Rais Magufuli awasomesha namba wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kwa mwendokasi

wwww

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
350
252
Kutokana na wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kuipiga chini CCM katika uchaguzi uliopita, sasa inaonekana Mhe. Rais ametoa maelekezo kwa Sumatra kuondoa magari yote kwenye route ya Mawasiliano - Posta, Kimara - Posta na Mbezi - Posta ili wanachi wa maeneo hayo waisome namba.

Katika utafiti wetu mdogo tulioufanya kwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wanasema Rais Magufuli ndio ametoa maelekezo kuyaondoa mabasi hayo ya abiria kwenye maeneo hayo. Wakazi hao wanasema hata Sumatra wenyewe wanadai wamepewa maelekezo kutoka ofisi kubwa ili kuyaondoa mabasi haya kabla ya muda wake.

Hali ya usafiri katika maeneo haya ni mbaya sana, kwasababu kwanza nauli ni kubwa sana halafu watu wa mbezi wanalipa nauli mara mbili kwenye mabasi ya mwendokasi.

Nauli za mwendo kasi kwa sasa ni Tshs. 650 kituo hadi kituo lakini abiria wanalipa Tshs. 700 kwa kisingizio kwamba wahudumu wa Mwendokasi hawana chenji ya Tshs.50, kwahiyo kiuhalisia nauli ya mwendokasi ni Tshs. 700 kituo hadi kituo na Tshs. 200 kwa wanafunzi.

Lakini kwa wakazi wa Mbezi nauli ni mara mbili ya hii na usumbufu juu.

SUMATRA hata kama mmepewa maelekezo ya Ofisi ya juu kwahiyo mnafurahia wananchi ya maeneo hayo wanavyopata shida sio?

Poa tu Mungu yupo atawatendea wananchi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kulingana na mapenzi yake.
 
Wiki sasa naisoma namba duh mtu unapanda gari no kupumua!
Afu wanafanya dhuruma Kwenye malipo hasa kwa watu wenye kadi. Ukichanja ile kadi ukaangalia salio unakuta shilling MIA TATU imepungua ukiiliza wanasema ni tatizo LA max malipo!
Huu ni unyonyaji na wizi mkubwa hautakiwi kuvumiliwa!
Sijui nani yuko juu ya huu wizi ni serikali, UDART au Max Malipo???
Naomba vyombo vinavyohusika vilishughulikie hili jambo hili.
 
ina maana hujawahi kuuona mpango wa usafiri wa miaka kadhaa iliyopita kuhusu huduma ya mabasi ya mwendo kasi??
Pia waulize madereva na hao wamiliki wa mabasi ni wamefukuzwa au leseni zao zimeisha za kutumia routes hizo?? Waliingia makubaliano wao wakijua kabisa kuwa leseni za hizo rputes zikiisha hawatatumia tena hizo routes na hii ilikuwa wakati mkwere akiwa rais.
 
Yaani jimbo la Ubungo ni majanga matupu, Hata bajaji na bodaboda zimezuiwa kupita barabara ya chuo kikuu, daladala zenyewe chache na zinachelewa kweli kuondoka vituoni. Hali hii inawakwaza kweli wateja wa barabara hiyo.

Sijui Mbunge wa hili jimbo la ubungo anafanya nini
 
Wiki sasa naisoma namba duh mtu unapanda gari no kupumua!
Afu wanafanya dhuruma Kwenye malipo hasa kwa watu wenye kadi. Ukichanja ile kadi ukaangalia salio unakuta shilling MIA TATU imepungua ukiiliza wanasema ni tatizo LA max malipo!
Huu ni unyonyaji na wizi mkubwa hautakiwi kuvumiliwa!
Sijui nani yuko juu ya huu wizi ni serikali, UDART au Max Malipo???
Naomba vyombo vinavyohusika vilishughulikie hili jambo hili.
Kama kilazzer kwenye salio utapigwa tuu, hamna namna! Wenzio hatuibiwi hata 50, na change hatuachi!!
 
waTAnzania mnataka maendeleo gani nyie? Cha muhimu acheni kulalama mtumieni Mbunge wenu , diwani aongee na serikali waongeze mabasi ya mwendo kasi! hilo ndio muhimu! Mradi umejengwa kwa pesa nyingi sana uacheni ufanye kazi na soon mtaona matunda yake! vuteni subira na acheni kumkatisha tamaa RAis.
 
Wabunge madiwani wa maeneo hayo kwa nn mlichaguliwa?? Mnafanya nn wakati mnaona wananchi wanateseka?

Kama wameshindwa kufanya mikutano ya siasa wataweza hili? We mgeni na Bwana Yule?
 
Back
Top Bottom