukabila kutaka chifu wa kichaga kuwa rais. Kama isingekuwa uwezo mkubwa wa nyerere kumpiku Marealle, leo hii Tanzania ingekuwa na ukabila wa hovyo kuliko hata ule wa Kenya. Leo hii Kenya wanashidwa hata kujenga BRT kwa kuwa wakikuyu wanaoneana haya kunyoosheana vidole kuhusu biashaa ya matatu. Wamefanya ufisadi KQ shirika linakufa kwa kuwa wakikuyu wamechukua chao, sasa hii ndo jamii unayotaka kuiiga?

Kama tungefuata akili za Marealle za umimi, leo mabeberu wangetumia mwanya huo kutufanya tupigane wenyewe kwa wenyewe kama vile Cameroon inavyopiganishwa.
Kusingizia African Underdevelopment kuwa imeletwa na, hao mnaowaita mabeberu, ni kutafuta visingizio vya kijinga tu.

Kwa hii sampuli ya watawala tulionao tusahau kabisa maendeleo, tutaendelea tu kuwa "The world's laughing stock throughout history".
 
Ndivyo anaenda kwa madikteta wenzake. Makatili wasio kuwa refined kama yeye.
Hawezi kwenda na Washington na London kwa vile kule wanathamini utu na haki za binadamu.
Aende akawasalimu pia manyambuda wenzake akina Putin, Rohani, Kim un na ampe hi Duterte!!!
Hahaha itakua anaenda kupata skills...
 
What is the impact asipoenda?

BTW asipoenda hilo unalotarajia litatokea ama!!!

Sometimes **** your mind prior speaking otherwise people gonna **** it.
Hilo lilikua ni swali, jifunze kutofaustisha kati ya swali na sentensi..
 
Nimekuwa nasubiri ziara ya Rais Magufuli China kwa muda mrefu,to me this is a dream come true.Natamani akitoka huko apitie Tehran and may be Moscow as a slap in the face to Western countries especially Washington.
Fuata link ifuatayo for more imformation.

=======

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini.

China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini.

Vyanzo vyetu vinasema ziara hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati mwafaka, ambapo China na Tanzania zinahitajiana zaidi kimkakati. Tanzania inaihitaji China katika mkakati wake wa kujenga viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

“Unajua China ni rafiki wa kweli…kuna hatua ambazo amezichukua Rais Magufuli za kuwadhibiti wanyonyaji wa rasilimali zetu zimewakera wadau wa maendeleo kutoka Bara la Ulaya.

“Ziara yake nje ya mipaka ya nchi kuanzia China, inapeleka ujumbe mzito sana, hiyo inanikumbuka miaka zaidi ya 40 iliyopita ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikwenda China kukutana na Mwenyekiti Mao.

“Kitendo cha Rais Magufuli kuanzia huko kinaleta hisia kali zaidi, maana ni dhahiri kwamba wote tunahitajiana, China inahitaji kuwekeza viwanda vyake Afrika na Tanzania imekaa kwenye nyonga ya Afrika ambako China inaweza kunufaika zaidi,” kinasema chanzo chetu.

Baadhi ya Watanzania waishio China wameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba kitendo cha Rais Magufuli kufanya ziara nchini China kitaleta imani ya wafanyabiashara wa China, hivyo Tanzania itakuwa kwenye nafasi ya kunufaika zaidi.

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Beijing, Salum Khamis Hussein, amesema nchi kama Tanzania ambayo inahitaji kukua kiviwanda pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa, inahitaji kuwa karibu zaidi na China.

“Tanzania inahitaji kuwa karibu zaidi na China, maana mambo mengi yanayofanywa na Rais Magufuli tunaona dhahiri namna yanavyoyakera mataifa ya Magharibi, mshirika wa kweli wa maendeleo ya Afrika kwa sasa ni China, japo tunatakiwa kujua namna ya kushirikiana naye.

“Zipo propaganda nyingi kuhusu China, hasa kwenye miradi, tumesikia kuhusu Zambia kwamba China sasa inaendesha migodi, Kenya nako tunaambiwa China wanataka kuendesha Bandari ya Mombasa, lakini ukweli ni kwamba tunawahitaji na wao wanatuhitaji, hivyo tunahitajiana,” anasema Salum.

JAMHURI limezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ambaye hakutaka kuzungumzia ziara hiyo isipokuwa kusisitiza kwamba huu ni mwaka wa uwekezaji.

Waziri Kabudi alisisitiza kuhusu kauli ya Rais Magufuli katika hafla ya kufungua mwaka wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (Sherry Party), kwamba, mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji. Hotuba hiyo ya Rais Magufuli imechapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.

Kwa kuzingatia kauli hiyo ya “mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji” JAMHURI linafahamu kuwa China imekuwa katika mipango ya kuwekeza viwanda 200 hapa nchini.

“Hilo (safari ya China) siwezi kulizungumzia. Ninachoweza kusema ni kwamba, kama alivyosema Mheshimiwa Rais katika ‘Sherry Party’ huu ni mwaka wa uwekezaji. Jambo jingine ninaloweza kusema ni kuwa uhusiano na ushirikiano wetu na nchi mbalimbali ni mzuri,” amesema Waziri Kabudi ambaye ameteuliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibuni akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.

JAMHURI limemtafuta Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambaye hakuwa tayari kuzungumzia ziara hiyo ya Rais Magufuli nchini China, akisisitiza kuwa suala hilo halijafika ‘mezani’ kwake, kwa hiyo si busara kulizungumzia.

Katika hali isiyo ya kawaida, hata watendaji wengine kadhaa wa serikali wamekuwa wazito kuzungumzia ziara hiyo, na miongoni mwao, wameshindwa hata kuzungumzia fursa za uwekezaji zilizopo kati ya China na Tanzania.

Safari hiyo ya Rais Magufuli nchini China itakuwa ya kwanza nje ya Bara la Afrika tangu aingie madarakani Novemba 5, 2015.

Rais Magufuli ataelekea China katika wakati ambao ujazo wa biashara kati ya taifa hilo na Tanzania unatajwa kufikia dola za Marekani bilioni 4.6, takriban Sh trilioni 10.3, kwa hiyo ziara yake inatajwa kuinufaisha Tanzania kupitia sera ya mambo ya nje ya diplomasia ya uchumi.

Rais Magufuli binafsi amewahi kusikika akiisifu China kwamba imekuwa ikitoa mikopo ambayo si tu ni yenye riba nafuu, bali pia isiyo na masharti ya ‘ajabu’.

Hali ilivyo

Oktoba mwaka jana China ilisherehekea miaka 69 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, siku ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi, kila mwaka na katika shughuli hiyo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, aliwaeleza waandishi wa habari mambo ambayo Tanzania inajivunia kutokana na uhusiano wake na China kwa zaidi ya miongo minne, akisema miongoni mwa mambo hayo ni yale ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kwa mujibu wa balozi huyo, kihistoria China iliiunga mkono Tanzania katika harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika na Tanzania kuongoza harakati za kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kutambulika katika Umoja wa Mataifa na kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyonufaika na misaada ya China tangu miaka ya 1960, na miongoni mwa manufaa hayo ni Reli ya Uhuru (Tazara) iliyojengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China, ukiwa ni mradi mkubwa wa kwanza kufanywa na China nje ya mipaka yake.

Alieleza kuwa Tanzania pia imekuwa ikinufaika na misaada ya China katika sekta ya elimu na afya na kwamba, kwa miaka 50 sasa China imekuwa ikituma madaktari wake kufanya kazi nchini huku maelfu ya Watanzania wakipata fursa ya mafunzo nchini China.

Balozi huyo anaamini kuwa Tanzania inaweza kunufaika zaidi na China katika maeneo mengine kadhaa yakiwamo ya utalii, kilimo na uwekezaji katika viwanda.

Takwimu zinabainisha kuwa miradi mipya isiyopungua 196 imesajiliwa nchini katika sekta za viwanda, makazi, kilimo na uvuvi, na ujazo wa kibiashara kati ya China na Tanzania ukitajwa kufika dola za Marekani bilioni 4.3 kwa mwaka.

