Kabla ya Rais Magufuli, Tanzania haikuwa inajulikana sana. Sasa hivi inajulikana kila pembe ya Dunia

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
KABLA YA JPM, MZUNGU ALIULIZA, WHERE IS TANZANIA, I NEVER HEARD OF IT, BAADA YA JPM, MZUNGU ANASEMA, I KNOW TANZANIA, IS SO BEAUTIFUL, I KNOW PRESIDENT MAGUFULI TOO!.

Leo 14:30pm 31/05/2020

Nikushukuru ewe Mungu Mwenyezi unayetujalia afya njema na uhai, kutupigania dhidi ya kila baya linalokuja mbele yetu. Hakika neno lako ni kweli tupu kwamba anayekuamini utamlinda na kumuongoza,

Kama lilivyo katika Zaburi: 118 tunakushukuru ewe Mwenyezi Mungu kwa kuwa ni mwema na fadhili zako ni za milele,katika shida zetu tulikuita Bwana,ukatujibu ukatuweka panapo nafasi,

Uko upande wetu hatutoogopa, mwanadamu atatutenda nini? Wanaotuchukia wameshindwa ni heri kukukimbilia wewe Ewe Mwenyezi Mungu,kuliko kuwatumainia wanadamu,

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu,nikupongeze sana Rais wetu John Pombe Magufuli kwa kuwa mtii na mwenye imani kwa Mwenyezi Mungu,while every other senses contradicted the fact,you believed in God,God will reward you a Leadership and Management with a difference,

Umeongoza mapambano makali kwa wingi wa hekima, utashi, maono, Utambuzi na Ustadi mkubwa dhidi ya Virusi vya Corona (Covid-19). Hakika, kama dereva wa gari (Tanzania) umekuwa dereva mwema sana mpaka sasa.

Hakika safari yetu katika vita hii imekuwa safari yenye ulinzi wa Mungu,Uponyaji wa Mungu,utetezi wa Mungu,Umetutoa hofu na kutupa faraja,umefanyika baraka nyingi sana zenye kuleta matumaini kwa kila Mtanzania.

Kwa kumtumaini Mungu katika kipindi hiki kigumu kwa ulimwengu mzima, umesimama imara sana kuongoza Taifa letu la Tanzania ,huu ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa kila mwanadamu hapa duniani katika nafasi aliyopo na hakika umemtumaini Mungu mwanzo hata Mwisho na umevishinda vita,

Ni Mungu mwenyewe awezaye kukulipa kwa kutushindia Vita hii ya virusi vya corona. Wapo waliopendekeza tufungiwe ndani kama kuku bila kujali uchumi wa mtanzania mmoja mmoja, huku wakitabiri mabaya juu yako na Taifa letu la Tanzania.

Kupitia wewe kama ilivyo katika Habakuki 2:1-3 tulimtumaini Mungu ulisimama imara katika zamu yako,ukajiweka juu ya mnara na kuiandika njozi na kuifanya iwe wazi sana katika vibao,katika njozi ndipo yalipo maono ya wapi Taifa linapaswa kwenda,Wewe ndiwe mbeba maono,Maono yetu umeyabeba wewe tu mteule na sio wengine.

Kuna wakati watesi walitegemea kuwa utayumba katika mapambano haya, lakini mpaka sasa hawaamini kinachoendelea hapa Tanzania. Kama dereva mzuri, haukusikiliza kelele za wapigadebe ambao mara zote hawatembei na gari,

Ahsante kwa kuitendea haki taaluma yako ya Kemia ukiwa mbobezi mwenye PhD katika Kemia uliangalia taaluma yako na dhamira yako ya ndani ya kuwaletea maendeleo Watanzania kisha ukaifuata.

Kwetu sisi “Waluguru” tunaamini katika mambo makubwa hata kumake statement duniani na daima tunasimamia kile tunachokiamini bila kuyumbishwa na kelele za wapiga debe kitu ambacho nimekiona kwako pia mpaka nikahisi uenda ukawa wa ukoo wetu wa Waluguru.

Ni dhahiri kabisa kwamba unafanya kazi kwa nguvu sana kuwapigania Watanzania wanyonge na wale waliodharaulika.

Ni mengi umefanya kwa ajili yetu hakika unastahili pongezi. Kuinua uchumi wa familia ukiachilia mbali wa taifa zima, lazima kukutana na migogoro ilihali ni kwa manufaa ya familia moja hii inasababishwa na utofauti katika utashi.

Kadharika, kuupambania uchumi wa taifa ni kazi ngumu sana inayotaka kujitoa maana yawezekana unayoyaona hawayaoni unaowaongoza na sio dhambi kuwaburuza mpaka wafike pale unapotaka wafike maana hata Wayahudi hawakujua kuwa Yesu amekuja kuwakomboa, mpaka pale alipokufa na kufufuka ndipo walipata kuamini japo wapo wengine mpaka sasa hawaamini.

Mpambano dhidi ya COVID-19 ni mapambano ya kiuchumi kuliko hata ugonjwa wenyewe. Kelele nyingi za nje dhidi ya Tanzania ni kuona kwamba shughuli za kiuchumi bado zinaendelea na watu wanachapa kazi ilihali wengine wamewafungia watu wao ndani na wameharibu kabisa Uchumi wao,

Katika hili, tunapambana vita mbili kwa wakati mmoja ambako vyote hakika tumeshinda. Ulifanyika Mussa kuwavusha wana wa Israel katika bahari ya Sham na kuwatoa utumwani Misri kuwapeleka kanaani kwenye nchi ya maziwa na asali.

Daima usisikilize kelele zao maana hata wao hawajui njia ya kuelekea kule wanakopelekwa bali wewe uliyetumwa kuwafikisha kule waendako. Yamkini wapo wanaofahamu njia na wapi wanapelekwa, lakini ukiwa kama Mussa si budi kuwapitisha kule ulikoelekezwa na Mungu hata kama kuna vikwazo.

Kipimo cha Uongozi bora sio kiwango cha maneno mazuri ambayo kiongozi atayazungumza ili apendwe na Wananchi,bali kipimo cha Uongozi bora ni matokeo chanya katika kuyabadilisha maono na ndoto za Wananchi kuwa kweli,

Umenipa faraja sana Mh Rais kuona uki ‘walk the talk’ hata baada ya watu kusema nguvu ya soda,povu tu, Actually it is no talk ni vitendo sana,Ni historia yako hii tangu na tangu ukiwa Waziri na Mbunge.

Thank you for basing your administration on rolling back the clock in Mwalimu Nyerere's basic principles.

You are widely praised for your open war against corruption and lethargy in the public service, and prison buses filled with former public officials became a familiar sight on Dar es Salaam’s streets as soon as you assumed the power,

You slapped Acacia Mining, a subsidiary of the world’s biggest gold mining company, with a historic tax bill, and launched a failed attempt at getting rid of cartels in the country’s potentially lucrative cashew nut sector,

On your first working day as president,You marched to the Finance ministry and redirected an important public ceremony’s celebrations to the anti-cholera program.

You also moved funding from a Worlds AIDs day event to anti-retroviral drugs, as part of his widespread austerity measures that involved cutting your salary and government spending, thank so much for patriotism for our country Tanzania.

In 2016, You famously visited your wife Mama Janeth in the country’s biggest hospital Muhimbili, winning praise for your confidence in the public health system.

Mwaka 2015 katika kampeni za uchaguzi Chama Cha Mapinduzi hakikuhitaji kutumia nguvu kumnadi Daktari John Pombe Magufuli kwa kuwa alikuwa mwenzetu,

Daktari John Pombe Magufuli ni kielelezo Cha Mwananchi mnyonge,nembo na alama ya Mwananchi wa hali ya chini,Daktari John Pombe Magufuli ni sauti ya mtu Masikini ambaye alizibwa mdomo na matajiri,

Kimsingi,CCM haikuhitaji kuwashawishi wanachama wake kumuunga mkono Daktari John Pombe Magufuli kwa sababu alikuwa mwenzao,

Daktari John Pombe Magufuli aliungwa mkono na takribani wana CCM wote waliomuunga mkono muda wote,kwa kuwa ndiye mtu sahihi kwa wakati sahihi kuleta mabadiliko halisi ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla.

