Mchange
Senior Member
- Jul 21, 2009
- 158
- 325
VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA.
----------------------------------------------------------
Kwako Rais John Pombe Magufuli,
Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba na Viongozi wengine waandamizi wa serikali.
Watumiaji wakuu wa Dawa za kulevya za aina zote hapa nchini ni watanzania.
Wawe vijana, watu wazima wa makamo ama wazee kabisa lakini ni Watanzania.
Leo kelele zimeongezeka kwa sababu watanzania wenzetu hasa wanaotuburudisha katika Sanaa kama Chid Benz na wengine kuonekana unga umewasonga.
Nimemwona Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ameenda Nyumbani kwa Mama yake Mzazi Chid Benz. Pengine ameenda kumpa pole ama tu kumsabahi,
Nimeona pia waziri huyo ameshika tuzo za msanii huyo ambaye kwa sasa hakika amepotea.
Utafiti wangu mdogo unaonyesha kwamba hivi sasa Unga (Madawa ya Kulevya ) unauzwa kwa wingi kuliko kipindi kingine chochote hapa nchini, wauzaji wanauuza hadharani na wanunuzi pia wananunua na wanatumia hadharani.
Polisi wetu baadhi ya maeneo wamekuwa wakibishania malipo na wauzaji ili wadiwakamate.
Hili tatizo sio Dogo.
Tatizo la Dawa za Kulevya haliwezi komeshwa kwa watanzania kuendelea kulalamika bila kuchukua hatua.
Wala tatizo hili haliwezi kumalizika kwa waziri kusema kuwa :serikali ipo serious inapambana na unga na itawakamata wauzaji na waache Mara moja".
Iko Hivi.
Wauzaji wote wanaishi mitaani hapa nchini.
Wanunuzi na Watumiaji wote wanaishi mitaani hapa hapa nchini.
Wasio kuwa watumiaji nasi tunaishi humu humu mitaani.
Mitaa yote Na vijiji vyake vina wenyeviti wa Mitaa.
Mitaa yote na vijiji vyake vina wajumbe wa serikali za Mitaa na wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM, CHADEMA, ACT na vyama vinginevyo.
Kwa kifupi ni kwamba wauzaji na wanunuzi pamoja na wasiotumia wote wanajuana.
Watumiaji wanaishi huku mitaani.
Rais, anzisha Ambush. Mwenyekiti wa Mtaa ambaye mtaani Kwake kutakutwa Mateja waathirika wa unga, yeye na wajumbe wake wakamatwe na wafunguliwe mashtaka ya uhujumu uchumi.
Mwenyekiti wa Mtaa ambaye mtaani Kwake anaviona na kuvijua vijiwe vya kuuzia unga, bange na Dawa nyingine, wakamatwe na wafungwe kwa makosa ya kuhujumu uchumi.
Rais, wakamate wenyeviti wa Mitaa wote ambao wananchi wao wanawajua wauzaji wa unga na hawaripotiwi.
Wafukuze kazi askari wote wanaohongwa ili kuendelea kuacha wauzaji waendelee kuuza unga.
Huu unga hauuzwi hewani. Wanaouza tunaishi nao na wananunua kadharika.
Serikali iache sasa kulalamika. Ichukue hatua.
Hatua ni Viongozi wawakilishi wa chini huku mitaani kuwajibika.
Habib Mchange
Mwananchi