Rais Magufuli: Chuo chochote kitakachojaribu kugoma sitasita kuwafukuza, tena kwa muda usiojulikana!

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
Wanajamvi nisaidieni kumfikishia mkuu huu ujumbe wangu.

Jana Rais Magufuli akiwa anajibu hoja za wanafunzi wa SUA alitoa onyo kali kwamba wanafunzi wasijaribu kuleta migimo na kwamba chuo chochote kitakachojaribu kugoma hatasita kuwafukuza tena kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Rais ni mwendelezo wa kauli zake za vitisho na kutia hofu wananchi. Ni mwendelezo wa kuwafanya watanzania kukosa ujasiri na kujiamini na kujihisi muda wote wako chini ya mamlaka isiyoguswa.

Ni ajabu kwa Rais aliyesoma hadi PhD kutumia lugha ya aina hii kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tena katika mazingira ambayo migogoro na migomo haikua sehemu ya tukio.

Unajiuliza nini kilimfanya Magufuli atoe kauli hii? Je hili ndio lilikua lengo kuu la yeye kwenda kuongea na wanachuo wa SUA ili apate audience ya kutolea vitisho kwa wanafunzi? Unawatisha ili iweje? Kwanini uwatishe kugoma au kuleta vurugu badala ya kujadiliana nao namna ya kuondoa matatizo yanayopelekea migomo?

Kwa hiyo unataka kutuambia hata wasipofundishwa mwezi mzima, wakikosa madarasa, wakionewa na uongozi wa chuo, wakifelishwa makusudi, watoto wakike wakidaiwa ngono na na waalimu wa kiume, wakiadhibiwa bila taratibu ...basi wanyenyekee tu na wasiwe na uwezo wa kuonesha kutoridhika kwao au kudai haki zao? Hili ndilo taifa la vijana unaotoka kujengea?

Sikiliza mzee… Kitu kimoja ambacho Rais Magufuli huna na umeonesha huwezi kuwa nacho, ni uwezo wa kupangilia mawazo na kauli zako ili zifanane na kile anachotaka kuwaaminisha watanzani kwamba ndicho unasimimia. Huwezi ukasema unataka kuwajengea wananchi kuwa majasiri na kutembea vifua mbele kama asemavyo kila wakati na wakati huohuo wananchi hao unawajengea roho za hofu, woga, mashaka na wasiwasi muda wote. Watu hawa wakishakuwa na woga na wewe kama Rais, wakiogopa serikali yako, na wakiogopa vyombo vyako vya usalama, ni wazi huo uoga utakuwa kila mahali. Wakikutana na wakenya watakuwa waoga pia maana ndani yao kuna kitu cha ujasiri kinakosekana. Wakikutana na wanyarwanda watajiona wadhaifu. Wakiwa mbele ya waganda watakuwa mazombi.

Mwisho wa siku, badala ya kuwa na watu unaotaka kutembea vifua mbele, unakua na watu wanaopiga magoti mbele ya kila mtu. Pili, hata kama wakitaka kujifanya ni wajasiri, wanakua wajarisi mambumbu maana hawana cha kusamimia. Wanakuwa na ujasiri wa kulazimisha na kujihami kama wewe Rais ulivyo maana muda wote ni kama hujiamini hivyo unalazimisha kuonekana una nguvu na mamalaka ya kiungu. Ndivyo ulivyo, tulio karibu nawe tunakufahamu hivyo. Unatujengea vijana ambao hawana uwezo wa kutumia akili na uwezo wao wa kufikiri kukabiliana na wanayokutana nayo na badala yake wanataka kutumia nguvu na kulazimisha mambo bil amantinki au mantiki za kuegesha.

Sikiliza mzee: Ukitaka kujua udhaifu wa namna unavyoongoza kwa kujengea hofu, hebu jiulize maswali kwanza. Kwa utawala uliona nao nyumbani kwako, familia yako ina ujasiri kiasi gani? Wanaokuzunguka wana ujasiri kiasi gani? Mawaziri wako wana ujasiri kiasi gani? Kama hawa wote wanavyokuogopa wewe ndivyo wanavyoogopa au kukosa ujasiri mbele ya kila mtu. Jiulize, watoto wako wana ujasiri kiasi gani? Ni wazi wanavyokuogopa wewe ndivyo wasivyo na ujasiri kwenye jamii. Ndio mana hata hawajulikani na hawana ujasiri wa kujitambulisha kwenye jamii ambayo baba yao anaiongoza. Ni matunda ya hofu uliyowajengea na haiwasaidii maishani.

Sikiliza mzee: Vyuo vikuu ndipo vijana wanapojifunza mambo mengi zaidi ya elimu ya darasani na tafiti kama ulivyowaambia. Ndio wanagundua vipaji walivyonavyo.. ndipo wanajifunza uongozi,.. ndipo wanajifunza kujua haki zao na za wengine na jinsi ya kuzidai.. ndipo wanajifunza kukabili watawala na kuwataka kutekeleza mambo ya msingi ya kijamii. Kugoma au kuanzisha vuguvugu vyuoni ni moja ya ishara kwamba vijana hao wanajua haki zao na hawakubaliani na watawala. Habari za kugoma kwa kuwa wamefeli test ni mambo ya kizamani na huwezi yaona katika karne hii. Unatujengea vijana waoga na wanaomini katika huruma za miungu watu. Watakuwa hivyo vyuoni, watakuwa hivyo makazini, watakuwa hivyo kwa waajiri binafsi, watakuwa hivyo mbele ya jumuiya ya kimataifa. Hivi ndivyo unavyoijenga Tanzania ya viwanda na kujiamini kama unavyohubiri kila siku?

Sikiliza mzee: Acha uongo, acha kutisha watu, acha kujenga taifa la wasomi waoga na wasiojiamini. Acha vijana waishi ndoto zao na wajifunze kukabiliana na matatizo yanayowakabili. Kama wewe ni tatizo, acha wakabiliane nawe na ujipange kutumia busara kukabiliana nao badala ya vitisho.

ngoja nikuulize mzee: Zaidi ya kutazama panya wanaotegua mabomu (unayapenda) ulitazama madarasa na mambweni hawa vijana wanaposoma? Ulipata wasaa mzee wangu wa kuulizia serikali yao imewapa fedha kiasi gani za kufanya tafiti tangu uiingie madarakani? Ulitazama wanafunzi hawa wanafundishwa na matutorial wangapi na uhaba wa wahadhiri wenye kiwango kinachotakiwa? Yaani wewe uliona vitisho ndio mambo ya maana kuliko yote kujadili na jumuiya wa wanachuo?

Acha vitisho na acha kujichanganya!
 
Hahah let me quote this "Sikiliza mzee "....

Ila Magufuli kauli zake huwa zinakingana sana hata jana kuna baadhi ya mameno ya kiingereza alikuwa anayatamka ndivyo sivyo....

Kwa maraisi wote waliowahi kuiongoza Tanzania huyu magufuli ndio raisi aliekosa kujiamini..... utendaji wake pia ni wa mashaka
 
Bila kunji SUA isingekuwa nzuri kama ilivyosasa nawakumbusheni tu kuwa isingekuwa freedom square mambo SUA yangekuwa hovyo sana.
 
Wanajamvi nisaidieni kumfikishia mkuu huu ujumbe wangu.

Jana Rais Magufuli akiwa anajibu hoja za wanafunzi wa SUA alitoa onyo kali kwamba wanafunzi wasijaribu kuleta migimo na kwamba chou chochote kitakachojaribu kugoma hatasita kuwafukuza tena kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Rais ni mwendelezo wa kauli zake za vitisho na kutia hofu wananchi. Ni mwendelezo wa kuwafanya watanzania kukosa ujasiri na kujiamini na kujihisi muda wote wako chini ya mamlaka isiyoguswa. Ni ajabu kwa Rais aliyesoma hadi PhD kutumia lugha ya aina hii kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tena katika mazingira ambayo migogoro na migomo haikua sehemu ya tukio. Unajiuliza nini kilimfanya Magufuli atoe kauli hii? Je hili ndio lilikua lengo kuu la yeye kwenda kuongea na wanachuo wa SUA ili apate audience ya kutolea vitisho kwa wanafunzi? Unawatisha ili iweje? Kwa nini uwatishe kugoma au kuleta vurugu badala ya kujadiliana nao namna ya kuondoa matatizo yanayopelekea migomo? Kwa hiyo unataka kutuambia hata wasipofundishwa mwezi mzima, wakikosa madarasa, wakionewa na uongozi wa chuo, wakifelishwa makusudi, watoto wakike wakidaiwa ngono na na waalimu wa kiume, wakiadhibiwa bila taratibu ...basi wanyenyekee tu na wasiwe na uwezo wa kuonesha kutoridhika kwao au kudai haki zao? Hili ndilo taifa la vijana unaotoka kujengea?

Sikiliza mzee… kitu kimoja ambacho Rais Magufuli huna na umeonesha huwezi kuwa nacho, ni uwezo wa kupangilia mawazo na kauli zako ili zifanane na kile anachotaka kuwaaminisha watanzani kwamba ndicho unasimimia. Huwezi ukasema unataka kuwajengea wananchi kuwa majasiri na kutembea vifua mbele kama asemavyo kila wakati na wakati huohuo wananchi hao unawajengea roho za hofu, woga, mashaka na wasiwasi muda wote. Watu hawa wakishakua na woga na wewe kama rais, wakiogopa serikali yako, na wakiogopa vyombo vyako vya usalama, ni wazi huo uoga utakua kila mahali. Wakikutana na wakenya watakua waoga pia maana ndani yao kuna kitu cha ujasiri kinakosekana. Wakikutana na wanyarwanda watajiona wadhaifu. Wakiwa mbele ya waganda watakua mazombi. Mwisho wa siku, badala ya kuwa na watu unaotaka kutembea vifua mbele, unakua na watu wanaopiga magoti mbele ya kila mtu. Pili, hata kama wakitaka kujifanya ni wajasiri, wanakua wajarisi mambumbu maana hawana cha kusamimia. Wanakua na ujasiri wa kulazimisha na kujihami kama wewe Rais ulivyo maana muda wote ni kama hujiamini hivyo unalazimisha kuonekana una nguvu na mamalaka ya kiungu. Ndivyo ulivyo, tulio karibu nawe tunakufahamu hivyo. Unatujengea vijana ambao hawana uwezo wa kutumia akili na uwezo wao wa kufikiri kukabiliana na wanayokutana nayo na badala yake wanataka kutumia nguvu na kulazimisha mambo bil amantinki au mantiki za kuegesha.

Sikiliza mzee.. ukitaka kujua udhaifu wa namna unavyoongoza kwa kujengea hofu, hebu jiulize maswali kwanza. Kwa utawala uliona nao nyumbani kwako, mke wako ana ujasiri kiasi gani? Kama anavyokuogopa wewe ndivyo anavyoogopa au kukos aujasiri mbele ya kila mtu. Watoto wako wana ujasiri kiasi gani? Ni wazi wanavyokuogopa wewe ndivyo wasivyo na ujasiri kwenye jamii. Ndio mana hata hawajaulikani na hawana ujasiri wa kujitambulisha kwenye jamii ambayo baba yao anaiongoza. Ni matunda ya hofu uliowajengea.

Sikiliza mzee.. vyuo vikuu ndipo vijana wanapojifunza mambo mengi Zaidi ya elimu ya darasani na tafiti kama ulivyowaambia. Ndio wanagundua vipaji walivyonavyo.. ndipo wanajifunza uongozi,.. ndipo wanajifunza kujua haki zao na za wengine na jinsi ya kuzidai.. ndipo wanajifunza kukabili watawala na kuwataka kutekeleza mambo ya msingi ya kijamii. Kugoma au kuanzisha vuguvugu vyuoni ni moja ya ishara kwamba vijana hao wanajua haki zao na hawakubaliani na watawala. Habari za kugoma kwa kua wamefeli test ni mambo ya kizamani na huwezi yaona katika karne hii. Unatujengea vijana waoga na wanaomini katika huruma za miungu watu. Watakua hivyo vyuoni, watakua hivyo makazini, watakua hivyo kwa waajiri binafsi, watakua hivyo mbele ya jumuiya ya kimataifa. Hivi ndivyo unavyoijenga Tanzania ya viwanda na kujiamini kama unavyohubiri kila siku.

Sikiliza mzee.. acha uogo, acha kutisha watu, acha kujenga taifa la wasomi waoga na wasiojiamini. Acha vijana waishi ndoto zao na wajifunze kukabiliana na matatizo yanayowakabili. Kama wewe ni tatito, acha wakabiliane nawe na ujipange kutumia busara kukabiliana nao badala ya vitisho.

ngoja nikuulize mzee.. Zaidi ya kutazama panya wanaotegua mabomu (unayapenda) ulitazama madarasa na mambweni hawa wavijana wanaposoma? Ulipata wasaa mzee wangu wa kuulizia serikali yao imewapa fedha kiasi gani za kufanya tafiti tangu uiingie madarakani? ulitazama wanafunzi hawa wanafundishwa na matutorial wangapi na uhaba wa wahadhiri wenye kiwango kinachotakiwa? yani wewe uliona vitisho ndio mambo ya maana kuliko yote kujadili na jumuiya wa wanachuo?

Acha vitisho na acha kujichanganya
Huyu ni unconventional prezidaa ndio maana kila mala antaka kuonbewa
 
Kawaida mtu akishindwa anabaki kutoa vitisho au kutafuta visingizio. Ati walimu wanafundisha panya kwa hiyo elimu iko juu. Haha mtu na PhD anaongea, tena ya Chemistry ambayo ni natural science. Na masters nje kabisa, hahaha! Kuna watu wanasoma na wengine wanaenda shule kucheza. Hizi ndo zile za kupewa bure.
 
siku waoga wakiamua kukubali kuuliwa makusudi ikifika, mtamuonea huruma MUNGU mtu kwa jinsi atakavyofanywa!
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom