ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
- Mamlaka ya ustawishaji wa mji wa dodoma kuvunjwa kwake hakujafanyiwa research ya kutosha. Kimsingi CDA imejitahidi sana kuondoa tatizo la migogoro tofauti na ilivyo kwa halmashauri nyingine. Watendaji wengi wa halmashauri wanafanya kazi kwa kutanguliza maslahi. wote humu jamvini tutakuwa mashahidi kwamba halmashauri nyingi za miji na majiji zina migogoro mikubwa ikiwa ni pamoja na watu kuuziwa viwanja mara mbili, watu kuuziwa maeneo ya open space na matatizo mengineyo mengi tu , Leo kuivunja CDA ina maana muda si mrefu tutaanza kusikia dodoma wakianza migogoro kama kinondoni, ilala na halmashauri nyinginezo, tutaanza kusikia maeneo ya wazi wameuziwa vigogo , nk . Dodoma haijawahi kuwa na matatizo makubwa kama yale yaliyokuwa kwenye halmashauri nyinginezo za miji na majiji .
- Nilitegemea kila halmashauri kungeanzishwa chombo kama hiki cha CDA ili kupunguza urasimu na migogoro kwenye halmashauri zetu, matokeo yake wamekivunja , hao wanao furahia kuvunjwa kwa CDA ni vema kujiuliza mara mbilimbili huenda ikawa CDA olikuwa kikwazo kwao kupiga madili ya viwanja. Muda si mrefu tutaanza kusikia kero na migogoro mbalimbali ikianza kuibuka dodoma