Leo Tarehe 02/09/2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli anakutana na Watendaji wa Kata wa nchi nzima.
Fuatilia Mkutano huo moja kwa moja kupitia TBC1 na katika Mtandao wa youtube kupitia Channel ya Ikulu Live.
===Updates
wimbo wa Taifa ndo unapigwa sasa tayari kuanza kwa Kikao
Watendaji wa Kata wanatambulishwa kimkoa, wameanza na Mkoa wa Arusha
Sasa anayeongea ni Katibu Mkuu Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ambaye baadaye atamkaribisha Dkt. Magufuli. Dkt. Ndumbaro anafafanua kazi za Mtendaji wa Kata kuwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na Kuisemea Serikali katika shughuli zote za Maendeleo na Huduma za Jamii zilizotekelezwa ambazo ni pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, Treni Upatikanaji wa maji, Elimu bure n.k
===Updates
Saa 4:07 asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli anaanza kuongea.
Ameanza kwa kutambua uwepo wa Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri OfisI Ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Katibu Mkuu Utumishi, Laurean Ndumbaro
Rais amewahakikishia Watendaji kutembea vifua mbele kwa vile anajua ni wawakilishi wake katika ngazi ya Kata. Rais pia ameongelea changamoto ambazo watendaji wanakkumbana nazo katika kutekeleza Majukumu yao ikiwemo kutoshirikishwa katika vikao, kuhamishwa kutoka vituo vyao bila utaratibu n,k
Rais amewataka Watendaji hao kusimamia amani katika Kata zao. Aidha amewataka Watendaji walioko katika kata za Mipakani kuhakikisha wanawatambua Wageni wanaoingia nchini hasa kip[indi hiki ambacho kuna zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Rais pia amewataka Watendaji hao kushughulikia kero za Wananchi kama vile migogoro ya Ardhi, Unyanyasi wa Wananchi n.k, amewataka Watendaji hao kutokaa Maofisini na badala yake waende 'Field'. Rais amewataka Watedaji hao kusimamia miradi ya Maendeleo katika Kata zao kwa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo pesa za Maendeleo zinazopelekwa katika Kata zao.