Rais Magufuli awasomesha namba wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kwa mwendokasi

Taarifa hii ina mapungufu makubwa sana. Nijuavyo mimi ni kwamba mabasi ya mwendo kasi yanafika mpaka Mbezi. Hakuna sehemu ambako usafiri hauna shida kama maeneo hayo hasa kama unaelekea Posta na Kariakoo au hata Morocco. Usafiri upo wa kutosha na wa haraka. Imefika wakati sasa wenye daladala za kawaida wanalalamika hawafanyi biashara. Tena wengine wameamua kusitisha route za huko na kwenda kutafuta kwingineko. Haya ndiyo maendeleo. Msianze kulalamika kwa mambo msiyojua
Mkuu kweli usemayo ila magari ni machache sana hasa Morocco mbezi. Unaweza kukakaa pale Morocco terminal zaidi ya dk 40 hakuna gari. Tunaomba sana waongeze magari zaidi asubuhi na jioni
 
Kutokana na wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kuipiga chini CCM katika uchaguzi uliopita, sasa inaonekana Mhe. Rais ametoa maelekezo kwa Sumatra kuondoa magari yote kwenye route ya Mawasiliano - Posta, Kimara - Posta na Mbezi - Posta ili wanachi wa maeneo hayo waisome namba.

Katika utafiti wetu mdogo tulioufanya kwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wanasema Rais Magufuli ndio ametoa maelekezo kuyaondoa mabasi hayo ya abiria kwenye maeneo hayo. Wakazi hao wanasema hata Sumatra wenyewe wanadai wamepewa maelekezo kutoka ofisi kubwa ili kuyaondoa mabasi haya kabla ya muda wake.

Hali ya usafiri katika maeneo haya ni mbaya sana, kwasababu kwanza nauli ni kubwa sana halafu watu wa mbezi wanalipa nauli mara mbili kwenye mabasi ya mwendokasi.

Nauli za mwendo kasi kwa sasa ni Tshs. 650 kituo hadi kituo lakini abiria wanalipa Tshs. 700 kwa kisingizio kwamba wahudumu wa Mwendokasi hawana chenji ya Tshs.50, kwahiyo kiuhalisia nauli ya mwendokasi ni Tshs. 700 kituo hadi kituo na Tshs. 200 kwa wanafunzi.

Lakini kwa wakazi wa Mbezi nauli ni mara mbili ya hii na usumbufu juu.

SUMATRA hata kama mmepewa maelekezo ya Ofisi ya juu kwahiyo mnafurahia wananchi ya maeneo hayo wanavyopata shida sio?

Poa tu Mungu yupo atawatendea wananchi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kulingana na mapenzi yake.
Toa ushahidi,vinginevyo utahudhuria jela mda si mrefu
 
Borq sikai upande wa magari hayo. Yani hayana unafuu wowote wa usafiri. Kugombaniana kule kule kubanana vile vile. Yani kero tupu.
Poleni wakazi wa mbezi na kimara
 
Hata nadhani umetumia vibaya jina la Rais, kila jambo linautaratibu wake mpango kuondoa daladala morogoro road umekuwepo kabla ya utawala wa muheshimiwa Magufuri.

Pia zoezi hili ni kwaajili ya kupisha mabasi ya mwendo kasi lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari mjini.

Kwa kukusaidia walalamikie dart waongeze mabasi ili kuondoa usumbufu kwenu.
 
tatizo la ubungo wabunge wote wanaopewa wakishapata hawana time na wananchi kilichobaki ni kurudi ccm tu nakumbuka hata alipokuwa keenja hakukuwa na shida ya maji lkn yalipoanza mambo ya upinza ikawa shida sasa maji hayaonekani na matatizo mengine ndio kama hayo ya mambo ya usafiri na wabunge madiwani wapo hakuna ana stuka hata kidogo
 
Tangu nimeshtukia huo uTAPELI kitambo sana nimeacha kutumia Card nilikuwa naifanyia uchunguzi kimegundua Pesa inakatwa....kidogo kidogo....hawa jamaa ni matapeli wakiwango cha juu sana
Dawa ni kuniachana na kadi tuu nimegundua!
 
tatizo la ubungo wabunge wote wanaopewa wakishapata hawana time na wananchi kilichobaki ni kurudi ccm tu nakumbuka hata alipokuwa keenja hakukuwa na shida ya maji lkn yalipoanza mambo ya upinza ikawa shida sasa maji hayaonekani na matatizo mengine ndio kama hayo ya mambo ya usafiri na wabunge madiwani wapo hakuna ana stuka hata kidogo
Ndio maana nyie mpo kwaajili ya wanaume tu...Kwahiyo shida ikizi suluhisho ni kuinua MIKONO sio kupambana hadi kieleweke...unasema kipindi cha Keenja kulikuwa na MAJI yapi....
 
Kwaakili kama hizi kwanini ccm wasikupe Tuzo ya Fulana na Kofia....inaonekana huishi Dar....manake hata kam ungeishi MBUTU japo siku 1 ungepanda huo wanaita mwendokasi then usingeandika huu UGOLO
Asante mkuu,ila naona kwa mawazo yako ningewaponda ungenipa na like,ila sijafanya kile unachokiwaza wewe.
 
Ndio maana nyie mpo kwaajili ya wanaume tu...Kwahiyo shida ikizi suluhisho ni kuinua MIKONO sio kupambana hadi kieleweke...unasema kipindi cha Keenja kulikuwa na MAJI yapi....
umongea nini wewe choko hao wananchi watapambana na nani ikiwa wawakilishin wao hawaonekani majimboni mpaka wakati wa campain
 
Wiki sasa naisoma namba duh mtu unapanda gari no kupumua!
Afu wanafanya dhuruma Kwenye malipo hasa kwa watu wenye kadi. Ukichanja ile kadi ukaangalia salio unakuta shilling MIA TATU imepungua ukiiliza wanasema ni tatizo LA max malipo!
Huu ni unyonyaji na wizi mkubwa hautakiwi kuvumiliwa!
Sijui nani yuko juu ya huu wizi ni serikali, UDART au Max Malipo???
Naomba vyombo vinavyohusika vilishughulikie hili jambo hili.

Ndugu, una uhakika na hilo la upungufu katika kadi yako?
 
Huu ulalamishi hauwezi kutufikisha popote, ushabiki ufiotumia fikra wa uchadema na u CCM ni hatari kwa nchi hii kama ulivyo usimba na uyanga kwenye soka letu. unatunyima firsa ya kuyatazama mambo kwa mtazamo chanya. Hivi kila siku mnasifia maendeleo nchi za watu unafikiri yalishuka kama mvua. Jiji la Dar leo lina watu milioni 5, projoection ya 2030 linaweza ku double population, bado mtu anajidai kutetea daladala kwa jina la siasa, hatua za maendeleo lazima zipigwe, Mwendokasi pamoja na changamoto zake umesaidia sana kuwa na uhakika na uharaka wa usafiri kwa wakazi wa mbezi, wanafunzi leo wanasafiri kwa heshima na utu kama watoto wa watu wenye akili, hakuna kusukumwa wala kutukanwa kama ilivyokuwa kwenye daladala, kitu kilichokuwa kinawafanya wajione kama vile kusoma ni adhabu.

Maendeleo yana gharama, tusaidiane kuelekeza nguvu kuibana serikali na wahusika waboreshe huduma, mabasi yaongezwe na miundombinu iimarishwe, hatuwezi kubaki kwenye daladala wakati idadi ya watu jiji hili inakuwa kwa kasi ya ajabu.
Tuache ulalamishi, tuchape kazi, sisi tunaotumia mwendokasi tunashukuru kwa adha tuliyokuwa nayo kuondoka, shida ya kulipa 2000 kwenye NOAH hatunayo tena, hatukai barabarani saa 2 mpaka tatu.
Mkiacha siasa zenu uchwara na figisu za wenye daladala na wapiga debe MWENDOKASI NI MKOBOZI WETU.
 
Wabunge madiwani wa maeneo hayo kwa nn mlichaguliwa?? Mnafanya nn wakati mnaona wananchi wanateseka?

wabunge na madiwan wa wapinzani wanafikisha malalamiko sawa lkn hawasikilizwi ili kuonesha kwa wananchi kuwa utendaji wao ni mbovu na ni waki maslahi binafsi
 
Kutokana na wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kuipiga chini CCM katika uchaguzi uliopita, sasa inaonekana Mhe. Rais ametoa maelekezo kwa Sumatra kuondoa magari yote kwenye route ya Mawasiliano - Posta, Kimara - Posta na Mbezi - Posta ili wanachi wa maeneo hayo waisome namba.

Katika utafiti wetu mdogo tulioufanya kwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wanasema Rais Magufuli ndio ametoa maelekezo kuyaondoa mabasi hayo ya abiria kwenye maeneo hayo. Wakazi hao wanasema hata Sumatra wenyewe wanadai wamepewa maelekezo kutoka ofisi kubwa ili kuyaondoa mabasi haya kabla ya muda wake.

Hali ya usafiri katika maeneo haya ni mbaya sana, kwasababu kwanza nauli ni kubwa sana halafu watu wa mbezi wanalipa nauli mara mbili kwenye mabasi ya mwendokasi.

Nauli za mwendo kasi kwa sasa ni Tshs. 650 kituo hadi kituo lakini abiria wanalipa Tshs. 700 kwa kisingizio kwamba wahudumu wa Mwendokasi hawana chenji ya Tshs.50, kwahiyo kiuhalisia nauli ya mwendokasi ni Tshs. 700 kituo hadi kituo na Tshs. 200 kwa wanafunzi.

Lakini kwa wakazi wa Mbezi nauli ni mara mbili ya hii na usumbufu juu.

SUMATRA hata kama mmepewa maelekezo ya Ofisi ya juu kwahiyo mnafurahia wananchi ya maeneo hayo wanavyopata shida sio?

Poa tu Mungu yupo atawatendea wananchi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kulingana na mapenzi yake.
Yaani wananitia hasira mpaka basi
Kama umepanga huko hama hulazimishwi na mtu kuishi mbezi,na kama umejenga ni afadhali yako kwani zile gharama za kodi unakuwa unahamishia kwenye gharama za usafiri!!!!waswahili mnachosha kweli na malalamiko ya ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom