Rais Magufuli hajawahi kuwa na Mpinzani

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
647
304
Ukweli usemwe tu. Kiutendaji, uwezo binafsi, ubunifu, uchapakazi, uzalendo ni vitu vinavyomuuza Rais Magufuli tokea awe mwanasiasa -- mbunge, waziri na sasa ni Rais

Rais Magufuli hajawai kuwa na mshindani katika kariba yake katika mambo hayo. Akiwa waziri katika wizara mbalimbali uwezo wake ulimuuza, hakuhitaji kuita vyombo vya habari na kusema yeye ni nani na anafanya nini, bali kazi zake na uwajibikaji vilimuuza.

Ni mtu asieyumbishwa, mwenye msimamo. Na huyu Watanzania walimuhitaji ndio maana wenye macho ya kizalendo, wanyonge wanaoipenda nchi yao wanatamani Rais Magufuli aongezewe muda sababu anajibu kero zao na kuzitatua kwa wakati.

Ukweli usemwe. Leo hata Watanzania tukiamua kujifanya hatuoni yakifayofanywa na Rais Magufuli ndani ya miaka miaka mitano, malaika watatujia ndotoni na kutuonesha yaliyofanywa na Rais Magufuli.

Tukijifanya hatuoni, tukipita katika flyover zitatukumbusha hii ni kazi ya Magufuli.

Tukijifanya hatusikii, zahanati, vituo vya afya kila kona, hospital za wilaya , hospital za kanda zitatuambia bila Magu, leo usingepata matibabu karibu na nyumbani kwako.

Tukijifanya hatusikii Watanzania wanyonge watamsemea na kutukumbusha Elimu bure imefanya watoto wengi wa masikini wawe shuleni.

Tukijifanya hatuoni ,wamachinga watatukumbusha Rais magufuli amerudisha thamani Yao na kuwafanya wafurahie nchi yao bila bugudha.

Rais Magufuli ni Baba lao

Kazi zilizofanywa na Rais Magufuli katika Taifa hili hazina mfano.

Tumpe MITANO TENA KWA KISHINDO.

WATANZANIA TUNAMPENDA Rais wetu ,Jembe letu ,anatupeleka katika Nchi ya Uchumi wa Kati , watanzania tuchape kazi

#Maliki,Malick
 
Hata akiwa waziri Chato hakupingwa. Wapinzani walikuwa hawarudishi form
 
Eti na wewe unautaka Ubunge wa Mtama, kwa mawazo haya kweli?

Jua basi kutofautisha kati ya hajawahi kuwa na mpinzani na kutotaka upinzani kutokana na hulka yake ya Ubinafsi zaidi, kupenda sifa n.k ambazo zinapingana kuruhusu upinzani.
 
Ukweli usemwe tu. Kiutendaji, uwezo binafsi, ubunifu, uchapakazi, uzalendo ni vitu vinavyomuuza Rais Magufuli tokea awe mwanasiasa -- mbunge, waziri na sasa ni Rais.

WATANZANIA TUNAMPENDA Rais wetu ,Jembe letu ,anatupeleka katika Nchi ya Uchumi wa Kati , watanzania tuchape kazi

#Maliki,Malick
Naunga mkono hoja
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.
P
 
CCM iruhusu watu wachukue form msipoona mafuriko ya Zanzibar
 
Kwanini mataga na lumumba mnakua na wasiwasi hadi mnaamua kutumia uwongo kama huu wa mleta mada.
 
Yaani Kuna vijana wa ccm ni mapimbi hadi bc... acheni kudanganya bhana...hv mbona mnawakosea heshima watangulizi wake??? Kabla ya magufuri kuwa rais hatujawahi kuwa na ndege wala viwanda?? Reli ya Tazara imejengwa enzi ya magufuri ?? Mbona mnatafuta kutukanwa pasipo na sababu za msingi??... daah
 
Wapinzani wanokosa adabu wanapotaka kujilinganisha na Rais Magufuli

Huyu Magufuli ana uwezo mkubwa sana
Wapinzani wana vyombo vya dola? Iweje ulinganishe mtu mwenye vyombo vya dola mahakama na mtu asiye na kitu na mmemfunga mikono nyuma plasta mdomoni, acha kuja na mifano yako ya kishamba toka kolomije
 
Watu, mnamjulia sana JPM! Ukitaka ulaji unaingia JF na verified user name, kujikita kumsifu JPM. Nayeye kwa misifa anaamua kutengua na kumteua Maliki Malick.
Mleta mada anasaka Uteuzi kaamua kujitoa ufahamu akiamini kuwa uteuzi haupo mbali
 
Back
Top Bottom