Rais Magufuli awaombe msamaha matajiri

Rais Magufuli awaombe msamaha matajiri

Hovyo kabisa,sasa ulitaka hela atoe masikini?
Pote duniani hata marekani kina Bill Gates wanachangia maafa
Hiyo ni social responsibility yao
Chadema na ukawa mnatumia maafa kisiasa hii ni mbaya sana
Tatizo ninyi watoto Wa Lumumba bado hamjaijua Dunia vizuri.Masikini tunawapenda ila hatuwategemei kwa lolote.Hata katika ngazi ya familia ukiwa masikini huombwi ushauri wowote.Tatizo kidogo tu masikini hata kuchangia 1000 hawawezi.Kule wanahitaji zaidi ya bill 5 ili waathirika warudi kwenye maisha yao ya kawaida.Matajiri wakikaa kimya itakuwaje? Usitukane mamba wakati bado hujavuka mto! Huko mbeleni mitihani Ni mingi inakuja!
 
Matajiri wa nchi hii walifikia wakati ambapo wakageuka Miungu watu, wakashindwa kukumbuka ukweli kwamba kila mtu anapaswa kuwa mtenda haki kwa nafasi yake kwenye jamii. Rais JPM hajawadharau bali anawakumbusha tu kuhusiana na kujinyenyekeza na kujishusha maishani.
Unakumbuka issue ya yule mke wa waziri ambaye alijibizana hovyo na traffic police?. Hakuna anayepaswa kujiona yupo juu ya sheria, na kujiona anao ushawishi mkubwa kiasi cha sheria na matakwa yake kuwa sio kitu mbele yake.

Sio kweli Matajiri wengi ni wastarabu sana.
Baharessa, Mengi, Dewj, Abood, Moil, Manji, na wengine wengi ni watu wa watu na wanajichanganya sana na watu wa chini.
Hii tabia ya kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuwaponda na kuwasingizia matajiri sio nzuri.

Watu wenye hulka ya kujifanya miungu watu ni wale wanaopata mapesa kupitia vyeo vyao na madaraka serikalini.
Hawa ndio hatari sana. Hawa ndio wanatishia watu maisha.
Na hata sheria nyingi zinazotungwa zinatungwa kuwalinda wao wasiguswe wala kunyoshewa kidole. Hawa ni zaidi ya miungu watu. Ni miungu kabisa wa dunia hii. Wanataka kuitwa waheshimiwa na wanataka kila mtu awaogope na kuwatii kwa sababu ya mamlaka waliyonayo. Hawa hata familia zao ni tatizo sana kwenye jamii. Watoto wao hawaguswi. Zaidi hawana mchango wowote kwenye majanga kama haya. Na hata wakitoa basi wanatoa kwa malengo ya kupata umaarufu.

Tusiwasingizie wafanyabiashara matajiri kuwa ni watu wabaya. Wabaya siku zote ni majizi yaliyoshika madaraka makubwa yenye vipato vikubwa na madili mengi. Hawa ndio wenye dharau mana wanapata pesa nyingi bila kufanya biashara yoyote zaidi ya kuwatumia wafanyabiashara kama vitega uchumi wao.

Labda wewe unitajie mfanyabiashara tajiri anayejifanya mungu mtu.
 
Ki ungwana Magufuli awaombe msamaha, pia akae nao wamueleze changamoto zao
 
Hahahaha habari kama hizi hupeleka kiungulia ufipa na Chadema kwa ujumla.,

Chadema wamejipa ajira ya kuombea mabaya nchi yetu. Shame on you mshindwe na mlegee
 
Kusema kweli toka moyoni nimetiwa moyo sana na wafanyabiashara na matajiri kwa namna walivyojitoa kwa kuchangia zaidi ya 1.3b kwa ajili ya wenzetu wahanga wa tetemeko.Watu hawa waliochangia jasho lao wameonyesha kwamba nchi hii ni yetu sote na tunategemeana kwa hali na mali.Sisi masikini tunasema tunawapenda matajiri ilimuradi tu uwe utajiri wa halali.Binafsi huwa nasikitishwa sana na baadhi ya kauli za Rais wetu zinazoashiria kuwa upande wa masikini "Mimi ni Rais wa Masikini na wanyonge"..."Serikali ninayoiongoza imechaguliwa na masikini".Tumeona matajiri wakitufaa, kutuhifadhi na kutufuta machozi.Magufuli waombe msamaha matajiri kukosea sio dhambi
Rais Magufuli ndiye aliyewasamehe matajiri waliokwepa kodi bandarini.

Kinyume kabisa ngonjera inayoimbwa na ufipa boys hapa
 
Hivi kila tajiri ni mwizi?? na pana haja gani tukafanya HAPA KAZI TU, kama umasikini ndio uraia wema?? si tupumzike tu umaskini umee vema au? nachukia umasikini na nshakula yamini at aje 40's lazima niwe don inshallah panapo uhai.
 
Back
Top Bottom