Katika moja ya mikutano ya jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika, China ilikwisha kutangaza kutenga dola za Marekani bilioni tano kununua bidhaa kutoka Afrika, hatua ambayo inatajwa kuwa ni fursa nzuri kwa Tanzania.

Rais Xi Jinping Dar

Machi, 2013, Rais wa China, Xi Jinping, alifanya ziara nchini Tanzania kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Jakaya Kikwete, na mataifa haya mawili kutia saini mikataba 17 ya ushirikiano.

Mataifa haya mawili uhusiano wake umedumu kwa miaka takriban 57 sasa, tangu iliyokuwa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Rais Xi kwa wakati huo alifika Dar es Salaam akitokea Moscow, Urusi ambako ndiko alikoanza safari yake ya kwanza katika nchi za nje tangu kuapishwa kwake rasmi kuwa Rais wa China.

Katika mikataba hiyo 17 aliyotia saini Rais Xi, masilahi mbalimbali yaliguswa, yakiwamo ya kiuchumi na utamaduni. Miongoni mwa hayo ni ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo pamoja na mtandao wa reli wa kuunganisha na reli nyingine za Tanzania.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam kwa wakati huo, kiongozi huyo wa China alisema ziara yake ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizi, uhusiano ambao umeendelea tangu ulipoanza wakati wa Rais Julius Nyerere na Mao Zedong.

Wachambuzi wa mambo wanaeleza kuwa China inaitazama Afrika kama mbia muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, ikilenga kuwekeza katika madini, nishati na miundombinu, lakini pia Afrika ni soko muhimu la bidhaa za China.

Taarifa za mwaka 2013 wakati wa ziara hiyo zilibainisha kuwa China ni taifa la pili katika uwekezaji nchini Tanzania likitanguliwa na Uingereza.

Magufuli na safari za nje

Mwezi Januari mwaka 2017, Rais Magufuli ambaye imekuwa nadra kwake kusafiri nje ya nchi, kwa mara ya kwanza alisafiri nje ya Afrika Mashariki, kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia ambako alihudhuria mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhudhuria mkutano huo tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano, Novemba 2015.

Akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, ambao vilevile ulihudhuriwa na Antonio Guterres, akiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Ni mkutano huo ambao pia ulitumiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), iliyokuwa ikiwaniwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswana, Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea, Mba Mokuy.

Fursa zaidi China

Gazeti la JAMHURI linafahamu kuhusu kuwapo kwa ongezeko kubwa la wafanyabiashara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki pamoja na vifaa vya kielektroniki.

Biashara ya nguo imekuwa ikichukua nafasi kubwa, na soko la nguo za China nchini limekuwa likikua siku hadi siku, ingawa Rais Magufuli amekuwa na msimamo wa kuhakikisha pamba ya nchini inatumika kutengeneza nguo hapa Tanzania na si kuisafirisha nje ya nchi, kisha Tanzania kuagiza nguo kutoka nje.

Mji wa Guangzhou ni moja ya miji ambayo wafanyabiashara wa nguo wa Tanzania hufika kwa ajili ya kununua na kuleta bidhaa hizo nchini.

Miji mingine ambayo wafanyabiashara wa Tanzania hufika kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za kuuza nchini ni pamoja na Shenzhen.
Lakini wakati Magu anaufuta mradi wa bandari ya Bagamoyo si alisema "Wachina hawa wa sasa sio wale waliojenga reli ya Tazara!"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabeberu wa Kichina ndio balaa, anawaliza mpaka Mabeberu ya Kimarekani na Ulaya. Ufumbuzi wa uhakika na sisi tuwe Mabeberu ili tupelekeshane Mabeberu wengine, bila hivyo, kubadilisha Mabeberu hakutatusaidia bali tutaendelea kupandwa na tutaishia kulalamika tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusingizia African Underdevelopment kuwa imeletwa na, hao mnaowaita mabeberu, ni kutafuta visingizio vya kijinga tu.

Kwa hii sampuli ya watawala tulionao tusahau kabisa maendeleo, tutaendelea tu kuwa "The world's laughing stock throughout history".
It is your privilege that made you make that comment.
 
Aliwanyima zabuni ya kujenga reli ya kisasa hadi Kikwete akiingilia kati akambeza sasa anakula matapishi yake.. Akawapiga na vijembe wachina kwamba miradi yao ni ya ovyo kimsingi hatuna leader

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ndo nilietaja dola kuhusu kushuka kwake thamani wewe ndo unaeota kwamba itashuka thamani au huelewi kati yangu mimi na wewe nani anaota? Au ni mkimbizi huelewi kiswahili vizuri
So you think kushuka kwa dollar ndio kushuka kwa uchumi. And that is final? Yaani no other factors included, these were delibarated measures the government applied, whose consequences ndio huku kushuka kwa dollars, ambayo upinzani ndio credit yenu currently, ofcourse to fellow stupid nyumbus. Tides will change
Enda kadanganye wajinga wenzako na dharau zako, kuna wauza machungwa na mashamba yao wanafanya international trade making more dollars than, acha dharau.
Lets get into detailed debate on this issue, if you want.

Sasa kwa akili zako wewe uchumi uliopo umeshuka au umeimarika? Unapokua huna reserve kubwa ya dollar uchumi lazima uyumbe, unavyoongelea wanaofanya biashara kwa dollar wakati watu miezi mingi walizuiwa kuuza mazao nje unakua unatumia akili za wapi? Wewe ndo uliezungumzia kwamba what i said is final na hakuna other factors sio mimi..umeni label kama mpinzani sababu sijasema kile unachotaka au unachopenda kusikia? Kweli wewe ni mjinga zaidi yangu mimi inafaa uwe kiongozi wa wajinga..kiuhakika sina muda wa ligi za kindezi..
 
I don't understand your vague comment. What privilege are you talking about?
People such as yourself that are able to articulate well, in both languages, because you had teachers who received free education, would never comprehend what this animal called privilege is... the Somalis would.
 
Naposema mbadala si maanishi vitu vya bure bali uwezo wa nchi kufanya mazungumzo huku kukiwa na uchaguzi wa maamuzi. Mfano ni pale tulipowapiga chini Wachina na kuwachagua Yapi Markezi kwenye ujenzi wa reli.
Utafanya vipi uchaguzi wa maamuzi wakati una shida nzito na unayemwomba anakujua kabisa una shida kalii na huna tena kwingine kwa kuomba ??
 
Kwa sasa uchaguzi upo, unachagua kati ya mashariki au magharibi siyo kama ilivyokuwa miaka ya 90.
 
Nimekuwa nasubiri ziara ya Rais Magufuli China kwa muda mrefu,to me this is a dream come true.Natamani akitoka huko apitie Tehran and may be Moscow as a slap in the face to Western countries especially Washington.
Fuata link ifuatayo for more imformation.

=======

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini.

China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini.

Vyanzo vyetu vinasema ziara hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati mwafaka, ambapo China na Tanzania zinahitajiana zaidi kimkakati. Tanzania inaihitaji China katika mkakati wake wa kujenga viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

“Unajua China ni rafiki wa kweli…kuna hatua ambazo amezichukua Rais Magufuli za kuwadhibiti wanyonyaji wa rasilimali zetu zimewakera wadau wa maendeleo kutoka Bara la Ulaya.

“Ziara yake nje ya mipaka ya nchi kuanzia China, inapeleka ujumbe mzito sana, hiyo inanikumbuka miaka zaidi ya 40 iliyopita ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikwenda China kukutana na Mwenyekiti Mao.

“Kitendo cha Rais Magufuli kuanzia huko kinaleta hisia kali zaidi, maana ni dhahiri kwamba wote tunahitajiana, China inahitaji kuwekeza viwanda vyake Afrika na Tanzania imekaa kwenye nyonga ya Afrika ambako China inaweza kunufaika zaidi,” kinasema chanzo chetu.

Baadhi ya Watanzania waishio China wameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba kitendo cha Rais Magufuli kufanya ziara nchini China kitaleta imani ya wafanyabiashara wa China, hivyo Tanzania itakuwa kwenye nafasi ya kunufaika zaidi.

