Leo Tarehe 02/09/2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli anakutana na Watendaji wa Kata wa nchi nzima.
Fuatilia Mkutano huo moja kwa moja kupitia TBC1 na katika Mtandao wa youtube kupitia Channel ya Ikulu Live.
===Updates
wimbo wa Taifa ndo unapigwa sasa tayari kuanza kwa Kikao
Watendaji wa Kata wanatambulishwa kimkoa, wameanza na Mkoa wa Arusha
Sasa anayeongea ni Katibu Mkuu Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ambaye baadaye atamkaribisha Dkt. Magufuli. Dkt. Ndumbaro anafafanua kazi za Mtendaji wa Kata kuwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na Kuisemea Serikali katika shughuli zote za Maendeleo na Huduma za Jamii zilizotekelezwa ambazo ni pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, Treni Upatikanaji wa maji, Elimu bure n.k
===Updates
Saa 4:07 asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli anaanza kuongea.
Ameanza kwa kutambua uwepo wa Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri OfisI Ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Katibu Mkuu Utumishi, Laurean Ndumbaro
Rais amewahakikishia Watendaji kutembea vifua mbele kwa vile anajua ni wawakilishi wake katika ngazi ya Kata.
Rais pia ameongelea changamoto ambazo watendaji wanakkumbana nazo katika kutekeleza Majukumu yao ikiwemo kutoshirikishwa katika vikao, kuhamishwa kutoka vituo vyao bila utaratibu n,k
Rais amewataka Watendaji hao kusimamia amani katika Kata zao. Aidha amewataka Watendaji walioko katika kata za Mipakani kuhakikisha wanawatambua Wageni wanaoingia nchini hasa kip[indi hiki ambacho kuna zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Rais pia amewataka Watendaji hao kushughulikia kero za Wananchi kama vile migogoro ya Ardhi, Unyanyasi wa Wananchi n.k, amewataka Watendaji hao kutokaa Maofisini na badala yake waende 'Field'.
Rais amewataka Watedaji hao kusimamia miradi ya Maendeleo katika Kata zao kwa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo pesa za Maendeleo zinazopelekwa katika Kata zao.
***ZAIDI SOMA***
RAIS MAGUFULI
Nawahakikishia kuwa cheo cha Afisa Mtendaji Kata siyo kidogo, ninyi ni wawakilishi wangu na nawahakikishieni tembeeni vifua mbele na kamwe asitokee mtu wa kuwanyanyasa huko mliko.
Nimewaita tusalimiane, tujadiliane namna bora ya kutimiza wajibu wenu katika maeneo yenu mnakotoka, sina hakika katika maisha yenu kama mmeshawahi kuitwa na Wakuu wa Wilaya ama Wakurugenzi wa Halmashauri,kujadili kwa pamoja utendaji kazi wenu.
Najua mmekua mkionewa, mmekua mkihamishwa hovyo hovyo kwa utashi wa wakubwa wenu na nasema ni marufuku kwa Afisa Mtendaji Kata kuhamishwa bila kufuata taratibu.
Hiki ni kikao muhimu sana ndiyo maana nataka tuzungumze na kujadiliana juu ya utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kwakua ninyi ndiyo mko karibu na wananchi na hakuna anayezielewa na kuzijua changamoto za Vijiji na Kata nchini zaidi yenu.
Mna majukumu ikiwemo kuhakikisha usalama katika maeneo yenu, Amani ndiyo msingi wa maendeleo lakini nasistiza hususani kwa kata zilizoko mpakani, watambueni wageni wanaoingia mipakani na hakikisheni hawapati vitambulisho vya uraia ambavyo zoezi la kuvitoa kwa wananchi linaendelea.
Kutatua kero za wananchi ni jukumu lenu lingine, jiwekeeni utaratibu wa kukutana na wananchi na siyo kusubiri wananchi wabebe mabango wakati wa ziara ya Rais na kama hamtasikiliza na kutatua kero za wananchi uwepo wenu katika maeneo yenu hautakua na maana.
Kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zenu ni jukumu lenu na kamwe msikubali mradi kutekelezwa chini ya kiwango kwani na wewe utahusika, wewe ni bosi hupaswi kukaa pembeni wakati pesa zinachezewa.
Natoa rai kwa baadhi yenu, taarifa ninazo acheni kua madalali wa kuuza ardhi kwani ndio chanzo cha migogoro ya ardhi nchini, wacheni kujihusisha na vitendo vya rushwa na dhuluma, mnabambikia wananchi kesi, hamna huruma hata kwa wajane na yatima.
Siku zote mtangulizeni Mungu,mnaposhughulika na maisha ya wananchi, mkumbuke maisha mliyoanza nayo.
Nitasikitika sana baada ya kikao hiki Afisa niliyemteua akaenda kumnyanyasa kwa makusudi Afisa Mtendaji Kata nitamuona hatoshi lakini pia nitashangaa Mtendaji Kata kuwaonea wananchi wanyonge pia nitamuona hatoshi lakini tukumbuke kua hakuna mkubwa kuliko mwingine sisi wote ni sawa.
Najua kuna watu hawakufurahishwa ninyi kuitwa na mimi na kuna baadhi yenu mmetendewa isivyofaa.
Maneno ninayoyasema najua hayatawafurahisha wakubwa wenu ila mimi ndiyo mkubwa wenu wote na sababu kubwa ya kuwaita hapa ni kuwapa meno na kujitambua kuwa ni mabosi , tembeeni kifua mbele.
Dkt. Laurean Ndumbalo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.*
Mambo makubwa matatu mnayopaswa kuyatekeleza katika maeneo yenu ni moja kuisoma, kuielewa na kuitafsiri kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi mfano tunaposema Elimu bure,hakikisheni katika maeneo yenu watoto wote wanaopaswa kwenda shule wanakwenda.
Wajibu wenu wa pili ni kutembelea wananchi, kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yenu na kuzitatua lakini kwa zile zilizo nje ya mamlaka yenu zipelekeni ngazi inayofuata.
Jukumu lenu la tatu ni kuisemea Serikali ninyi mnapaswa kuyasemea yale yanayotekelezwa na Serikali kwa mfano mna wajibu wa kuwaambia wananchi katika maeneo yenu juu ya mambo makubwa yanayofanywa na Serikali mfano katika suala zima la miundombinu ikiwemo ya usafiri na usafirishaji, ujenzi wa barabara katika ngazi ya Miji, Wilaya na Mikoa kama ile inayounganisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa, kuna miradi kama ule wa Flyover na madaraja jijini Dar es Salam.
Kuna Ujenzi wa Meli mpya katika ziwa Ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika lakini tayari makandarasi wako kazini kuanza Ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi.
Yasemeeni makubwa yanayofanywa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, mambo mengine mengi. Serikali inatoa bilioni 450 kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya Elimu ya juu na kubwa zaidi sasa wanafunzi wana Uhuru wa kuchagua vyuo wanavyotaka kwenda kwa sifa stahiki tofauti na miaka ya nyuma ambako walikua wanalazimishwa kwenda TCU walikokua wanataka jambo ambalo Rais Magufuli alilikataa.
Mambo ni mengi tutakesha nikisema niyaorodheshe lakini waambieni kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), upatikanaji wa dawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ya afya kutoka shilingi Bilioni 31 mpaka Bilioni 270 ili kunusuru maisha ya Watanzania, vituo vya afya 300 vimejengwa na Hospitali 67 zimejengwa kwa wakati mmoja katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano, waambieni kuhusu kufufuliwa kwa Shirika la Ndege la ATCL, ndege sita tayari zimenunuliwa kwa fedha zetu wenyewe na nyingine mbili zinatarajiwa kuja kabla ya mwisho wa mwaka huu.
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO