Rais Magufuli: Chuo chochote kitakachojaribu kugoma sitasita kuwafukuza, tena kwa muda usiojulikana!

Ukitoa tatizo la UBINAFSI walilo nalo watanzania wengi, tatizo lingine kubwa kwa nchi yetu hasa kwa vijana wa leo ni tatizo la MALEZI kwa kijana aliyelelewa kwenye mazingira ya nidhamu na adabu acha kuandika..hata tu kuwaza kuandika ujinga kama huu hawezi, kwa hali ilivyo kwenye jamii yetu..vijana kutokuwa na nidhamu, adabu na maadili mema, nadhani awamu zijazo serikali ifikirie kuwa na wizara maalum inayoshughulikia mambo ya familia, kuwepo na miongozo, kanuni na sheria za jinsi ya kulea watoto wa taifa hili..tukiendelea kama ilivyo sasa taifa hili litaja kuwa taifa la wahalifu..dunia ya leo inahitaji kuwa na nidhamu na adabu kiwango cha juu sana ili ufanikiwe, iwe familia, jamii hata taifa kwa ujumla, leo China imefika hapo ilipo si kwa lelemama..Japan ni nchi ya mfano duniani kwa maendeleo iliyo nayo si kwa bahati..huyu anasema anatishwa , lakini hasemi maneno ambayo Rais aliwausia vijana wale kama watoto wake..amekariri kutishwa, lakini Rais ni Kiongozi,Mzazi, Mshauri na Mlezi..yote anayoyasema yanatokana na moja ya hadhi nilizotaja, wakati mwingine anasema kama Kiongozi tena Amiri Jeshi Mkuu..lakini wakati mwingine anasema kama Mzazi..mtu yeyote unapoamua kumuusia mtoto haijalishi lazima awe amekosea, nadhani tahadhari ni bora zaidi kuliko kurekebisha..
Pusi mweusi
 
Sikiliza mzee… Inaonekana nawe pia ni zao la hofu na woga.. na ndio mana unachoona ni hofu ya kumkosea Rais. Jaribu kuchambua ni wapi kwenye ujumbe huu mwandishi amekosa nidhamu na utupe uelewa wako nidhanimu ni kitu gani hasa na inatafsiriwaje kati ya kiongozi na anayeongoza. Mifano unayotoa wewe ya China haina tofauti na anayotoa rais .. mifano ya nchi zinazoendeshwa kimla na ambazo wananchi wao hawana uhuru wa mawazo yao na Amani ya moyo. Wanaofugwa kama kuku wasio na akili. Umshahoji wachina wangapi wakakueleza wanavyojisikia? Hata hivyo China haijajengwa kwa hofu na vitisho.. imejengwa kwa akili, nidhamu ya kazi, mifumo imara ya ndani, na mikakati mipana na shirikishi kwa taifa. Jiulize hiki ndicho anafanya unayetaka asiguswe kwa anayoongea. Yani wewe ukiwa amiri jeshi mkuu hadi ukiingia nyumbani kwako unajitambulisha hivyo? Huoni hiyo ni athari ya kukosa ujasiri na woga
 
Raisi chizi,..kwake uoga ndio ujasiri,kumsifu ndio uzalendo,..

watanzania tujipange kumuondoa huyu chizi kabla hajainakamisha nchi yetu,sisi ndio tuliomchagua anapaswa atuheshimu,kama hawezi kuwaheshimu watanzania basi tumuondoeni hapo alipo,halafu tumshitaki kwa kutonyanyasa na kutuulia viongozi wetu
 
Mkuu usimvunjie heshima yule mama, nyie hebu endeleeni na mijadala yenu bila kumuhusisha mama wa watu tafadhali, wewe utafurahi kusemewa hovyo mama yako? Heshima ichukue mkondo wake

Uko sahihi mkuu naiman64 ulichiomwambia Jembekillo ,sio sawa kumtukana mama wa watu. sijaandika kumtukana rais wala mke wake. andika mambo yanayotuhusu wananchi na tunza heshima za utu wao
 
Kuwa na adabu rais hakosolewi
"Everybody except God is subject to audit" a clause in auditing
Wanajamvi nisaidieni kumfikishia mkuu huu ujumbe wangu.

Jana Rais Magufuli akiwa anajibu hoja za wanafunzi wa SUA alitoa onyo kali kwamba wanafunzi wasijaribu kuleta migimo na kwamba chou chochote kitakachojaribu kugoma hatasita kuwafukuza tena kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Rais ni mwendelezo wa kauli zake za vitisho na kutia hofu wananchi. Ni mwendelezo wa kuwafanya watanzania kukosa ujasiri na kujiamini na kujihisi muda wote wako chini ya mamlaka isiyoguswa. Ni ajabu kwa Rais aliyesoma hadi PhD kutumia lugha ya aina hii kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tena katika mazingira ambayo migogoro na migomo haikua sehemu ya tukio. Unajiuliza nini kilimfanya Magufuli atoe kauli hii? Je hili ndio lilikua lengo kuu la yeye kwenda kuongea na wanachuo wa SUA ili apate audience ya kutolea vitisho kwa wanafunzi? Unawatisha ili iweje? Kwa nini uwatishe kugoma au kuleta vurugu badala ya kujadiliana nao namna ya kuondoa matatizo yanayopelekea migomo? Kwa hiyo unataka kutuambia hata wasipofundishwa mwezi mzima, wakikosa madarasa, wakionewa na uongozi wa chuo, wakifelishwa makusudi, watoto wakike wakidaiwa ngono na na waalimu wa kiume, wakiadhibiwa bila taratibu ...basi wanyenyekee tu na wasiwe na uwezo wa kuonesha kutoridhika kwao au kudai haki zao? Hili ndilo taifa la vijana unaotoka kujengea?

Sikiliza mzee… kitu kimoja ambacho Rais Magufuli huna na umeonesha huwezi kuwa nacho, ni uwezo wa kupangilia mawazo na kauli zako ili zifanane na kile anachotaka kuwaaminisha watanzani kwamba ndicho unasimimia. Huwezi ukasema unataka kuwajengea wananchi kuwa majasiri na kutembea vifua mbele kama asemavyo kila wakati na wakati huohuo wananchi hao unawajengea roho za hofu, woga, mashaka na wasiwasi muda wote. Watu hawa wakishakua na woga na wewe kama rais, wakiogopa serikali yako, na wakiogopa vyombo vyako vya usalama, ni wazi huo uoga utakua kila mahali. Wakikutana na wakenya watakua waoga pia maana ndani yao kuna kitu cha ujasiri kinakosekana. Wakikutana na wanyarwanda watajiona wadhaifu. Wakiwa mbele ya waganda watakua mazombi. Mwisho wa siku, badala ya kuwa na watu unaotaka kutembea vifua mbele, unakua na watu wanaopiga magoti mbele ya kila mtu. Pili, hata kama wakitaka kujifanya ni wajasiri, wanakua wajarisi mambumbu maana hawana cha kusamimia. Wanakua na ujasiri wa kulazimisha na kujihami kama wewe Rais ulivyo maana muda wote ni kama hujiamini hivyo unalazimisha kuonekana una nguvu na mamalaka ya kiungu. Ndivyo ulivyo, tulio karibu nawe tunakufahamu hivyo. Unatujengea vijana ambao hawana uwezo wa kutumia akili na uwezo wao wa kufikiri kukabiliana na wanayokutana nayo na badala yake wanataka kutumia nguvu na kulazimisha mambo bil amantinki au mantiki za kuegesha.

Sikiliza mzee.. ukitaka kujua udhaifu wa namna unavyoongoza kwa kujengea hofu, hebu jiulize maswali kwanza. Kwa utawala uliona nao nyumbani kwako, familia yako ina ujasiri kiasi gani? Wanaokuzunguka wana ujasiri kiasi gani? mawaziri wako wana ujasiri kiasi gani? Kama hawa wote wanavyokuogopa wewe ndivyo wanavyoogopa au kukosa ujasiri mbele ya kila mtu. Jiulize, watoto wako wana ujasiri kiasi gani? Ni wazi wanavyokuogopa wewe ndivyo wasivyo na ujasiri kwenye jamii. Ndio mana hata hawajaulikani na hawana ujasiri wa kujitambulisha kwenye jamii ambayo baba yao anaiongoza. Ni matunda ya hofu uliowajengea na haiwasaidii maishani.

Sikiliza mzee.. vyuo vikuu ndipo vijana wanapojifunza mambo mengi Zaidi ya elimu ya darasani na tafiti kama ulivyowaambia. Ndio wanagundua vipaji walivyonavyo.. ndipo wanajifunza uongozi,.. ndipo wanajifunza kujua haki zao na za wengine na jinsi ya kuzidai.. ndipo wanajifunza kukabili watawala na kuwataka kutekeleza mambo ya msingi ya kijamii. Kugoma au kuanzisha vuguvugu vyuoni ni moja ya ishara kwamba vijana hao wanajua haki zao na hawakubaliani na watawala. Habari za kugoma kwa kua wamefeli test ni mambo ya kizamani na huwezi yaona katika karne hii. Unatujengea vijana waoga na wanaomini katika huruma za miungu watu. Watakua hivyo vyuoni, watakua hivyo makazini, watakua hivyo kwa waajiri binafsi, watakua hivyo mbele ya jumuiya ya kimataifa. Hivi ndivyo unavyoijenga Tanzania ya viwanda na kujiamini kama unavyohubiri kila siku?

Sikiliza mzee.. acha uogo, acha kutisha watu, acha kujenga taifa la wasomi waoga na wasiojiamini. Acha vijana waishi ndoto zao na wajifunze kukabiliana na matatizo yanayowakabili. Kama wewe ni tatizo, acha wakabiliane nawe na ujipange kutumia busara kukabiliana nao badala ya vitisho.

ngoja nikuulize mzee.. zaidi ya kutazama panya wanaotegua mabomu (unayapenda) ulitazama madarasa na mambweni hawa vijana wanaposoma? Ulipata wasaa mzee wangu wa kuulizia serikali yao imewapa fedha kiasi gani za kufanya tafiti tangu uiingie madarakani? ulitazama wanafunzi hawa wanafundishwa na matutorial wangapi na uhaba wa wahadhiri wenye kiwango kinachotakiwa? yani wewe uliona vitisho ndio mambo ya maana kuliko yote kujadili na jumuiya wa wanachuo?

Acha vitisho na acha kujichanganya
 
Uko sahihi mkuu naiman64 ulichiomwambia Jembekillo ,sio sawa kumtukana mama wa watu. sijaandika kumtukana rais wala mke wake. andika mambo yanayotuhusu wananchi na tunza heshima za utu wao
Mama nae anahusika kwanini hammuongozi mume wake!!au na yeye anayapenda mume wake hayo anavyowafanyia watanzania!!?

Magufuli wakati wa kampeni za kugombania Uraisi alikuwa anawabembeleza watanzania wamchague mpaka kufika kulia kwenye majukwa,hivi sasa anawaona watanzania waliomchua hawana mpango wowote
 
Sikiliza mzee… Inaonekana nawe pia ni zao la hofu na woga.. na ndio mana unachoona ni hofu ya kumkosea Rais. Jaribu kuchambua ni wapi kwenye ujumbe huu mwandishi amekosa nidhamu na utupe uelewa wako nidhanimu ni kitu gani hasa na inatafsiriwaje kati ya kiongozi na anayeongoza. Mifano unayotoa wewe ya China haina tofauti na anayotoa rais .. mifano ya nchi zinazoendeshwa kimla na ambazo wananchi wao hawana uhuru wa mawazo yao na Amani ya moyo. Wanaofugwa kama kuku wasio na akili. Umshahoji wachina wangapi wakakueleza wanavyojisikia? Hata hivyo China haijajengwa kwa hofu na vitisho.. imejengwa kwa akili, nidhamu ya kazi, mifumo imara ya ndani, na mikakati mipana na shirikishi kwa taifa. Jiulize hiki ndicho anafanya unayetaka asiguswe kwa anayoongea. Yani wewe ukiwa amiri jeshi mkuu hadi ukiingia nyumbani kwako unajitambulisha hivyo? Huoni hiyo ni athari ya kukosa ujasiri na woga
Licha ya tafsiri pana ya nidhamu, kwa mwanachuo nidhamu ni kutumia muda wote kufanya kile unachopaswa kufanya na si kinyume, Rais aliwaambia wanafunzi wasome kilichowapeleka chuo ni kusoma siyo siasa au kuiga mambo yasiyo na faida kwao na kwa wazazi wao, chuo ni mahali pa kufunzwa kufikiri na kuamua kilicho bora kwa maisha yako na wengine..chuoni kuna uongozi na sheria zipo, ni wajibu wa mwanachuo kutii sheria za chuo na kile uongozi wa chuo unaelekeza, hakuna chuo kinafundisha wanafunz kugoma..zipo njia nyingi za kutatua changamoto si migomo..kwa mtu aliyelelewa holela holela hata anapoambiwa avae kuchomekea shati anapokwenda shule atasema ni imla..si kosa lake, ni kosa la malezi ndio maana nimeeleza..tatizo si wewe unayesema vitisho nk tatizo ni huko ulikoanzia ulivyozaliwa.
 
Raisi chizi,..kwake uoga ndio ujasiri,kumsifu ndio uzalendo,..

watanzania tujipange kumuondoa huyu chizi kabla hajainakamisha nchi yetu,sisi ndio tuliomchagua anapaswa atuheshimu,kama hawezi kuwaheshimu watanzania basi tumuondoeni hapo alipo,halafu tumshitaki kwa kutonyanyasa na kutuulia viongozi wetu
Kwa maneno km haya sidhani utaishi ukakwepa kifungo wewe..asiyefunzwa na ***** dunia itamfunza..endelea
 
soma "sign" yangu "doubt leads to death", hunitishe, sijalelewa kwa vitisho na wazazi wangu,kifungo ndio nini,jela zimejengewa binadamu,wamekoselewa Mitume itakuwa Magufuli!??nenda zako kalale mbele..hujui unachokiongea
Hata shetani hukumbuka while it is too late..endelea, tofautisha kutishwa na kuambiwa ukweli.
 
Hata shetani hukumbuka while it is too late..endelea, tofautisha kutishwa na kuambiwa ukweli.
Binadamu tuko tafauti,hatuwezi kuwa sawa wewe una mawazo yako mimi nina yangu,kwa upande wangu naona huyu raisi hatufai kutuongoza,anafanya watanzania wawe na nidhamu ya woga,taifa lenye raia wenye nidhamu ya woga haliwezi kupiga hatua kimaendeleo,..

Shetani ndio ana sifa za kuwatisha wengine ili yake yamuendee,wewe ndie shetani kwa hili.,,Katishe wengine...niko hapa kusema ninachokiamini
 
Watu hawaongozwi Kwa vitisho na mabavu Karne hizi.Watu Wana Uhuru wa kuwa na fikra huru na mawazo.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu Sana
 
Back
Top Bottom