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Beijing, Salum Khamis Hussein, amesema nchi kama Tanzania ambayo inahitaji kukua kiviwanda pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa, inahitaji kuwa karibu zaidi na China.

“Tanzania inahitaji kuwa karibu zaidi na China, maana mambo mengi yanayofanywa na Rais Magufuli tunaona dhahiri namna yanavyoyakera mataifa ya Magharibi, mshirika wa kweli wa maendeleo ya Afrika kwa sasa ni China, japo tunatakiwa kujua namna ya kushirikiana naye.

“Zipo propaganda nyingi kuhusu China, hasa kwenye miradi, tumesikia kuhusu Zambia kwamba China sasa inaendesha migodi, Kenya nako tunaambiwa China wanataka kuendesha Bandari ya Mombasa, lakini ukweli ni kwamba tunawahitaji na wao wanatuhitaji, hivyo tunahitajiana,” anasema Salum.

JAMHURI limezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ambaye hakutaka kuzungumzia ziara hiyo isipokuwa kusisitiza kwamba huu ni mwaka wa uwekezaji.

Waziri Kabudi alisisitiza kuhusu kauli ya Rais Magufuli katika hafla ya kufungua mwaka wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (Sherry Party), kwamba, mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji. Hotuba hiyo ya Rais Magufuli imechapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.

Kwa kuzingatia kauli hiyo ya “mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji” JAMHURI linafahamu kuwa China imekuwa katika mipango ya kuwekeza viwanda 200 hapa nchini.

“Hilo (safari ya China) siwezi kulizungumzia. Ninachoweza kusema ni kwamba, kama alivyosema Mheshimiwa Rais katika ‘Sherry Party’ huu ni mwaka wa uwekezaji. Jambo jingine ninaloweza kusema ni kuwa uhusiano na ushirikiano wetu na nchi mbalimbali ni mzuri,” amesema Waziri Kabudi ambaye ameteuliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibuni akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.

JAMHURI limemtafuta Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambaye hakuwa tayari kuzungumzia ziara hiyo ya Rais Magufuli nchini China, akisisitiza kuwa suala hilo halijafika ‘mezani’ kwake, kwa hiyo si busara kulizungumzia.

Katika hali isiyo ya kawaida, hata watendaji wengine kadhaa wa serikali wamekuwa wazito kuzungumzia ziara hiyo, na miongoni mwao, wameshindwa hata kuzungumzia fursa za uwekezaji zilizopo kati ya China na Tanzania.

Safari hiyo ya Rais Magufuli nchini China itakuwa ya kwanza nje ya Bara la Afrika tangu aingie madarakani Novemba 5, 2015.

Rais Magufuli ataelekea China katika wakati ambao ujazo wa biashara kati ya taifa hilo na Tanzania unatajwa kufikia dola za Marekani bilioni 4.6, takriban Sh trilioni 10.3, kwa hiyo ziara yake inatajwa kuinufaisha Tanzania kupitia sera ya mambo ya nje ya diplomasia ya uchumi.

Rais Magufuli binafsi amewahi kusikika akiisifu China kwamba imekuwa ikitoa mikopo ambayo si tu ni yenye riba nafuu, bali pia isiyo na masharti ya ‘ajabu’.

Hali ilivyo

Oktoba mwaka jana China ilisherehekea miaka 69 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, siku ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi, kila mwaka na katika shughuli hiyo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, aliwaeleza waandishi wa habari mambo ambayo Tanzania inajivunia kutokana na uhusiano wake na China kwa zaidi ya miongo minne, akisema miongoni mwa mambo hayo ni yale ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kwa mujibu wa balozi huyo, kihistoria China iliiunga mkono Tanzania katika harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika na Tanzania kuongoza harakati za kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kutambulika katika Umoja wa Mataifa na kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyonufaika na misaada ya China tangu miaka ya 1960, na miongoni mwa manufaa hayo ni Reli ya Uhuru (Tazara) iliyojengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China, ukiwa ni mradi mkubwa wa kwanza kufanywa na China nje ya mipaka yake.

