Rais Magufuli azindua rada ya kuongozea ndege

Rais Magufuli azindua rada ya kuongozea ndege

Kwa wale wazalendo tulio hewani tbc wacha tukuhabarisheni
Rais doc john magufuli azindua rada mpya ambazo zinatanua wigo wa usafiri wa anga
....sent from tbc wapinzani karibuni
1568621440422.jpeg
1568621460301.jpeg
 
Daaa injinia kakosa ofa ya kupewa mke na Rais ila sio mbaya amepata ofa ya kwenda kuhiji kuna watu wanabahati sana
 
Fuatilia kupitia TBC1 na Ikulu Online Tv. Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Rada hiyo ni kwa ajili ya kuongozea Ndege katika viwanja vya Ndege vya Dar es Salaam, Mwanza, kilimanjaro na Songwe



=> Mh. Rais kutoka bungeni tumekuja na wabunge kutoka mkoa wa Dar es Salaam na kwengineko wa kamati ya ujenzi, miongoni mwa wabunge hao kuna mwana kamati mpya ambaye ni mbunge Mtaturu - Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

=> Mh. Rais miaka kumi iliyopita ilinunuliwa Rada ambayo iliambatana na kashfa katika ununuzi wake kupitia kampuni moja kubwa sana ya mitambo ya uangalizi wa anga - Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

=> Mh. Rais mimi na timu yangu tulienda Uingereza kupambania kurejeshwa kwa fedha zetu paundi milioni 75 na tukafanikiwa, naomba nikupongeze wewe kwani kipindi chako imenunuliwa rada bila rushwa yoyote - Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

=> Mh. Rais kipekee kabisa napenda kukupongeza kwa kukubali kuhudhuria uzinduzi huu - Waziri wa uchukuzi, Isack Kamwelwe

=> Mh. Rais ili kuhakikisha kuwa mifumo ya rada zote zinafanya kazi kwa ufanisi tumeingia mkataba utaowezesha vipuri kupatikana kwa uhakika katika kipindi cha miaka 15 - Waziri wa uchukuzi, Isack Kamwelwe

=> Nyote huwa mnajua mimi huwa sipendi kabisa miradi inayoishia njiani, na ndio maana leo nimefurahi sana - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

=> Naomba nimpongeze kwa dhati mkurugenzi mkuu wa TCAA Johari, sina zawadi ya kumpa ila mwaka huu akitaka kwenda hija nitamlipia gharama - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

=> Kwakweli Johari wewe ni johari kweli kwenye kazi, yaani kwenye ufanisi wa kazi yupo makini sana, ningekuwa na binti ningempa - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

=> Aliyetuuzia rada kule Uingereza alijiuzuru, lakini wa kwetu hapa sijui kama kuna mtu alijiuzuru labda siku zijazo waamue kufanya hivyo - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

=> Shirika letu la ndege linafanya vizuri sana mkiona ndege zetu zinakamatwa msishangae - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

=> Ushahidi wa kwamba shirika letu linafanya vizuri, siku za nyuma tulikuwa tunamiliki asilimia 3 tu lakini hivi sasa tunamiliki asilimia 70 ya safari zote za Anga - Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli

Mh, nchi hii ya ajabu. Nchi nzima wanashangilia kuzindua Ungo, Ungo kweli! Hivi na USA , Denmark, Sweden and the like wakijenga Ungo mpya wanasimamisha nchi kushangilia? Najaribu kuwaza ikitokea break through say katika medicine ya kupewa Nobel prize kada wa CCM itakuwaje 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
 
Kumbe ndege zilikua zinatua apo kwenu bila ya kuwepo rada
 
Watoa mapovu mmemsikia Rais... eeeeeeh kasema amechomekea tu
Hapa kazi tu
 
Yaani sijui ni kwa nini ametaja jina lake kwa kugugumia...
Imeniuma sana aisee, kusema jimbo lake lilitelekezwa...
Yaani marisasi yote yale aisee[emoji22]
 
Rais Magufuli amesema ufisadi wa fedha ya rada ulisababisha waziri wa Uingereza kujiuzulu kwa hiari lakini yule wa Tanzania aliendelea kula bata.

Ashukuru ni zama zile lakini ingekuwa ni awamu ya 5 hii....hii....hii asingepona, amesisitiza Rais Magufuli.

Wadau nikumbusheni huo mkasa wa rada tafadhali

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom