Rais Magufuli awaombe msamaha matajiri

Rais Magufuli awaombe msamaha matajiri

Nyie watu wote hakuna mlijualo ni wapi imeandikwa kuchangia maafa ni wajibu wa matajiri ?? Swala la kuchangia ni hiyari ,na si lazima ,hili linatokana na mtu alivyo guswa na tukio husika, na hakuna lolote la kumfanya asipo changia na ndio maana hata serikali inawaomba haiwaamrishi msiwe wajinga kiasi hiki, yaan kweli chama changu cha mapinduzi kimedumaza fikra za vijana wake wengi aisee tena wewe Lizaboni huwa ni mrukiaji wa mambo mengi ambayo huyafahamu wala huyajui huwa unatia aibu mara nyingi sana kwa kuongea nonsense ,hata kama ni kuitetea serikali wakati ,wingine unatia aibu kupindukia.
Social responsibility inakulazimu kurudisha kwa wale uliowakamua
Ndio maama hata buzwagi wanatoa mirahaba,wanajenga shule na hospitali
 
Hovyo kabisa,sasa ulitaka hela atoe masikini?
Pote duniani hata marekani kina Bill Gates wanachangia maafa
Hiyo ni social responsibility yao
Chadema na ukawa mnatumia maafa kisiasa hii ni mbaya sana
ALitaka wote tuishi kama mashetani/masikini.. leo nani angechanga hiz 1.3B?
 
Social responsibility inakulazimu kurudisha kwa wale uliowakamua
Ndio maama hata buzwagi wanatoa mirahaba,wanajenga shule na hospitali
Kitu cha msingi unacho takiwa kukijua na ukubali kubadilika kimawazo ni kwamba swala la kujitolea kwenye maafa kwa matajiri ni la hiyari kulingana na uzito na kuguswa kwa muhusika si la lazima hata kidogo na ndio maana hata serikali huwa inatumia lugha ya kuwaomba tena sana na sio kuwataka au kuwapa amri maana hata serikali inajua hiyo ni hiyari ka hao kufanya hivyo ,ni jukumu la serikali kuhangaikia maafa na ndio maana kuna mfuko wa maafa na una budget yake ,kubali kuelimishwa na kuelimika usiwe mpumbavu.
 
Kwa hiyo Okwi ulikuwa unataka matajiri walambwe miguu?.

Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwenye kuingiza pato maishani.

Kusaidia jamii inayokumbwa na maafa ni wajibu pia wa kila mtu.

Iwapo ungeniambia kwamba ipo haja ya viwango vya kodi kupunguzwa kwa sababu ya tax base kuongezeka, hapo ningekuelewa lakini sio kusema matajiri wanyenyekewe na kuwa na nguvu kuliko mwananchi wa kawaida.

Hiyo jamii ambayo mwenye fedha anaogopwa, ndio ile ambayo imetufikisha hapa.
 
Kitu cha msingi unacho takiwa kukijua na ukubali kubadilika kimawazo ni kwamba swala la kujitolea kwenye maafa kwa matajiri ni la hiyari kulingana na uzito na kuguswa kwa muhusika si la lazima hata kidogo na ndio maana hata serikali huwa inatumia lugha ya kuwaomba tena sana na sio kuwataka au kuwapa amri maana hata serikali inajua hiyo ni hiyari ka hao kufanya hivyo ,ni jukumu la serikali kuhangaikia maafa na ndio maana kuna mfuko wa maafa na una budget yake ,kubali kuelimishwa na kuelimika usiwe ********.
Kwa suala hilo kuwa ni hiyari, wala sio kigezo cha tajiri au mfanyabiashara kuja na masharti kwa serikali. Mabilionea wa nchi za dunia ya kwanza wanalipa kodi na wanachangia fedha yanapotokea maafa.
 
Kitu cha msingi unacho takiwa kukijua na ukubali kubadilika kimawazo ni kwamba swala la kujitolea kwenye maafa kwa matajiri ni la hiyari kulingana na uzito na kuguswa kwa muhusika si la lazima hata kidogo na ndio maana hata serikali huwa inatumia lugha ya kuwaomba tena sana na sio kuwataka au kuwapa amri maana hata serikali inajua hiyo ni hiyari ka hao kufanya hivyo ,ni jukumu la serikali kuhangaikia maafa na ndio maana kuna mfuko wa maafa na una budget yake ,kubali kuelimishwa na kuelimika usiwe ********.
Kwa hiyo wewe umechukia sana matajiri kutoa michango ya maafa
Ukawa mpo tayari hata kama watanzania wenu wafe ili tu serikali ipate pa kulaumiwa
 
Kwa hiyo Okwi ulikuwa unataka matajiri walambwe miguu?.

Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwenye kuingiza pato maishani.

Kusaidia jamii inayokumbwa na maafa ni wajibu pia wa kila mtu.

Iwapo ungeniambia kwamba ipo haja ya viwango vya kodi kupunguzwa kwa sababu ya tax base kuongezeka, hapo ningekuelewa lakini sio kusema matajiri wanyenyekewe na kuwa na nguvu kuliko mwananchi wa kawaida.

Hiyo jamii ambayo mwenye fedha anaogopwa, ndio ile ambayo imetufikisha hapa.
hapana mkuu sitaki matajiri walambwe miguu bali waheshimiwe na kauli za kuwaunganisha watanzania wote bila kujali hali zao.ni rais wa vyama vyote.hii haimuondolei nguvu ya kuwatumbua mafisadi
 
Sahihi kabisa Mkuu. Matajiri kuchangia maafa ni wajibu wao na si hiari. Magufuli anawachora tu pembeni. Ole wao wale watakaokaa kimya.
Wacheni vitisho visivyo na maana kwahiyo usipochangia ndio utafungwa jela .? Eti ole wako watakaokaa kimya hovyo kabisa wewe. Huo utajiri alimsaidia kuutafuta.
 
Matukio haya ni "maandishi yaliyoandikwa ukutani" yakiuonya ufalme huu uliofitinika,uongozi uliofeli vipimo vya utawala bora,ukapungua katika masuala ya kuliunganisha Taifa na badala yake umetumika kulipasua vipande vipande hauwezi kamwe kuendelea.

Dalili za kuanguka kwa ufalme huu zi dhahiri,wakati waliopo nje ya "boma" wakiendelea kumtukuza mfalme,yeye aliye ndani ya boma anajihisi kuelemewa na mzigo mzito,amechanganyikiwa na hajui la kufanya,sasa hivi kila alisemalo linageuka kuwa sumu iuwayo Mshikamano wetu,kinywa chake kimekuwa upanga ukatao kuwili,kinakata na kumpatiliza kila ampingaye ndani ya dk.5

Bado kitambo kidogo kama busara hazitatumika,kama mfalme hatofanya toba,kama akiendelea kushupaza shingo,ndiposa tutashuhudia anguko kuu la Taifa litakaloletwa na mbegu za chuki,ubaguzi na ukandamizwaji wa haki zipandwazo na wale tuliowapa dhamana ya kuliunganisha Taifa letu.

Hapo ndipo tutakapozikumbuka sauti za Mh.Mbatia,sauti ya kumlilia "Mama Tanzania". Kama vile mwanamke mwenye busara awezavyo kuijenga nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe,ukosefu wa busara hurudi kuwa uharibifu wa nyumba yake mwenyewe,ni busara pekee ziwezazo kuliokoa Taifa toka kwenye anguko linalotunyemelea kwa kasi.
 
Hovyo kabisa,sasa ulitaka hela atoe masikini?
Pote duniani hata marekani kina Bill Gates wanachangia maafa
Hiyo ni social responsibility yao
Chadema na ukawa mnatumia maafa kisiasa hii ni mbaya sana
hovyo kabisa, amesema aache kuwasimanga!
 