Daktari John Pombe Magufuli ndiye mtu sahihi kuahidi mabadiliko ndani ya CCM na Taifa,kwa historia na utendaji kazi wa Daktari John Pombe Magufuli bila kuwa na tuhuma za kifisadi,utekelezaji wa miradi mikubwa iliyoshindwa kutekelezwa tangu tupate Uhuru,ndiye mtu sahihi kwa Sasa hapa Tanzania.

Kimsingi tatizo la CCM lilikuwa ni ukosefu tu wa nia ya kufanya mabadiliko kusudiwa kwani uwezo na sababu zilikuwepo,

-Hotuba ya kwanza ya kihistoria ya Rais Daktari John Pombe Magufuli,bungeni Dodoma.

Moja ya vitu vilivyonivutia sana katika hotuba ile ni jinsi Rais Daktari John Pombe Magufuli alivyoweza kujibu swali ambalo kwa miaka kadhaa lilionekana kuwatatiza viongozi wetu mbalimbali,

Kwa nini Tanzania ni Masikini licha ya utajiri lukuki wa rasilimali ilionao!?

Daktari John Pombe Magufuli alieleza bayana na kwa kirefu jinsi ufisadi,rushwa na uhalifu vilivyochangia kukwamisha Maendeleo ya Taifa letu,

Daktari John Pombe Magufuli alifafanua kwa kutumia takwimu halisi,jinsi mabilioni ya fedha yalivyotumika visivyo na matumizi yasiyo muhimu na yaliyo nje ya uwezo wa Taifa letu Masikini,

Kwa hakika hotuba ile ya Rais Daktari John Pombe Magufuli pale Bungeni Dodoma ilikuwa hotuba ya kihistoria iliyopiga vita kabisa utovu wa nidhamu wa hali ya juu uliokuwa ukifanywa katika awamu zilizopita na kutoa mwelekeo mpya wa Tanzania mpya ya Uchumi wa kati,kuboresha miundo mbinu ya nishati ya Umeme na usafiri na kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Wapinzani hawakubaki nyuma,kwao sio rahisi kuridhishwa,baadhi ya wapinzani waliosikiliza hotuba ile walidai kuwa eti haina tofauti na hotuba nyingine kadhaa zilizokuwa nzuri kuzisikiliza lakini zikaishia kuwa maneno matamu tu,

Wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa hata mtangulizi wake yaani Rais Mstaafu Kikwete naye pia alianza urais wake kwa hotuba za kutia moyo kama hizo lakini mengi ya aliyoahidi ,hususani lile la "Maisha bora kwa kila Mtanzania yaliishia kuwa ahadi tu.

Sikukubaliana kabisa na ukosoaji huo,wakosoaji hao hoja zao zinaweza kuwa na mantiki kidogo,kutokana na ombwe la wanasiasa wengi kupenda kuongea vitu vizuri,masikioni mwa watu,pasipo kuvitimiza wala kuwa na njia ya kutimiza,

Ni kweli kwamba ukosefu wa hotuba za kuvutia si moja ya matatizo yanayoikabili nchi yetu,wengi wa wanasiasa na viongozi wetu ni mahiri sana kwa maneno lakini tatizo huwa katika kutafsiri maneno yao kuwa vitendo.

Wakosoaji hao hawakuwa sahihi kwa sababu hotuba hiyo ilikuwa ya kutoka moyoni mwa Daktari John Pombe Magufuli na haikuhitaji "rocket science" kubaini hiyo ilikuwa hotuba ya Kiongozi anayeguswa na yanayoisibu nchi yake,

Daktari John Pombe Magufuli ni kiongozi mwenye uelewa wa changamoto zinazoukabili Uongozi wake,na mwenye dhamira thabiti ya kukabiliana na changamoto hizo.

Kuna mbinu moja muhimu ya kubaini iwapo mtu anaongea ukweli au anahadaa,nayo ni kumwangalia usoni,Tangu kuanza kwa kampeni zake za urais hadi wakati wa hotuba yake ya kwanza bungeni,Dodoma.

