Rais Magufuli, ikimbie hasira ya Mungu

Rais Magufuli, ikimbie hasira ya Mungu

1."Ninakulipa mshahara, nimekupa gari halafu unatangaza mpinzani kashinda ".

2."Ole wake yoyote atakayempiga mtu aliyevaa kijani(CCM)

3.CCM itatawala milele

Kuna mambo yanasikitisha sana...

Cc: mahondaw
 
Pamoja na kwamba ninaishi Australia, lakini wewe bado ni Rais wangu tu ,nipo hapa Australia kimwili tu, lakini kiroho nipo Tanzania.
Rais wangu, hata wewe huwa unasema kwamba "msema kweli ni mpenzi wa Mungu ".
Basi acha na mimi niseme kweli sasa ,Rais wangu Magufuli umezungukwa na kundi la watu wa ajabu kupindukia.
Urais ni taasisi, wewe Kama mkuu wa nchi umezungukwa na watu wa Kila aina, lakini kwanini yote haya yanatokea?
Wataalamu wa uchumi wapo tu wanaangalia? Wataalamu wa siasa na Diplomasia za kimataifa nao wapo tu wanaangalia?
Au pengine tatizo ni wewe labda hushauriki na sasa wameamua ni bora wakae kimya siku ziende.
Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nijikite tu na uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao wananchi wengi wameonekana kuususia na baada ya hapo wewe umeamua kuwabebesha msalaba wakuu wa mikoa kwamba kwanini watu hawajiandikishi ili kupiga kura.
Rais wangu, unataka wakuu wa mikoa wafanye nini juu ya hili? kwamba wananchi wakamatwe kisha wakajiandikishe na kupiga kura?..
Au wakuu wa mikoa waitishe mikutano kuwasihi na kuwabembeleza wananchi ili wajitokeze kupiga kura?
Wakuu wa mikoa wafanye nini ktk hili?
Umesema kwamba utawawajibisha endapo ktk mikoa yao wananchi hawatakuwa na mwitikio.
Hapa ndipo nimelazimika kukueleza Rais wangu uikimbie hasira ya Mungu.
Bahati mbaya zaidi, taifa la Tanzania halina watumishi shupavu wa Mungu, wanaoweza kusimamia kweli ya Mungu, nao wameingia Kwenye kundi la kusifia tu, hapana kukosoa.
Rais wangu, wewe ndo chanzo cha wananchi kukosa ari ya kushiriki uchaguzi, kauli zako huwa zinaegemea upande wa CCM tu na ni kauli za kibaguzi kabisa.
Hizi ni baadhi ya kauli zako za kibaguzi...
1."Ninakulipa mshahara, nimekupa gari halafu unatangaza mpinzani kashinda ".
2."Ole wake yoyote atakayempiga mtu aliyevaa kijani(CCM)
(Hapa ulipaswa kusema, Ole wake yoyote atakayempiga mtanzania)
3.CCM itatawala milele (Hakuna atawalaye milele zaidi ya Mungu)
Kwa kauli Kama hizo ,watu wameona kuwa wanapoteza muda bure kwa sababu washindi wanajulikana .
Rais wangu, ktk hilo wakuu wa mikoa watafanyeje ?.
Tenda haki ili uweze kujitenga na ghadhabu Mungu.
Mr.haambiliki!
 
Umefeli mno na huo mfano wako maana Magufuli alisharopoka akulipe mshahara halafu umtangaze mpinzani mshindi..! Ni aibu mno kwa Magufuli na ni mpuuzi.
Huwezi kuchukua dhana ya kususia uchaguzi katika mtazamo mmoja tu na kuhitimisha kuwa CCM haikubaliki.

Hivi unadhani kama kuna pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Hassan Mwakinyo kuna washabiki gani wengi wanaweza kwenda kununua tiketi wakati wanajua mshindi. Kutokununua tiketi katika pambano hilo hakuna umaana kuwa Floyd Mayweather hakubaliki bali washabiki wanajua matokeo ya pambano.

Kwa mantiki hii, Hata kama mashabiki hawatahudhuria pambano lakini Floyd Mayweather atakuwa ameishapata pesa yake kutoka kwa waandaaji wa pambano.

Hoja yangu ina maana kuwa hata kama wapiga kura wengi hawatajiandikisha, CCM watakuwa wameishapata kile wanachokitafuta ambacho ni madaraka kwenye Merikali za Mitaa.
 
Hata nikitoka lazima niwe na return ticket
Siwezi kuishi kwa mabeberu Mimi

Kule ni kuzuri kwa mazingira ya nje tu lkn maisha ya kishetani mno
Maisha ya kishetan anayapenda jiwe ndio watanzania wengi tunaishi sio ulaya wew kenge
 
Mkuu Your Son Drink Water, kwa vile adhabu huletwa na karma, akitenda uovu na mabaya, atalipwa majanga, na akitenda wema, atalipwa neema na mafanikio, then ni binadamu na sio malaika, mema yake ni mengi kuliko mabaya yake, hivyo mema yakizidi mabaya, hivyo licha ya mabaya ulioorodhesha, lakini kwa mema yake ambayo ni mengi kuliko mabaya, then rais Magufuli atabarikiwa na Tanzania itabarikiwa.
P
Karma karma till when mzee acha hizi mambo

Tunapotea hafu unaleta story za karma

Kama Taifa tumepoteza mwelekeo!

Sio kwa vyama vya upinzani wala tawala kote anii
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
Jidanganye kuwa huumwi jino...kila mtu ana kinywa chake. Kama wapinzani ndio wanapata hasara, mbona malalamiko yanatoka kwingine?

Asikwambie mtu, kama wewe ni cashier, mbeba zege akikususia ujira wake, hautakuwa na amani.
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).

Umeandika nini? Nadhani dhana uliyonayo ikihamia kati ya familia na familia au mtu na mtu ndipo utagundua ujinga unaoushabikia hapa. Sina interest na siasa lakini thinking za namna hii ni hatari kwa amani ya nchi
 
Leo nipo nyumbani nilipowaambia watoto zangu wawili ambao umri wao tayari kujiandikisha ,waende kwa jambo ,walinishangaa wakaniambia baba wewe siumebaki miaka michache usitaafu
 
Back
Top Bottom