Kwa hiyo wewe umechukia sana matajiri kutoa michango ya maafa
Ukawa mpo tayari hata kama watanzania wenu wafe ili tu serikali ipate pa kulaumiwa
Komaza akili ndugu usiwe mtumwa wa fikra mimi sio mnafiki na wala sio ukawa ila sipendi unafiki kugeuza njano kuwa nyeusi nasimamia uhalisia na hilo linanifanya mionekane mwana ukawa na hivyo basi kama kuongelea ukweli na uhalisia ni kuwa mwana ukawa basi niko radhi kubatizwa uanachama huo ila nitasimamia ukweli na sitaufunika ukweli sipingi matajiri kutoa misaada na ninawaunga mkono maana hata mimi nimefanya kwa sehemu yangu kwenye maafa yaliyo tokea eneo ninalo ishi lakini ukubali kuelimika kuwa swala la kutoa misaada ni la hiyari sio kama mnavyo dannganyana na shoga yako Lizaboni kuwa ni lazima mnakosea kusema hivyo na hampo sawa hata kidogokidogo msishirikiane kwa mambo ya kinafiki simamia ukweli unao uona wewe na nafsi yako ikushuhudie kweli SIPENDI UNAFIKI NA SITAUPENDA KAMWE.
Kwa hiyo wewe umechukia sana matajiri kutoa michango ya maafa
Ukawa mpo tayari hata kama watanzania wenu wafe ili tu serikali ipate pa kulaumiwa
 
Hovyo kabisa,sasa ulitaka hela atoe masikini?
Pote duniani hata marekani kina Bill Gates wanachangia maafa
Hiyo ni social responsibility yao
Chadema na ukawa mnatumia maafa kisiasa hii ni mbaya sana
Pesa za kuvunja UKUTA zipo lakini za maafa madawati nk mnachangisha watu , mngesikia chadema wanafufua UKUTA Pesa za kuvunja ingepatikana haraka sana .
 
Kwa watanzania hawa KUWA TAJIRI ni sawa kuwa UTUMWANI ni hisani tu ya mwenyezi MUNGU kuendelea kuwalinda na mali zao, hakika akitokea kiongozi wa kuwanyanganya mali zao na kugawia maskini nchi nzima itakuwa vigelegele na shangwe, Hakika ukimchukia Tajiri usitegemee wewe na family yako kuwa iko siku utapata mali, na ukikaa unamtamani Tajiri (role model) hakika iko siku ndani ya family yako UTAJIRI UTAPIGA HODI km sio wewe mwenyewe.

Watanzania msitegemee neema ya mali, kwa kuendelea kuwa bagua matajiri, tutabaki omba omba na masoko ya nchi kama kenya n.k.
Uko sahihi kabisa mkuu napenda sana mtu siye na chembe ya unafiki ,aana hata ona haya kuuongea ukweli
 
hapana mkuu sitaki matajiri walambwe miguu bali waheshimiwe na kauli za kuwaunganisha watanzania wote bila kujali hali zao.ni rais wa vyama vyote.hii haimuondolei nguvu ya kuwatumbua mafisadi
Matajiri wa nchi hii walifikia wakati ambapo wakageuka Miungu watu, wakashindwa kukumbuka ukweli kwamba kila mtu anapaswa kuwa mtenda haki kwa nafasi yake kwenye jamii. Rais JPM hajawadharau bali anawakumbusha tu kuhusiana na kujinyenyekeza na kujishusha maishani.
Unakumbuka issue ya yule mke wa waziri ambaye alijibizana hovyo na traffic police?. Hakuna anayepaswa kujiona yupo juu ya sheria, na kujiona anao ushawishi mkubwa kiasi cha sheria na matakwa yake kuwa sio kitu mbele yake.
 
Hovyo kabisa,sasa ulitaka hela atoe masikini?
Pote duniani hata marekani kina Bill Gates wanachangia maafa
Hiyo ni social responsibility yao
Chadema na ukawa mnatumia maafa kisiasa hii ni mbaya sana
Nafikiri wewe ndo utakuwa hovyo zaidi...kusema yeye ni rais wa maskini si suala la kushabikia.....
 
ALitaka wote tuishi kama mashetani/masikini.. leo nani angechanga hiz 1.3B?
Pesa zilizotumika kupangua UKUTA zingeweza kuwajengea nyumba wote waliothirika na Hilo janga la tetemeko , hata Pesa anayolipwa Lipumba Kwa ajili ya kuvuruga Upinzani ingeweza kusiadia mengi cha ajabu Pesa za kudhoofisha Upinzani zipo nyingi tu , lakini Pesa za kukabiliana na maafa na kununulia madawati wanachangisha watu .
 
Back
Top Bottom