Alieleza kuwa Tanzania pia imekuwa ikinufaika na misaada ya China katika sekta ya elimu na afya na kwamba, kwa miaka 50 sasa China imekuwa ikituma madaktari wake kufanya kazi nchini huku maelfu ya Watanzania wakipata fursa ya mafunzo nchini China.

Balozi huyo anaamini kuwa Tanzania inaweza kunufaika zaidi na China katika maeneo mengine kadhaa yakiwamo ya utalii, kilimo na uwekezaji katika viwanda.

Takwimu zinabainisha kuwa miradi mipya isiyopungua 196 imesajiliwa nchini katika sekta za viwanda, makazi, kilimo na uvuvi, na ujazo wa kibiashara kati ya China na Tanzania ukitajwa kufika dola za Marekani bilioni 4.3 kwa mwaka.

Katika moja ya mikutano ya jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika, China ilikwisha kutangaza kutenga dola za Marekani bilioni tano kununua bidhaa kutoka Afrika, hatua ambayo inatajwa kuwa ni fursa nzuri kwa Tanzania.

Rais Xi Jinping Dar

Machi, 2013, Rais wa China, Xi Jinping, alifanya ziara nchini Tanzania kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Jakaya Kikwete, na mataifa haya mawili kutia saini mikataba 17 ya ushirikiano.

Mataifa haya mawili uhusiano wake umedumu kwa miaka takriban 57 sasa, tangu iliyokuwa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Rais Xi kwa wakati huo alifika Dar es Salaam akitokea Moscow, Urusi ambako ndiko alikoanza safari yake ya kwanza katika nchi za nje tangu kuapishwa kwake rasmi kuwa Rais wa China.

Katika mikataba hiyo 17 aliyotia saini Rais Xi, masilahi mbalimbali yaliguswa, yakiwamo ya kiuchumi na utamaduni. Miongoni mwa hayo ni ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo pamoja na mtandao wa reli wa kuunganisha na reli nyingine za Tanzania.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam kwa wakati huo, kiongozi huyo wa China alisema ziara yake ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizi, uhusiano ambao umeendelea tangu ulipoanza wakati wa Rais Julius Nyerere na Mao Zedong.

Wachambuzi wa mambo wanaeleza kuwa China inaitazama Afrika kama mbia muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, ikilenga kuwekeza katika madini, nishati na miundombinu, lakini pia Afrika ni soko muhimu la bidhaa za China.

Taarifa za mwaka 2013 wakati wa ziara hiyo zilibainisha kuwa China ni taifa la pili katika uwekezaji nchini Tanzania likitanguliwa na Uingereza.

Magufuli na safari za nje

Mwezi Januari mwaka 2017, Rais Magufuli ambaye imekuwa nadra kwake kusafiri nje ya nchi, kwa mara ya kwanza alisafiri nje ya Afrika Mashariki, kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia ambako alihudhuria mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhudhuria mkutano huo tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano, Novemba 2015.

Akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, ambao vilevile ulihudhuriwa na Antonio Guterres, akiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Ni mkutano huo ambao pia ulitumiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), iliyokuwa ikiwaniwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswana, Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea, Mba Mokuy.

Fursa zaidi China

Gazeti la JAMHURI linafahamu kuhusu kuwapo kwa ongezeko kubwa la wafanyabiashara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki pamoja na vifaa vya kielektroniki.

Biashara ya nguo imekuwa ikichukua nafasi kubwa, na soko la nguo za China nchini limekuwa likikua siku hadi siku, ingawa Rais Magufuli amekuwa na msimamo wa kuhakikisha pamba ya nchini inatumika kutengeneza nguo hapa Tanzania na si kuisafirisha nje ya nchi, kisha Tanzania kuagiza nguo kutoka nje.

Mji wa Guangzhou ni moja ya miji ambayo wafanyabiashara wa nguo wa Tanzania hufika kwa ajili ya kununua na kuleta bidhaa hizo nchini.

Miji mingine ambayo wafanyabiashara wa Tanzania hufika kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za kuuza nchini ni pamoja na Shenzhen.
Aisee
 
Back
Top Bottom