Rais Magufuli: Chuo chochote kitakachojaribu kugoma sitasita kuwafukuza, tena kwa muda usiojulikana!

Kuwa na adabu rais hakosolewi
Mungu tu ndio hakosolewi kwakuwa hakosei na hajawahi kukosea na hatokosea lakini kwa binadamu yoyote anakosea na atakosolewa maana yeye sio Mungu na hatokaa awe hata malaika labda shetani.
 
sijui kama anafanya review ya haya mambo anahongea? mtu yeyote anayefanya mambo bila tathmini huishia pabaya.
jana alikemea wanafunzi wasifanye siasa vyuoni leo huko Bukoba wanavyuo ( uvccm) wamejitokeza na kuapa kuunga mkono juhudi zifanywazo na serikali yake. kule mawalimu nyerere kuna tawi kabisa la uvccm na yeye alienda pale kulizindua. kumbuka ile story ya kuongea na yule kada wa ccm aliyejidai mwananchi na ile hadithi ya kumpa bajaji mlemavu kote huku alienda kufanya siasa chuo kikuu. unawezaje kuwambia wanafunzi wasifanye siasa vyuoni ? kuna wabunge na mawazir wanasoma. kwa hiyo wakifika chuo waache ubunge na uwazir mpaka wamalize? yeye mwenyewe alosoma PhD kama akiwa wazir mbona hajaacha kwanza siasa mpaka alipomaliza?
AJIFUNZE KUHUTUBIA KULINGANA NA MAZINGIRA SIO KUONGEA KILA LINALOMJIA
 
Hahah let me quote this "Sikiliza mzee "....

Ila Magufuli kauli zake huwa zinakingana sana hata jana kuna baadhi ya mameno ya kiingereza alikuwa anayatamka ndivyo sivyo....

Kwa maraisi wote waliowahi kuiongoza Tanzania huyu magufuli ndio raisi aliekosa kujiamini..... utendaji wake pia ni wa mashaka
FB_IMG_1461816575181.jpg
 
Itakuja kufika kipindi tutakatazwa kulitaja hata jina lake inabidi uwe nakibali kulitaja tu,honesty najisikia ovyo sana nikikuta uzi kumhusu huyu mhutu yaani natamani kukimbilia hata shimoni maana nhhhhh


Nadhani mimi na wewe tuko sawa.......... yaani hakuna jema kwake ni shida sijui tulikosea wapi na tulikosea kwa Mungu kiasi gani........ huyu mtu sio kabisa ana laana haswa
 
Na mapapai kuzaa ndani ya miezi 5!!.
Rais alidanganywa SUA hawazalishi mbegu ya mapapai. Atume watu wake wakadhibitishe hili. kuna kipindi tulifunga safari kutoka katavi kwenda SUA kununua mbegu ya mapapai tkaelekenzwa twende kwenye maduka ya pembejeo. Mbegu nyigi tulizozikuta madukani ni za ASIA
 
Banch???? instead of batch....

Who said this?
-------> Magufuli

Where?
-------> Sua

Ni bora mheshimiwa awe anatumia lugha ya taifa na kuachana na lugha ya malkia maana anazidi kujichafulia CV tu.....
Hawezienda nje wanakoongea kiinglish maana anajua for sure ataaibika kupita maelezo. Anasingizia kujua kingereza sio usomi kujihami. Ati yeye ni wa hapahapa, Kiswahili chenyewe shida. Ndio maana anakimbilia kisukuma alichokulia. Umemsikia akitamka herufi "r"? Hasira zake inaashiria upungufu mkubwa sana wa misamiati ya kuwasiliana na wengine. Mama yake alishauliza "mtamweza kweli kuendana naye akiwa raisi? Ninavyomfahamu huyu mwanangu hawezekani" lisema alipokuwa anahojiwa na vyombo vya habari nyumbani kwake Chato. Kwa kuwa furaha iliwazidi watanzania kumpata chaguo la JK na Mkapa na chama chao kinyume na Lowasa, hata kuelewa maana ya yule mama haikuwa issue. Kila mtu ana udhaifu wake, kupanga ni kuchagua hebu tuendelee mbele na kipindi hiki tulichojitakia wenyewe. Dunia inatushangaa sasa tulivyo na speed ya kuwapiku madikteta duniani. Endeleeni kukiombea KITI alichokikalia hata kama mna kigugumizi kumwombea yeye binafsi. Siku moja Mungu atajibu maombi yenu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Itakuja kufika kipindi tutakatazwa kulitaja hata jina lake inabidi uwe nakibali kulitaja tu,honesty najisikia ovyo sana nikikuta uzi kumhusu huyu mhutu yaani natamani kukimbilia hata shimoni maana nhhhhh
Mimi Afadhali ya uzi humu ndani.
Nikigongananae kwenye Tv siwezi kula kabisa,yaani atakama nilibakisha masaa mawili namaliza siku ananiharibia kabisa siku
 
Wanajamvi nisaidieni kumfikishia mkuu huu ujumbe wangu.

