Tetesi: Rais Magufuli kufuta ubunge viti maalum, ni kwa kurejesha mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Ikiwa ni kuondokana na gharama zisizo za msingi, serikali ya Magufuli inasemekana iko tayari kuanza mchakato wa katiba mpya kwa kuanza kuleta upya mapendekezo ya tume ya jaji Warioba yaliyotupiliwa mbali awali. Ambapo pamoja na mambo mengine ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima wabunge wa viti maalum hawatakuwepo, kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba..

"Wabunge hawa wa viti maalum hawana kazi wanayofanya zaidi ya kuliingizia taifa hasara" Dr. Bana alipoulizwa kuhusu mapendekezo ya Warioba kurudiwa upya

Pamoja na hilo, Rais pia kadhamiria kurudisha miiko ya uongozi kama moja ya njia ya kurudisha nchi katika misingi ya uwajibikaji na uzalendo....

Mytake: Rais Magufuli kama unataka ubaki katika historia ya nchi hii, basi tunaomba utuletee upya mapendekezo ya Jaji Warioba...
 
Miongoni mwa vitu muhim sana ili kuirudisha nchi hii katika msitari stahiki ni kurudisha miiko ya uongozi kuwa sheria kamili. Hii itatusaidia huko mbeleni atakapokuja Rais ambaye hana utashi wa kupambana na wezi na wala rushwa
 
japokuwa wabunge wengi wa viti maalum ni uwezo wao ni mdogo na wanachangia kwa emotions zaidi kuliko reason, siungi mkono kufutwa kwao, labda wangepunguza idadi sio kufuta, na madiwani pia......Wanawake wasshirikishwe kwenye siasa wakuu wana mchango mkubwa sana kwa jamii
 
viti maalumu ni chaka la viongozi wa vyama kuwabeba watu wasio na sifa hata chembe ya kuwa wabunge samahan kwa wale wanaopata nafasi hizo kwa uwezo na sio kubebana. Najiuliza hivi inakuwaje mtu kama Mukya na yule mkwe wa Ndesambulo walipata nafasi ya kuwa wabunge wa viti maalum alafu mtu kichwa kama mama Anna Mghwira akakosa
 
viti maalumu ni chaka la viongozi wa vyama kuwabeba watu wasio na sifa hata chembe ya kuwa wabunge samahan kwa wale wanaopata nafasi hizo kwa uwezo na sio kubebana. Najiuliza hivi inakuwaje mtu kama Mukya na yule mkwe wa Ndesambulo walipata nafasi ya kuwa wabunge wa viti maalum alafu mtu kichwa kama mama Anna Mghwira akakosa
Lumumba wanataka kutuondoa kwenye hoja ya Jessica!!
 
Magufuli mguu nje mguu ndani...kama dish vile!! Mengi mazuri mengi maovu!!
 
Hiyo ni tetesi tu ambayo imeletwa na mtoa mada,halijadhibitishwa na hata kama likipita si kwa kipindi hiki ila itakuwa ni kwa mwaka 2020.
 
Back
Top Bottom