MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
UHABA wa sukari ulioibuka kwa kasi nchini unatajwa kuwa ni mbinu chafu za baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wenye lengo la kuutikisa na kuujaribu utawala wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli. RAI linaripoti.
Kitendo cha kuadimika kwa sukari kinatajwa kuwa ni jaribio kubwa na zito kwa Rais Magufuli kutokana na bidhaa hiyo kugusa maisha ya kila siku ya watu wengi.
Wanaoiona hatua hii ya uhaba wa sukari kama jaribio kwa Rais Magufuli, wanasema kuwa dhamira kuu ya wanaoficha sukari ni kumgombanisha na wananchi wake na kwamba kama atafanikiwa kulidhibiti jaribio hili, hataweza kujaribiwa tena.
Hoja hii inakuja kutokana na sakata la sukari kuwa mwiba mkali kwa serikali kwa kipindi kirefu sasa, hali iliyosababisha kuwaangusha baadhi ya wanasiasa na watendaji wengine kwenye tawala zilizopita.
Profesa Simon Mbilinyi, Idd Simba na Joseph Mungai ni miongoni mwa wanasiasa waliojikuta wakilazimika kung’oka kwenye viti vyao vya uwaziri ili kuikoa serikali.
Wakati wa utawala wa awamu ya tatu, Profesa. Mbilinyi alilazimika kuachia ngazi mwaka 1997 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya sukari kama ilivyokuwa mwaka 2001 baada ya Simba kulazimishwa kuachia ngazi ili kuisuru serikali.
Simba alikumbana na kadhia hiyo baada ya kuhusishwa kwenye uamuzi wa kutoa vibali kwa kampuni kadhaa vya kuagiza sukari nje ya nchi, lengo likiwa ni kukidhi mahitaji makubwa ya sukari yaliyokuwa yakilikumba taifa wakati huo.
Uamuzi huu wa kutoa vibali kwa wafanyabiashara hao badala ya kuwa wa manufaa, ukaonekana kuwaumiza zaidi walaji, hali iliyomuingiza matatizoni kwa madai kuwa uamuzi wake huo uligubikwa na rushwa.
Simba akawekwa katika mazingira magumu kama yaliyomkumba Profesa Mbilinyi, hata hivyo alijitetea kuwa alitoa vibali hivyo kwa maelekezo ya Baraza la Mawaziri kwa hiyo hakuona kama alikuwa amefanya kosa lolote la kiutendaji hivyo, akakataa kujiuzulu kama alivyokuwa akitakiwa na baadhi ya watu kupitia katika vyombo vya habari.
Agosti 2001, sakata hilo la sukari likaingizwa bungeni, Mbunge wa Kwela (CCM), Chrisant Mzindakaya akaibuka na hoja binafsi dhidi ya Simba. Akatoa taarifa kuhusu kile alichokiona kuwa ni kashfa kwa waziri huyo, serikali na hata Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akaweka shinikizo la kutaka Simba, kwanza ajiuzulu nafasi yake ya uwaziri na pili aliombe radhi Bunge kwa kulidanganya wakati alipokuwa akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake pale alipozungumzia suala zima la sakata hilo.
Simba akalieleza Bunge bayana kwamba hata jiuzulu kwani haoni kama ametenda kosa lolote. Kauli yake hiyo haikuweza kumuokoa na wala haikuweza kukiokoa chama chake. Upinzani mkali ukaendelea toka ndani ya CCM na nje wakimtaka ajiuzulu.
Miezi mitatu baada ya shinikizo kuendelea, hatimaye Simba akaamua kujiuzulu uwaziri, akisema wazi kwamba amelazimika kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kuinusuru serikali yake kusambaratika na chama chake kustawi. Huo ukaonekana kuwa ni ushindi kwa wapinzani wake.
Kadhia hiyo iliyomkumba Simba na Serikali ya awamu ya tatu, inatajwa kuinyemelea serikali ya Magufuli kutokana na uamuzi wake wa awali wa kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje.
Hatua hiyo ya kufunga milango ya uagizaji wa sukari kutoka nje, inatajwa kuwakera baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, hali iliyowasukuma kwa makusudi kutosambaza sukari madukani.
Rais Magufuli, alipiga marufuku uagizaji na uingizaji sukari kutoka nje ya nchi Febrauri 18, mwaka huu na kuwataka watendaji wa Serikali, kutotoa vibali vya kuingiza bidhaa hiyo.
Alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari kuingia nchini, vibali atavitoa mwenywe si mtu mwingine yeyote ili kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.
Rais aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam, wakati akitoa shukrani zake kwa waandishi wa habari, wasanii na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.
Aliongeza kuwa, inasikitisha kuona sukari ikiingizwa nchini kutoka nje wakati nchi ina viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa hiyo na kusababisha Watanzania wengi kupoteza ajira kutokana na sukari wanayozalisha kukosa soko.
“Nakuagiza Waziri Mkuu, kwamba ni marufuku mtendaji yeyote wa Serikali kutoa kibali cha kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi…vibali vyote nitatoa mimi.
“Katika kampeni zangu mwaka 2015, nilisema Serikali yangu itakuwa ya viwanda hivyo lazima tuvithamini viwanda vya ndani na kulinda bidhaa zinazozalishwa,” alisema.
Pamoja na Rais Magufuli kuwa na nia njema ya kuvipa nafasi viwanda vya ndani, takwimu zinaonesha kuwapo kwa upungufu wa sukari wa zaidi ya tani 150,000 kwa mwaka kutokana na viwanda vya ndani kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 302,000 huku mahitaji yakiwa ni tani 450,000 kwa mwaka.
Pamoja na ukweli huo duru za habari zinaweka wazi kuwa nchi haikustahili kuingia kwenye uhaba wa sukari katika kipindi hiki kwani bado wafanyabiashara wengi walikuwa na hifadhi ya kutosha na kwamba yanayoendelea sasa ni hujuma za baadhi ya wafanyabiashara.
Mbali ya kupiga marufuku uingizaji wa sukari, pia Rais Magufuli anaingizwa majaribuni kutokana na mwenendo wake wa kiutendaji unaomuweka kando na matajiri, huku ukimsogeza karibu na Watanzania wa hali ya chini.
Tangu aingie madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Magufuli amekuwa ni mtu wa kutumbua majipu pamoja na kubana mianya mbalimbali ya rushwa na ukwepaji wa kodi, hali inayotajwa kuwaathiri wafanyabiashara wasio waaminifu.
Hatua yake hiyo ya kushughulika na majipu inatazamwa vibaya na baadhi ya matajiri na wafanyabiashara waliokuwa wakinufaika na mfumo dhaifu wa ukusanyaji wa kodi uliokuwa ukiwapa nafasi wafanyabiashara kukwepa kodi.
Kauli na matendo yake yenye kujali masilahi ya wengi yanatazamwa kama kitanzi kwa baadhi ya wafanyabiashara na kwamba hatua pekee waliyoamua kuichukua ni kumuingiza majaribuni kwa kutumia sukari kumtikisa.
Kwa namna moja au nyingine hatua hiyo inaonekana kufanikiwa ingawa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa wameendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kupambana na watu wenye nia ovu na nchi.
Rais Magufuli ameshaahidi kuwashughulikia wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwapokonya mali walizochuma isivyohalali.
“Nataka niwahakikishie ndugu zangu, serikali ninayoiongoza ambayo ninyi wenyewe masikini ndio mlinichagua mimi, nitaisimamia kwa ajili ya masikini na hawa watu wamefaidi mno jasho la Watanzania, haitawezekana na haitawezekana,”alisema.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilifuatiwa na usakaji wa bidhaa hiyo uliyokuwa ukifanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kushirikiana na jeshi la polisi nchi nzima.
Hata hivyo zipo taarifa kuwa uamuzi wa kuwapokonya wafanyabiashara sukari umekuwa mgumu, badala yake wote waliokutwa na kiasi kikubwa cha sukari kwenye maghala yao kuamriwa kuiuza chini ya usimamizi wa serikali.
Pamoja na jitihada hizo za serikali za kupambana na hujuma za baadhi ya wafanyabishara, bado hali ya sukari nchini si shwari katika maeneo mbalimbali, ingawa tayari serikali imeiagiza kutoka nje.
Katika kuhakikisha tatizo hilo linakwisha Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuongeza uzalishaji wa sukari nchini na kwamba nia yao ni kuhakikisha tatizo linakoma ifikapo 2019.
“Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.
“Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.
“Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii ‘gap’ iliyopo,” alisema.
WAFANYABIASHARA WAKIRI
Mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini aliliambia RAI kuwa kinachofanyika sasa kwenye suala la sukari ni uhaini na kwamba dhamira ya wanaofanya hivyo ni kumjaribu Rais Magufuli.
“Huu ni uhaini tu, wafanyabiashara wanaoficha sukari wanachokifanya ni kumjaribu Rais Magufuli, utaratibu huu si mzuri na unakwamisha jitihada njema za Rais.
“Nawaomba wafanyabiashara wenzangu waachane na utamaduni huu badala yake washirikiane na serikali kuwaletea maendeleo Watanzania wote,” alisema mfanyabiashara huyo ambaye aliomba kutoandikwa jina lake gazetini.
Hata hivyo aliweka wazi kuwa pamoja na jitihada za Rais Magufuli za kutaka matajiri waishi kama mashetani bado hatafanikiwa kwa sababu ni lazima kuwe na tofauti ya matajiri na masikini.
Aidha, aliongeza kuwa anauhakika tatizo la sukari ni la muda mfupi na litakwisha hivi karibuni kwani tayari maelfu ya tani za sukari yameshaagizwa na yanatarajiwa kuingia nchini.
SOURCE:Gazeti la RAI