Rais Magufuli kukabidhi jukumu la Uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mkutano wa 40 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika leo Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo Rais John Magufuli anatarajiwa kukabidhi jukumu la uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi.

Mkutano wa Dodoma utafanyika kwa njia ya video kwa kuongozwa na Rais wa Msumbiji. Kaulimbiu ya mkutano huo ni;’Miaka 40 ya kuimarisha amani na usalama, kukuza maendeleo na kuhimili changamoto zinazoikabili dunia’

Rais Magufuli amekuwa Mwenyekiti SADC kwa mwaka mmoja. Alikabidhiwa jukumu hilo Agosti mwaka jana kutoka kwa Rais wa Namibia Dk Hage Geingob.

Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alizishukuru nchi 16 wanachama wa SADC kwa namna walivyoshirikiana na Tanzania kufanikisha ajenda muhimu za kikanda.

Waziri Kabudi pia alimshukuru Rais Magufuli kwa uongozi mahiri ulioziwezesha sekta za jumuiya hiyo kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC jijini Dar es Salaam.

"Ushirikiano wa pamoja umewezesha haya. Uongozi bora wa Rais John Joseph Pombe Magufuli umetuwezesha kufikia malengo ya SADC yaliowekwa. Ushirikiano mkubwa wa Sekretarieti ya SADC kupitia Dk Tax umewezesha haya. Mawaziri wenzangu kutoka nchi zote 16 za jumuiya wakiwamo mawaziri wa afya, wamefanya kazi kubwa kuikabili Covid-19)," alisema Profesa Kabudi.

Alisema Tanzania inashukuru kuwa, inapoachia kiti cha uenyekiti, ajenda ya viwanda kupitia Mkakati wa Viwanda (2015-2063) imebaki kuwa endelevu katika kukuza uchumi wa SADC na hatua za utekelezaji zimefanyika ikiwamo kuanzisha viwanda vya dawa.

Kabudi alitaja maeneo mengine ambayo Tanzania imefanikiwa kutekeleza kama kipaumbele chake kuwa ni Kiswahili kuridhiwa kuwa lugha ya nne ya SADC.

"Wapendwa mawaziri, tunayashukuru maamuzi ya Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa uamuzi wa kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya nne ya Jumuiya yetu. Kiswahili ni lugha ya ukombozi iliyotumiwa na wapigania uhuru kama lugha ya mafunzo na mawasiliano wakati wa kupigania uhuru kusini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, chini ya Uenyekiti wa Tanzania, ajenda ya viwanda imetekelezeka kwa nchi wanachama kupata uwezo wa kutengeneza dawa zenyewe baada ya mataifa mengi duniani kuzuia dawa zisitoke nje ya nchi zao kutokana na mahitaji kuongezeka katika kudhibiti Covid-19 na nchi za SADC zilitengeneza vitakasa mikono, barakoa, mashine za kupumua na vifaa mbalimbali vilivyohitajika.

Alisema ni katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, Tanzania imefanikiwa kuingia katika nchi za uchumi wa kipato cha kati, miaka mitano kabla ya lengo lake.
 
AKABIDHI TU AMETUUMBUA NA KUTUTILIA AIBU VYA KUTOSHA. ILIKUWA NI KAMA PICHA TU. MTU GANI HUWEZI HATA KUKAA NA WENZAKO MKAJADILI MAENDELEO NA DIPLOMASIA?
 
Moja ya maeneo muhimu na kipaumbele cha SADC ni ulinzi na usalama, katika mwaka mmoja wa kipindi chetu tumeimarisha usalama, ikiwemo kusimamia kumaliza migogoro ya Congo na kwingine, nawapongeza Wananchi wa Lesottho kwa kufikia makubaliano ya amani

Tumeboresha pia uchumi ikiwemo kuziimiza Nchi zote zilizopo SADC kuanzisha na kuendeleza viwanda, katika mwaka mmoja uliopita tumesimamia uandaaji wa ajenda za maendeleo ya Jumuiya yetu, katika kipindi cha Uenyekiti wetu tumeandaa dira ya maendeleo ya SADC ya mwaka 2050

Naishukuru Timu ya Sekritarieti kwa ushirikiano walionipa, namshukuru Waziri Kabudi kwa kuongoza kikao cha Mawaziri wa SADC, Jumuiya yetu mwaka huu imetimiza miaka 40 tangu ilipoanzishwa 1980, idadi ya Nchi wanachama imeongezeka kutoka Nchi 9 waanzilishi hadi Nchi 16

Ninayo furaha kubwa ya kukabidhi Uenyekiti wa SADC kwa Ndugu yangu ambaye ni Rafiki mkubwa wa Tanzania Rais wa Msumbiji, Nyusi nina uhakika atatoa mchango katika kushughulikia changamoto zilizopo kwenye Jumuiya yetu, Tanzania tunaahidi kumpa Mwenyekiti mpya ushirikiano

====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Agosti, 2020 amekabidhi uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi baada ya kuongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika mkutano wa 40 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao kwa kuwaunganisha viongozi wakuu 16 kutoka nchi wanachama ambapo Mhe. Rais Magufuli amekabidhi uenyekiti akiwa Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Jamhuri ya Botswana Mhe. Mokgweetsi Masisi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ) na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Matemela Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ.
 
Back
Top Bottom