Rais Magufuli jifunze kuwa vetting ni muhimu sana kabla ya kugawa cheo

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Leo nakuomba sana sana ukumbuke kuwa wale wapinzani wote mliowanunua na kuwapa mavyeo au kuwashindisha kwenye uchaguzi wa marudio hawakuwa wamefanyiwa vetting ama ya kiserikali ama ya kichama. Mngekuwa mmewafanyia vetting watu kama akina Protabas Katambi, Kafulila, Cecil Mwambe, Karanga, Mollel, Mtulia, Mtela Mwampamba, n.k. mngeona kabisa hawafai kuwa viongozi wazuri.

Sikatai wapo ambao ni wazuri kama akina Mtatiro, Kitila Mkumbo, Juliana Shonja, n.k lakini hao angalau kuwafahamu ilikuwa ni rahisi kutokana na kazi walizokuwa wakizifanya.

Mtatiro alikuwa ni Mwandishi mzuri wa Makala Gazeti la Mwananchi na katika kumsoma hakuwa na upendeleo uliokuwa ukijitokeza wa wazi, Shonja alikuwa ni mdada mzuri kumcontain ilikuwa rahisi tu.

Kitila Mkumbo alikuwa Mwalimu wa Chuo na tabia zake zilijulikana tangu awali ingawa ukweli naye ana tamaa sana ya madaraka pamoja na kuwa tamaa yake hiyo haina madhara.

Rais wangu akina Protabas na wenzake wamekuchafulia sana, hawafai hao. Jamii yote inaona wamekosea sana kujaribu hata kuchukua fomu - kwa nini wasingesubiri tu wabaki na nafasi ulizowapa. Walichukulia ni rahisi rahisi kupata mavyeo kupitia siasa.

Uliwaacha watu wako kwenye chama walio wanyenyekevu na wavumilivu kwa muda mrefu na vetting zao zipo wazi kabisa ukawakimbilia wale wapinzania kwa kuwanunua na kuwagawia mavyeo bila hata vetting ili kudhoofisha upinzani - sasa majibu unayapata kutoka kwa wananchi.

Pls usirudie kosa la hivyo. Kuna watu wa CCM hawatakupa kura kwa sababu uliwaacha ukawakimbilia watu wenye ulafi wa madaraka!
 
Hii inaonyesha wazi kuwa zile chaguzi za marudio zilikua total wastage of resources! Hakukua na uchaguzi zaidi ya uchafuzi.

Leo hii hakuna mwana ccm hata mmoja aliyewapa pole kwa kuangukia pua! Hii pia inapeleka meseji mbili kubwa.

Kwanza, hawakubaliani na walichokifanya wakubwa wao I mean viongozi wao
Pili, Wanachama wana nguvu kuliko Mwenyekiti wao anavyodhani na kwamba wanaweza kuamua chochote kile na kikawa tofauti na Mwenyekiti anavyodhani
 
Hili nililisikia sehemu kuwa anawapa watu vyeo just because wanamsifu au wanajipendekeza kwake. Kuna mahali nilisikia Kuna mdada amemteua kuwa Jaji hajui hata kuandika hukumu. Siku hizi hakuna cha vetting we jitoe ufahamu kumsifia tu anakupa cheo.
 
Back
Top Bottom