Uso wa Daktari John Pombe Magufuli wakati anaongea ulikuwa ukionyesha bayana kuwa kila neno linalotoka mdomoni mwake ni la dhati,linatoka moyoni na si sehemu ya porojo tulizozowea kutoka kwa wanasiasa,

Mtaalam yeyote wa kubaini ukweli na uongo hatoshindwa kubaini uthabiti wa kauli za Rais Daktari John Pombe Magufuli,Uthabiti upo wazi kwa yeyote anayemwangalia usoni wakati anaongea.

Nimalizie kwa Wazo la leo,

Americans before JPM: Where are they from

Tanzanian: Tanzania

Americans: Where's that? I never heard of it.

Americans after JPM: where are you from?

Tanzanian: Tanzania

Americans after JPM: Yeah I know Tanzania is so beautiful,I know President Magufuli too.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
for the wrong reasons of course.

kila mtaa niliowahi kuishi maishani mwangu, watu niliokuta wapo maarufu hapo mtaani ni wale ambao utakuta ni wezi, wagomvi, vijana wahuni na wasichana malaya.

that speaks volume about the so called "Tanzania popularity" under the current (5th) regime.
 
Nimeishi Thailand miaka miwili iliyopita . Nakuhakikishia 99% hawaijui Tanzania. Angalau Kwa percentage mdogo Kenya inajulikana
 
Kabla ya Rais Magufuli, Tanzania haikuwa anajulikana sana. Sasa hivi inajulikana kila pembe ya Dunia
Haya ndiyo matatizo ya kuzaliwa kwenye mikesha ya mwenge baada ya CCM kuzaliwa mwaka 1977.

Kuna wakati Tanzania ilijulikana kama kisiwa cha Amani si barani Afrika tu bali duniani na watalii walipigana vikumbo kukitembelea kisiwa hicho

Kuna wakati mwakilishi wa Tanzania akiongea kwenye mkutano wa UN wawakilishi wa mataifa yote hupigana vikumbo kusikiliza masimamo wa Tanzania.

Kuna wakati umoja wa Afrika (OAU) kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ulisubiri msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tamko la Rais wake.

Kuna wakati Mtanzania hakuhitaji viza kuingia nchi zilizokuwa za Jumuiya ya Madola, nchi nyingi za Ulaya na Asia, na ulipotua katika nchi hizo hukupekuliwa.

Kuna wakati nchi nyingi za Afrika ziliiona Tanzania kama mfano wa kuigwa na miji mingi mikubwa ilikuwa na barabara zilipopewa jina la Rais wa Tanzania.

Kuna wakati wapigania uhuru kutoka nchi mbali mbali ya Afrika waliweka kambi nchini Tanzania na waliitegemea Tanzania kwa misaada ya hali na mali.

Kuna wakati viongozi wa nchi zilizoendelea walipigania fursa ya kuitembelea Tanzania wakiwa tayari kutoa misaada ya kimaendeleo na kiuchumi.

Kuna wakati watoto wengi waliozaliwa ndani na nje ya Tanzania walipewa jina la aliyekuwa Kiongozi wa Tanzania kwa jinsi lilivyojulikana na lilivyoheshimika.

Kuna wakati viongozi wa mashirika ya fedha ya kimataifa katika kutimiza majukumu yao kwa nchi mbali mbali walitafuta kwanza ushauri wa uongozi wa Tanzania.

Kuna wakati kiongozi wa Tanzania alipotembelea nchi yoyote ile alitunukiwa vyeti vya heshima na wananchi wa mataifa hayo kujitokeza kwa mamilioni kumlaki.

Kuna wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na heshima kama taifa na wananchi wake waliona fahari kujitambulisha kama raia bila kusita wala kuona aibu.

Those were the days my friend...
...Those were the days, oh yes those were the days!
 
Haya ndiyo matatizo ya kuzaliwa kwenye mikesha ya mwenge baada ya CCM kuzaliwa mwaka 1977.

Kuna wakati Tanzania ilijulikana kama kisiwa cha Amani si barani Afrika tu bali duniani na watalii walipigana vikumbo kukitembelea kisiwa hicho

Kuna wakati mwakilishi wa Tanzania akiongea kwenye mkutano wa UN wawakilishi wa mataifa yote hupigana vikumbo kusikiliza masimamo wa Tanzania...
Mzee ulale. Usiweke uchungu moyoni..umri wako sio sawa na Mdude Chadema au Salary Slip. Utajiumiza bure
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom