Rais Magufuli: Hakuna fedha za tetemeko kwenda Magereza. Wafungwa "watetemeke" kujenga magereza yao

kweli kabisa mkuu,sijui mkuu ataupata ujumbe wako muruwa kabisa,na kwa kuwa eneo hilo liko ukanda wa matetemeko,sidhani kama wafungwa watajua aina ya teknolojia ya kutumia
Ataupata tu! Ndio maana alisema "anatamani malaika waje wafungie mitandao japo kwa mwaka mmoja"! Ni wazi anadurusu sana mitandao ya kijamii kupata public opinion kuhusu mustakabali wa NJI yetu!
 
hapa ndipo unakuta ule msemo wa bora kuwa mbwa Ulaya kuliko mfungwa Tanzania
 
Huyu jamaa ni zaidi ya bulldozer! Hiyo sio kauli ya kuwafariji wahanga wa tetemeko.
Kwani kuna wafungwa waliojeruhiwa? Kama hakuna wajenge haraka ili wasiendelee kubanana kwenye vyumba vilivyoko. Ila vifaa vya ujenzi wapewe kutokana michango ya maafa kama wengine.
 
“Katibu Mkuu Kiongozi, hakuna kuwapelekea wafungwa wa Karagwe fedha yoyote, hizi za maafa ya tetemeko. Watetemeke na kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli na kuibua kicheko kwa watu waliohudhuria hafla hiyo.

Rais John Magufuli amesema Serikali haitajenga Gereza la Kitengule Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera lililobomoka kwa tetemeko la ardhi, badala yake ameliagiza Jeshi la Magereza liwatumie wafungwa kufanya kazi hiyo.

Alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga mazoezi ya kijeshi ambayo kitaalamu yanaitwa ‘amphibious landing’ yaliyofanyika Kijiji cha Baatini, Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Katika mazoezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kushuhudia wanajeshi wakilikomboa eneo lililotekwa na maadui ukanda wa majini, Rais Magufuli alimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kutopeleka fedha za maafa kujenga gereza hilo.


tumsubiri 2020 na sisi tumtetemeshe bila huruma.
 
hivi bati wafungwa watazitolea wapi? misumari,makoa,mbao,mabomba ya maji,waya za umeme,magrill?
si ndio maana wanaomba hela?
au.....??!!
Kweli. Hata kama wana nguvu kazi vifaa lazima wapewe. Pesa itayookolewa ni ile tu ya kulipa mafundi na vibarua. Kwa msaada wa vifaa ni lazima
I thought angewahimiza magereza na kuwapa mtaji wa kuwa na kampuni yao ya ujenzi na ufundi ambayo itauzia fenicha au kujengea serikali.Hili l
 
Duu kwa mtindo huu kunasiku wafungwa watalalia kitanda Kwel? just thinking....
 
Kuna tatizo hapa na tunaliona ila tumejifunika tu tusionekane tunaliona tatizo maana ukiliona na ukalisema basi wewe ni mtu mbaya..
1. Umaskini
2. Ujinga
3 . Maradhi
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Hapa nakuunga mkono 100% percent hatuwezi kulisha watu wahalifu ....
Na tuwajengee pa kulala wana uwezo wa kufanya hivyo hata chakula walitakiwa walime chao sio kulia lia budget......

Kwani si Mtanzania???
Yeye ni RAISI wa Watanzania wote. Kauli yake sijaipenda hata kidogo. Mfungwa anastahili haki Kama waathirika wengine WA tetemeko.
Kwani TETEMEKO alilileta yeye?
 
Hivi unajua ni pesa ngapi unakatwa kwenye mshahara wako kupelekewa hawa waarifu?

Fatilia magereza ya China wafungwa uwa wanaishi vipi
Nchi kama China, Vietnam, Russia, wafungwa ndo wanaofanya kazi hakuna kutegemea serikali kwa kila jambo
Hata hapa Tanzania miaka ya nyuma magereza kama kitengure , lilikuwa linazalisha chakula mpaka cha kuuza kupata hela , wana ng'ombe zaidi ya elfu 5 wana mifuko yao ya kuendesha shughuli zao, na mambo mbali mbali hivyo wajenge wao, na cement wanunue wenyewe,
 
Back
Top Bottom