Rais Magufuli, ikimbie hasira ya Mungu

Rais Magufuli, ikimbie hasira ya Mungu

Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).

Umeandika sawa na mtu asiefikiria. Hata watu wote wangejiandikisha na wakapigia kura chama tofauti bado ccm watajitangaza kushinda. Unadai kuwa ccm wanachekelea watu kutojiandikisha sasa kwa nini Magufuli anatishia kuwaadhibu viongozi wa mikoa itakayokuwa na idadi ndogo ya waliojiandikisha? Ni aibu kwa ccm watu kususia uchaguzi maana inadhihirisha kutokukubalika kwao.
 
Kampeleke huyo aliyekuzaa akashangae terminal three, jitu jinga wewe
Hiuo terminal three ndo nn ziara ya jpm ulisikia habari ya terminal 3, SGR na Nyerere Dam kalazimiaha ndege tuone kama itarudi huko napenda iende ila abiria wako wapi
 
1570937082942.jpeg
 
wamepita hapa usiku huu wanatangaza tukajiandikishe...
ni kupoteza muda tu,magufuli ameua democrasia, miaka ya nyuma uchaguzi wa Serikal za mitaa unakuwa na shamra shamla,, uku nnapoishi upinzani wanaogopa kumtangaza hata mgombea wao maana wanaogopa policcm wasije kumteka pamoja na greenguard
 
Umeandika sawa na mtu asiefikiria. Hata watu wote wangejiandikisha na wakapigia kura chama tofauti bado ccm watajitangaza kushinda. Unadai kuwa ccm wanachekelea watu kutojiandikisha sasa kwa nini Magufuli anatishia kuwaadhibu viongozi wa mikoa itakayokuwa na idadi ndogo ya waliojiandikisha? Ni aibu kwa ccm watu kususia uchaguzi maana inadhihirisha kutokukubalika kwao.
Huwezi kuchukua dhana ya kususia uchaguzi katika mtazamo mmoja tu na kuhitimisha kuwa CCM haikubaliki.

Hivi unadhani kama kuna pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Hassan Mwakinyo kuna washabiki gani wengi wanaweza kwenda kununua tiketi wakati wanajua mshindi. Kutokununua tiketi katika pambano hilo hakuna umaana kuwa Floyd Mayweather hakubaliki bali washabiki wanajua matokeo ya pambano.

Kwa mantiki hii, Hata kama mashabiki hawatahudhuria pambano lakini Floyd Mayweather atakuwa ameishapata pesa yake kutoka kwa waandaaji wa pambano.

Hoja yangu ina maana kuwa hata kama wapiga kura wengi hawatajiandikisha, CCM watakuwa wameishapata kile wanachokitafuta ambacho ni madaraka kwenye Merikali za Mitaa.
 
Hali si hali uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Nipo countryside huku watu hawana mwamko, mabalozi wa nyumba kumi (CCM) wenyeviti wa vitongoji na wenyeviti wa vijiji wanapita kuhamasisha ila watu hawataki, kuna bibi ni CCM damu damu ila amesikika akisema, namnukuu "nani aende kupoteza muda wake, viongozi tunaowataka mnawakatalia mbali kwa kuwaibia kura au kuwapoteza"

Shime tujitokeze kujiandikisha, maana tusipojiandikisha twajikomoa wenyewe, hatumkomoi yeyote yule.

Kupiga kura ni muhimu na kunampa mtu haki ya kuamua kuchagua mtu sahihi hata kama hatochaguliwa
hata walete wadada wa kiiraq(Wambulu) Kutushawishi,sinyanyui mguu wangu
 
Huwezi kuchukua dhana ya kususia uchaguzi katika mtazamo mmoja tu na kuhitimisha kuwa CCM haikubaliki.

Hivi unadhani kama kuna pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Hassan Mwakinyo kuna washabiki gani wengi wanaweza kwenda kununua tiketi wakati wanajua mshindi. Kutokununua tiketi katika pambano hilo hakuna umaana kuwa Floyd Mayweather hakubaliki bali washabiki wanajua matokeo ya pambano.

Kwa mantiki hii, Hata kama mashabiki hawatahudhuria pambano lakini Floyd Mayweather atakuwa ameishapata pesa yake kutoka kwa waandaaji wa pambano.

Hoja yangu ina maana kuwa hata kama wapiga kura wengi hawatajiandikisha, CCM watakuwa wameishapata kile wanachokitafuta ambacho ni madaraka kwenye Merikali za Mitaa.
Mawazo haya hayana mashiko
 
You are deliberately missing my point. Kwa mtu mwenye kutumia akili yake anajua kuwa hakuna uchaguzi isipokuwa ni uharamia ("chaguzi" ndogo Kinondoni na kwingine zilidhihirisha hilo). Kwa nini mtu aende kuhalalisha huo uharamia? Kwa manufaa ya nani?
On the other hand, ccm wanahitaji watu wengi kiasi cha kutosha ili kuhalalisha uharamia wao, kutopatikana kwa idadi ya kutosha ni aibu kwao. Mfano wako wa Mayweather ni irrelevant in this case kwa kuwa umaarufu alionao sio wa kulazimisha bali ni self-evident.
Ingekuwa hoja yako ni sahihi basi Magufuli asingetokwa na povu hadharani kiasi hicho kwani hana cha kupoteza. Anajua HAKUBALIKI, period.
 
Watanzania wamekata tamaa. Wananchi wengi ukiongea nao utakachosikia, 'halafu bado tuna miaka mingine karibu 6 na mtu huyu'. Wengi wanatamani kipindi hiki kingekuwa ndiyo kipindi chake cha mwisho.

Wengi wanaamini kupiga kura ni kupoteza muda maana utawala wa awamu hii hauheshimu maamuzi ya wananchi. Wanachosubiri hasa ni amalize vipindi vyake viwili akapumzike, japo wanaona muda uliobakia ni mrefu mno.

Kwenye kuheshimu uhuru na haki za raia, utawala bora na ujenzi wa mifumo ya utawala bora, Rais Magufuli amewakatisha tamaa Watanzania wengi. Ameamua kuwa Rais wa ujenzi wa barabara japo kiuhalisia barabara zilizojengwa awamu hii hazifiki hata 25% ya zilizojengwa wakati wa awamu ya nne. Lakini matangazo ya mafanikio kidogo yamekuwa zaidi ya 1000% ya awamu zilizopita.

Awamu hii ilichozizidi awamu zote ni matangazo kuwa makubwa kila kunapokuwa na mafanikio kidogo.
 
Takataka
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
 
Rais wangu, hata wewe huwa unasema kwamba "msema kweli ni mpenzi wa Mungu " tenda haki ili uweze kujitenga na ghadhabu Mungu.
Mkuu Your Son Drink Water, kwa vile adhabu huletwa na karma, akitenda uovu na mabaya, atalipwa majanga, na akitenda wema, atalipwa neema na mafanikio, then ni binadamu na sio malaika, mema yake ni mengi kuliko mabaya yake, hivyo mema yakizidi mabaya, hivyo licha ya mabaya ulioorodhesha, lakini kwa mema yake ambayo ni mengi kuliko mabaya, then rais Magufuli atabarikiwa na Tanzania itabarikiwa.
P
 
Kwa staili hii mwakan wabunge wote watatokea chama tawala..
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
Ni mpumbavu pekee anayeweza kujipanga foleni kupiga kura wakati anajua fika somebody somewhere at location xyz is controlling the envisaged results. It is a simple definition of craziness....
 
Pamoja na kwamba ninaishi Australia, lakini wewe bado ni Rais wangu tu ,nipo hapa Australia kimwili tu, lakini kiroho nipo Tanzania.
Rais wangu, hata wewe huwa unasema kwamba "msema kweli ni mpenzi wa Mungu ".
Basi acha na mimi niseme kweli sasa ,Rais wangu Magufuli umezungukwa na kundi la watu wa ajabu kupindukia.
Urais ni taasisi, wewe Kama mkuu wa nchi umezungukwa na watu wa Kila aina, lakini kwanini yote haya yanatokea?
Wataalamu wa uchumi wapo tu wanaangalia? Wataalamu wa siasa na Diplomasia za kimataifa nao wapo tu wanaangalia?
Au pengine tatizo ni wewe labda hushauriki na sasa wameamua ni bora wakae kimya siku ziende.
Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nijikite tu na uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao wananchi wengi wameonekana kuususia na baada ya hapo wewe umeamua kuwabebesha msalaba wakuu wa mikoa kwamba kwanini watu hawajiandikishi ili kupiga kura.
Rais wangu, unataka wakuu wa mikoa wafanye nini juu ya hili? kwamba wananchi wakamatwe kisha wakajiandikishe na kupiga kura?..
Au wakuu wa mikoa waitishe mikutano kuwasihi na kuwabembeleza wananchi ili wajitokeze kupiga kura?
Wakuu wa mikoa wafanye nini ktk hili?
Umesema kwamba utawawajibisha endapo ktk mikoa yao wananchi hawatakuwa na mwitikio.
Hapa ndipo nimelazimika kukueleza Rais wangu uikimbie hasira ya Mungu.
Bahati mbaya zaidi, taifa la Tanzania halina watumishi shupavu wa Mungu, wanaoweza kusimamia kweli ya Mungu, nao wameingia Kwenye kundi la kusifia tu, hapana kukosoa.
Rais wangu, wewe ndo chanzo cha wananchi kukosa ari ya kushiriki uchaguzi, kauli zako huwa zinaegemea upande wa CCM tu na ni kauli za kibaguzi kabisa.
Hizi ni baadhi ya kauli zako za kibaguzi...
1."Ninakulipa mshahara, nimekupa gari halafu unatangaza mpinzani kashinda ".
2."Ole wake yoyote atakayempiga mtu aliyevaa kijani(CCM)
(Hapa ulipaswa kusema, Ole wake yoyote atakayempiga mtanzania)
3.CCM itatawala milele (Hakuna atawalaye milele zaidi ya Mungu)
Kwa kauli Kama hizo ,watu wameona kuwa wanapoteza muda bure kwa sababu washindi wanajulikana .
Rais wangu, ktk hilo wakuu wa mikoa watafanyeje ?.
Tenda haki ili uweze kujitenga na ghadhabu Mungu.
Umesema kweli yote na kamwe asitafutwe mchawi
 
Back
Top Bottom