Baada ya kukamilika siku 14 za msamaha kwa wahujumu, Je Rais Magufuli atumie busara za Harun El Rashid kuwasamehe ambao hawakuandika barua? Au...!.

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
βœ…
35,671
2,000
Wanabodi,

Zile siku 14 za msamaha wa rais Magufuli za kuandika barua kukiri makosa na kuahidi kutorudia tena na kulipa walichoiba zimekamilika. Ofisi ya DPP imeishaanza kuzifanyika kazi kwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani ili kuisajili misamaha hiyo kimahakama, kwa barua hizi kupokelewa mahakamani kama uthibitisho wa kukiri kutenda kosa, mahakama itatoa hukumu ya kiasi fulani cha faini ya makosa hayo, mtuhumiwa akilipa faini hiyo anaachiliwa na kuendelea kulipa lile deni alilosababisha kidogo kidogo kwa utaratibu watakaokuwa wamekubaliana na DPP. Hivyo watuhumiwa wenye cash cash ya ukweli, kuanza kuanza kuachiliwa anytime from now maana barua hizo zimeanza kuwasilishwa mahakamani siku ya jana.

Hoja ya bandiko hili ni ni kwa wale ambao wana kesi za uhujumu na utakatishaji fedha, lakini hawajaandika barua za kukiri makosa na kuomba msamaha. Jee kutoandika barua huko ni uthibitisho kuwa wamebambikiwa?. Jee tuwaombee msamaha kwa rais Magufuli atumie uadilifu wa Harun El Rashid kuwasamehe?.

Uandilifu wa Harun El Rashid katika kushughulikia mashauri, nimeuzungumza hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...u-harun-el-rashid-wa-alfu-lela-ulela.1194175/
Lakini kwa faida ya wale wavivu kufuata links, ninakuwekea hapa kisa kimoja cha Mwanamke Tajiri na Mwanamke Masikini kilichoamuliwa na Harun el Rashid.
Kayafa Mkuu Khalifa Harun El Rashid.
Kwa wale wa zamani waliosoma vitabu hadithi vya Hekaya za Abunuwas na Alfu Lela Ulela, hadithi nyingi zimemzungumzia Kayafa Mkuu wa Baghdad enzi hizo kwa jina la Khalifa Mkuu, Kayafa Harun El Rashid alivyokuwa ni mtu wa kutenda haki bin haki kwa kutoa haki kwa wote wakiwemo wanyonge, maana kikawaida mnyonge huwa hana haki mpaka mwenye nguvu aseme.

Moja ya simulizi hizo ni kisa cha mwanamke mjane masikini aliyeachwa kizuka na msiba wa mumewe mpenzi waliopendana sana na kuishi muda mrefu bila kujaaliwa kupata mtoto hadi mumewe anafariki hawakubahatika kupata mtoto.

Katika mji huo kukawa na tajiri mkubwa mwenye mali nyingi, wake wengi, watumwa wengi, mifugo mingi, in short alikuwa na kila kitu isipokuwa hakubahatika kupata mtoto na sasa umri umekwenda. Akatoa nadhiri kwa mke wake yeyote atakaye mzalia mtoto, mtoto huyo ndie atakuwa mrithi wa kila kitu pale atakapofariki na ni mama atakayepata mtoto ndio atarithi kasri lake. Then just imagine harakati za kusaka ujauzito miongoni mwa wake wa tajiri huyo. Huku na kule mara paa!, mke mdogo wa tajiri huyo kashika ujauzito, (wanawake wakisasa wakigundua kushika ujauzito wa tajiri ni dili, hata kama tajiri mwenyewe hawezi kushikisha ujauzito, atashikishishwa or ikishindikana kabisa kumshikishisha, then, atashikishiwa!).

Mwanamke wa Kiislam akifiwa na mumewe, hukaa edda siku 90 ili kujiridhisha mwanamke huyo yuko ok na hana kiumbe cha al marhum, baada ya siku 90 akiwa OK, anaruhusiwa kuolewa tena, lakini alikutwa na ujauzito wa marehemu mumewe hivyo anakuwa hawezi kuolewa tena mpaka baada ya uzazi.

Yule mwanamke masikini alifiwa na mumewe, hivyo akakaa edda siku 90, ni kwenye edda, ndipo ikagundulika mwanamke huyo akakutwa na kiumbe, akailea mimba yake kwa taabu, shida, dhiki na mateso hadi siku ya kujifungua.

Kule kwenye kasri la Tajiri nako bi mdogo, mrembo mrembo kweli, akashika ujauzito. Taarifa kumfikia mumewe tajiri, alipata furaha isiyo kifani, akaamuru kuanzia siku hiyo, bi mdogo asifanye kazi yoyote hadi siku ya kujifungua. Mumewe akamuwekea wajakazi wa kutosha hadi kuoga alikuwa haogi tena bali anaogeshwa!. Kwa vile kati ya wake zote wa tajiri yule, ni yeye pekee amebahatika kushika ujauzito, hivyo kuna hatari ya wake wenzie kumuonea vivu, wakamdhuru hivyo akamletea wapishi maalum kumpikia chakula chake, alikuwa na wahudumu zaidi ya 10 wakimuhudumia.

Kufuatia tajiri huyo kuoa wake wengi bila kufanikiwa kupata mtoto, hivyo ujauzito wa mke mdogo ukatiliwa mashaka kama kweli ni wa tajiri, hivyo ikasomwa itkafu, kama kiumbe sio cha tajiri, Allah afanye yake kwa kumtuma Israel kutimiza wajibu wake.

Siku ya uchungu kwa bi mdogo tajiri, ika coincide na siku ya uchungu kwa mwanamke masikini, wakajikuta wamelazwa hospitali moja na usiku huo wakajifungua pamoja, vichanga vya kiume.

Katika kujifungua yule mwanamke tajiri kutokana na kubweteka, hakuwa na mazoezi yoyote, akashindwa ku push, na matokeo ya mwanamke mjamzito akishindwa ku push, tunayajua ndio maana inasisitizwa sana mazoezi ni muhimu kwa wamama wajawazito. Yule mwanamke masikini kutokana na shita, taabu na matatizo, alikuwa ngangari, akajifungua salama bila tatizo lolote, akakiangalia kichanga chake na kukiona kina birth mark ya baba yake kwenye paji la uso wake, hivyo ni copyright ya mumewe kipenzi, akafarijika sana, na kukabidhi kichanga kwa wakunga kikaoshwe.

Kwa vile kichanga cha tajiri ni sii riziki, kichanga cha masikini bukheri wa afya. Mwanamke tajiri, kwa kuijua sababu ya kichanga chake kuwa sii rizki, na lengo ni kuwa mrithi wa utajiri wa mumrwe, huku akiamini kukipora kichanga cha masikini ni kukinusuru kugeuka chokoraa kama mama yake na pia ndio kumsaidia huyo mwanamke masikini asije kitumbukiza kwenye shimo la choo, au kukitelekeza, hivyo akatumia jeuri ya pesa zake, akahonga wakunga kubadilisha vichanga yule bukheri akapewa mwanamke tajiri na yule sii riziki akapewa mwanamke masikini. Yule mwanamke masikini akalia sana kwa uchungu kuwa kichanga bukheri ndie mtoto wake, hakuna aliyemsikiliza!. (masikini huwa hana sauti mbele ya tajiri mwenye pesa),

Kayafa alikuwa na tabia ya kutoka under disguise na kujichanganya na watu wa hali zote na kupata first hand info kwa masikio yake na sio kusubiri kuletewa. Hivyo siku hiyo katika tembea tembea zake, akainyaka hiyo ya kugombea mtoto, kesho yake akatuma ujumbe, wanawake wote wawili waje, waletwe mbele ya baraza lake, tajiri na kichanga bukheri na masikini na maiti.

Khalifa akawasikiliza wote wawili na kusikiliza ushahidi wa mkunga wote wakamkandamiza yule masikini.

Kayafa akatoa hukumu ya haki bin haki kuwa ili kumaliza huo mgogoro mtoto anayegombewa bora agawanywe nusu kwa nusu ili kila mwanamke apewe nusu ya mtoto.

Ukumbi mzima ukazizima kwa makofi na vigelegele kuwa kwenye kila mgogoro wa kugombea kitu, haki bin haki ni kugawana pasu kwa pasu kwa kitu kinachogombewa, ili kila mmoja apate nusu, yaani a win win situation!.

Baada ya ukumbi kutulia akatoa fursa kwa washitaki kutoa neno la mwisho kabla ya utekelezaji wa hiyo hukumu.

Akaanza mwanamke tajiri, huku akionyesha uso wa furaha alimshukuri Khalifa Mkuu Kayafa Harun el Rashid kwa kutoa hukumu ya haki, hivyo mtoto akigawanywa kila mmoja atakuwa ametendewa haki. Ukumbi makofi na vigelegele.

Ilipokuja zamu ya yule mwanamke masikini, yeye aliendelea kulia tuu kwa uchungu na kumuomba Khalifa Mkuu kuwa anaomba kufuta kesi ya kugombea mtoto, na kusema basi yuko tayari kupokea ile maiti ya kichanga ndiye mwanaye na kile kichanga bukheri ni cha mwanamke tajiri, hivyo anaomba msamaha kwa kugombea mtoto wa mwenzake, hivyo hagombei tena na yuko tayari kupokea adhabu ya kifo kwa kusema uongo mbele ya Kayafa.