Jana Rais Magufuli akiwa anajibu hoja za wanafunzi wa SUA alitoa onyo kali kwamba wanafunzi wasijaribu kuleta migimo na kwamba chou chochote kitakachojaribu kugoma hatasita kuwafukuza tena kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Rais ni mwendelezo wa kauli zake za vitisho na kutia hofu wananchi. Ni mwendelezo wa kuwafanya watanzania kukosa ujasiri na kujiamini na kujihisi muda wote wako chini ya mamlaka isiyoguswa. Ni ajabu kwa Rais aliyesoma hadi PhD kutumia lugha ya aina hii kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tena katika mazingira ambayo migogoro na migomo haikua sehemu ya tukio. Unajiuliza nini kilimfanya Magufuli atoe kauli hii? Je hili ndio lilikua lengo kuu la yeye kwenda kuongea na wanachuo wa SUA ili apate audience ya kutolea vitisho kwa wanafunzi? Unawatisha ili iweje? Kwa nini uwatishe kugoma au kuleta vurugu badala ya kujadiliana nao namna ya kuondoa matatizo yanayopelekea migomo? Kwa hiyo unataka kutuambia hata wasipofundishwa mwezi mzima, wakikosa madarasa, wakionewa na uongozi wa chuo, wakifelishwa makusudi, watoto wakike wakidaiwa ngono na na waalimu wa kiume, wakiadhibiwa bila taratibu ...basi wanyenyekee tu na wasiwe na uwezo wa kuonesha kutoridhika kwao au kudai haki zao? Hili ndilo taifa la vijana unaotoka kujengea?

Sikiliza mzee… kitu kimoja ambacho Rais Magufuli huna na umeonesha huwezi kuwa nacho, ni uwezo wa kupangilia mawazo na kauli zako ili zifanane na kile anachotaka kuwaaminisha watanzani kwamba ndicho unasimimia. Huwezi ukasema unataka kuwajengea wananchi kuwa majasiri na kutembea vifua mbele kama asemavyo kila wakati na wakati huohuo wananchi hao unawajengea roho za hofu, woga, mashaka na wasiwasi muda wote. Watu hawa wakishakua na woga na wewe kama rais, wakiogopa serikali yako, na wakiogopa vyombo vyako vya usalama, ni wazi huo uoga utakua kila mahali. Wakikutana na wakenya watakua waoga pia maana ndani yao kuna kitu cha ujasiri kinakosekana. Wakikutana na wanyarwanda watajiona wadhaifu. Wakiwa mbele ya waganda watakua mazombi. Mwisho wa siku, badala ya kuwa na watu unaotaka kutembea vifua mbele, unakua na watu wanaopiga magoti mbele ya kila mtu. Pili, hata kama wakitaka kujifanya ni wajasiri, wanakua wajarisi mambumbu maana hawana cha kusamimia. Wanakua na ujasiri wa kulazimisha na kujihami kama wewe Rais ulivyo maana muda wote ni kama hujiamini hivyo unalazimisha kuonekana una nguvu na mamalaka ya kiungu. Ndivyo ulivyo, tulio karibu nawe tunakufahamu hivyo. Unatujengea vijana ambao hawana uwezo wa kutumia akili na uwezo wao wa kufikiri kukabiliana na wanayokutana nayo na badala yake wanataka kutumia nguvu na kulazimisha mambo bil amantinki au mantiki za kuegesha.

Sikiliza mzee.. ukitaka kujua udhaifu wa namna unavyoongoza kwa kujengea hofu, hebu jiulize maswali kwanza. Kwa utawala uliona nao nyumbani kwako, mke wako ana ujasiri kiasi gani? Kama anavyokuogopa wewe ndivyo anavyoogopa au kukos aujasiri mbele ya kila mtu. Watoto wako wana ujasiri kiasi gani? Ni wazi wanavyokuogopa wewe ndivyo wasivyo na ujasiri kwenye jamii. Ndio mana hata hawajaulikani na hawana ujasiri wa kujitambulisha kwenye jamii ambayo baba yao anaiongoza. Ni matunda ya hofu uliowajengea.

Sikiliza mzee.. vyuo vikuu ndipo vijana wanapojifunza mambo mengi Zaidi ya elimu ya darasani na tafiti kama ulivyowaambia. Ndio wanagundua vipaji walivyonavyo.. ndipo wanajifunza uongozi,.. ndipo wanajifunza kujua haki zao na za wengine na jinsi ya kuzidai.. ndipo wanajifunza kukabili watawala na kuwataka kutekeleza mambo ya msingi ya kijamii. Kugoma au kuanzisha vuguvugu vyuoni ni moja ya ishara kwamba vijana hao wanajua haki zao na hawakubaliani na watawala. Habari za kugoma kwa kua wamefeli test ni mambo ya kizamani na huwezi yaona katika karne hii. Unatujengea vijana waoga na wanaomini katika huruma za miungu watu. Watakua hivyo vyuoni, watakua hivyo makazini, watakua hivyo kwa waajiri binafsi, watakua hivyo mbele ya jumuiya ya kimataifa. Hivi ndivyo unavyoijenga Tanzania ya viwanda na kujiamini kama unavyohubiri kila siku.

Sikiliza mzee.. acha uogo, acha kutisha watu, acha kujenga taifa la wasomi waoga na wasiojiamini. Acha vijana waishi ndoto zao na wajifunze kukabiliana na matatizo yanayowakabili. Kama wewe ni tatito, acha wakabiliane nawe na ujipange kutumia busara kukabiliana nao badala ya vitisho.

ngoja nikuulize mzee.. Zaidi ya kutazama panya wanaotegua mabomu (unayapenda) ulitazama madarasa na mambweni hawa wavijana wanaposoma? Ulipata wasaa mzee wangu wa kuulizia serikali yao imewapa fedha kiasi gani za kufanya tafiti tangu uiingie madarakani? ulitazama wanafunzi hawa wanafundishwa na matutorial wangapi na uhaba wa wahadhiri wenye kiwango kinachotakiwa? yani wewe uliona vitisho ndio mambo ya maana kuliko yote kujadili na jumuiya wa wanachuo?

Acha vitisho na acha kujichanganya
Ukitoa tatizo la UBINAFSI walilo nalo watanzania wengi, tatizo lingine kubwa kwa nchi yetu hasa kwa vijana wa leo ni tatizo la MALEZI kwa kijana aliyelelewa kwenye mazingira ya nidhamu na adabu acha kuandika..hata tu kuwaza kuandika ujinga kama huu hawezi, kwa hali ilivyo kwenye jamii yetu..vijana kutokuwa na nidhamu, adabu na maadili mema, nadhani awamu zijazo serikali ifikirie kuwa na wizara maalum inayoshughulikia mambo ya familia, kuwepo na miongozo, kanuni na sheria za jinsi ya kulea watoto wa taifa hili..tukiendelea kama ilivyo sasa taifa hili litaja kuwa taifa la wahalifu..dunia ya leo inahitaji kuwa na nidhamu na adabu kiwango cha juu sana ili ufanikiwe, iwe familia, jamii hata taifa kwa ujumla, leo China imefika hapo ilipo si kwa lelemama..Japan ni nchi ya mfano duniani kwa maendeleo iliyo nayo si kwa bahati..huyu anasema anatishwa , lakini hasemi maneno ambayo Rais aliwausia vijana wale kama watoto wake..amekariri kutishwa, lakini Rais ni Kiongozi,Mzazi, Mshauri na Mlezi..yote anayoyasema yanatokana na moja ya hadhi nilizotaja, wakati mwingine anasema kama Kiongozi tena Amiri Jeshi Mkuu..lakini wakati mwingine anasema kama Mzazi..mtu yeyote unapoamua kumuusia mtoto haijalishi lazima awe amekosea, nadhani tahadhari ni bora zaidi kuliko kurekebisha..
 
Naomba mnisaidie kumuuliza mheshimiwa Rais, hivi ni sababu gani iliyomfanya ahamishwe kutoka Seminary hadi kuhamia Lake Secondary?

Vv
 
Back
Top Bottom