Rais Magufuli azindua Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro, aitaka mifuko ya hifadhi kuwekeza kwenye viwanda badala ya majengo

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli anazindua kiwanda cha bidhaa za ngozi kilichopo mkoani Kilimanjaro. Rais ameshafika na kwa sasa ni wimbo wa Taifa kabla ya kuanza shughuli Rasmi. Kuwa nami.

======

TAARIFA FUPI YA MRADI

Mkurugenzi PSSF:
Ujenzi wa mradi huu ni utekelezaji wa maelekezo yako uliyoyatoa tarehe 9 May 2016 uliyoyatoa wakati wa ufunguzi wa majenga ya vitega uchumi wa mifuko ya hifadhi ya jamii jijini Arusha, katika hotuba yako ulituelekeza kuwekeza zaidi katika viwanda badala ya kuwekeza tu katika majengo.

Katika kutekeleza, May 2017 mfuko kwa kushirikiana na Jeshi la magereza tulianzisha kampuni ya ubia inayojulikana Karanga leather Industries company Limited ambayo kwa kwa sasa inajulikana kama Kilimanjaro International Leather Industries yenye mtaji wa bilioni 70 inamilikiwa na mfuko wa PSSF kwa asilimia 86 na Jeshi la Magereza kwa asilimia 14. Jeshi la Magereza likiwa limechangia eneo la kiwanda lenye ekari 25 pamoja na kiwanda cha zamani.

Mfuko wa PSSF unachangia gharama za ujenzi wa majengo, ununuzi wa mashine na mitambo na gharama za uendeshaji. Ujenzi huu unasimamiwa na wataalam wa ndani kupitia taasisi za umma.

Mkandarasi wa ujenzi ni Jeshi la Magereza kwa kiasi cha bilioni 27, mashine na mitambo vimenunuliwa nchini Italy kwa gharama ya Euro milioni 23.6, takribani bilioni 60 zikijumuisha gharama za usafirishaji, ufungaji wa mashine, mafunzo na ushuru wa forodha. Mpaka kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu bilioni 136.


MAGUFULI: Kuanzishwa kwa kiwanda hiki, mimi nina uhakika sasa baada ya mwaka mmoja, miwili tukikutana hata katika kusheherekea, nina uhakika tutakuwa tumevaa viatu vitavyokuwa vimetengenezwa hapa Kilimanjaro.

Wafungwa lazima watumike katika kuzalisha mali, ukifungwa lazima ukatumike vizuri ili ujutie makosa yako ili siku nyingine usifungwe tena na ukishatoka hapa utatoka umeshajua kuzalisha viatu akafungue kiwanda chako. Kufungwa ni sehemu ya mafunzo.

Nizipongeze pension fund zetu, PSSF na bodi yake pamoja na mkurugenzi mmeanza vizuri sana kwa sababu siku za nyuma pension fund zilikuwa zinawekeza kwenye majengo tu na kule ndiko kulikuwa na percentage nikasema masuala ya kuwekeza kwenye majengo uachwe.

Utakuta jengo limejengwa kwa mabilioni, wapangaji wapo nusu tu, faida yake ni ndogo.

Ukiwekeza kwenye viwanda faida yake ni kubwa. Kiwanda hiki kitakuwa kinatoa ajira ya watu elfu 3. Ungejenga jengo lisingetoa ajira ya watu 3,000 na hawa ni wale watakuwa wanafanya permanently hapa. Wale wengine watakaokuwa wanaleta vyakula, ngozi kwa nchi nzima unaweza ukajikuta umetengeneza ajira ya zaidi ya watu milioni 1.

==========

19B5EA6A-4A1C-49F2-837E-9CBDD9463F85.jpeg


Mwisho Rais Magufuli amezindua kiwanda na kununua viatu kadhaa ikiwemo vya Mke wa Askofu Shoo, mwandishi wa habari nk

Sho.jpeg
ShoMagu.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya viatu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo kwa ajili ya mke wake mara baada ya kumnunulia katika Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga Moshi mkoani Kilimanjaro jana mara baada ya kukizindu​
 
Nchi inatakiwa kiwanda vya aina mbali mbali tuwauzie watu products na sio raw materials ili tupate faida kubwa sawa jiwe! ila Lissu imekaa vizur inasound good.
 
PSSSF na NSSF wana pesa ya kufanya miradi, lakini pesa ya kumlipa mfanyakazi aliyetumikia Taifa na kchangia mifuko hiyo kwa miaka Mingi na badae kupoteza ajira na kuendelea kuteseka na familia yake, Hawana..!!

Hovyo sana....
 
PSSSF na NSSF wana pesa ya kufanya miradi, lakini pesa ya kumlipa mfanyakazi aliyetumikia Taifa na kchangia mifuko hiyo kwa miaka Mingi na badae kupoteza ajira na kuendelea kuteseka na familia yake, Hawana..!!
 
Kiwanda cha 202 ndani ya awam ya tano. Magufuli oyeeeeeeeee
Tuliambiwa kumejengwa viwanda zaidi ya elfu 6000 na pia mwaka jana tuliambiwa kila mkoa unatakiwa ujenge viwanda 100 kabya ya desemba. kwa maana hiyo mikoa 26 x 100 tunayo viwanda 2600. kwa mwaka jana tu. Sasa wewe unaturudisha nyuma tena kwenye viwanda 202
 
PSSSF na NSSF wana pesa ya kufanya miradi, lakini pesa ya kumlipa mfanyakazi aliyetumikia Taifa na kchangia mifuko hiyo kwa miaka Mingi na badae kupoteza ajira na kuendelea kuteseka na familia yake, Hawana..!!
Nyoosha maelezo , mara wana pesa mara hawana ... Hawara.
 
Gharama za mkandarasi MT = 27 bil
Gharama za machines = 60 bil

Total. 87 bil

+ + +

Usafirishaji, ushuru wa forodha, trainings

Total 136 bil...

Meaning around Tshs 50 bil zitatumika kwa shipping, customs taxes, trainings of personnel etc

PCCB cheki hiyo last 50 bil, nyingi sana sanaaaaaaa, something is clearly wrong here..!! That is too much money
 
Back
Top Bottom