Ukumbi mzima ukaibuka na kelele za zomea zomea huku wakiimba "asulubiwe!, asulubiwe!". Kwa kawaida mtu ukisema uongo barazani kwa Kayafa Khalifa Mkuu, unahukumiwa kifo kwa kusulubiwa! .

Ndipo Khalifa Mkuu akaunyamazisha ukumbi huku watu wakitaraji hukumu ya kusulubiwa kwa mwanamke masikini ndio inatangazwa kwa sababu ameisha kiri kosa la kusema uongo mbele ya kayafa.

Khalifa akasema kabla sijatangaza hukumu ya kusulubiwa ningependa kumsikia huyu mwanamke kwa nini amedanganya na kuja kukiri barazani ambapo anajua hukumu yake ni kifo?.

Ndipo yule mwanamke masikini huku akiendelea kulia kwa kububujikwa machozi akasema kiukweli kabisa, mtoto hai ni wakwake, na alipozaliwa alimuona na ile alama ya marehemu baba yake kwenye paji la uso wake, lakini kwa vile hukumu ni ya mtoto kugawanywa nusu kwa nusu kila mtu apate nusu, kitendo cha kumgawanya mtoto kwa kuchinjwa, hivyo mwanaye kuuwawa, kuliko mwanae kuuwawa bora akubali tuu kuwa mtoto ni wa mwanamke tajiri ili aendelee kuishi kwa alelewe na mwanamke mwenzake angalau atabaki hai kuliko kuridhia utekelezwaji wa hukumu ile, na kwa jinsi anavyompenda mwanae, baba yake ameishakufa, kama mtoto atagawanywa, na yeye atakufa kwa kihoro, hivyo ameamua bora aseme kuwa amedanganya, ili akubali kuutoa uhai wake kumuokoa mwanaye.

Ndipo Kayafa Mkuu Khalifa Harun El Rashid akatoa hukumu ya haki bin haki. Akaamuru mtoto akabidhiwe kwa mwanamke masikini na atahudumiwa na serikali maisha yake yote na kibao kikamgeukia mwanamke tajiri na wakunga waliokula ile dili.
Katika wahujumu na watakatishaji fedha, kuna makundi matatu ya watu na aina tatu za wahujumu.
Tukianza na makundi ya wahujumu, kuna wahujumu wakubwa, matajiri wenye uwezo wa kulipa chochote. Kuna wahujumu wa kati ambao ni watu wa kawaida, na wahujumu wadogo, masikini wa kutupwa hata wakiandika barua za msamaha, hawana uwezo wa kulipa chochote.
Tukija makosa ya uhuhujumu ya kuombea msamaha
1. Kuna Wahujumu kweli na watakatishaji kweli pesa, hawa wataomba msamaha na pesa wanazo na watalipa pale pale watakuwa huru.
2. Wahujumu waliohujumu kidogo na kubambikiwa kesi kubwa, hawa pia wataandika barua na kulipa kulipa kidogo kidogo.
3. Waliobambikiwa kesi za uhujumu, kwenye kundi hili la waliobambikiwa, nako kuna makundi matatu yake.
1 Waliobambikiwa lakini ni matajiri, hawa wataandika barua na kukiri uhujumu ili tuu kuununua uhuru wao kwa gharama yoyote, hawa watalipishwa na watalipa ila kwa vile wamelazimika kukubali tuu ili wawe huru, fedha zao zina bad karma ya malipizi, Mungu atawalipia.
2. Kuna waliobambikiwa ni watu wa kawaida na wengine ni masikini, hawa pia wangetamani kuandika barua wakiri watoke na wengine watakuwa wameandika barua kukiri kwa kusisitiza kuwa wamesingiziwa, ili watoke, lakini pia watakiri kuwa wangekuwa na fedha pia wangelipa, hawa pia wanapaswa kuachiwa bila kulipa chochote.
3. Kundi la tatu, hawa ni watu wakweli, ambao wataamua kusimama na ukweli mpaka mwisho kuwa wao wamesingiziwa, sio wahujumu, hawataandika barua za kukiri makosa ya kubambikiwa, au wakiandika sio kukiri bali kusisitiza wamesingiziwa, hawa ndio Mungu atasiimama nao.

Sasa kwa kuutumia uadilifu na busara kama za Khalifa Harun el Rashid, jee tumuombe rais Magufuli atumie huruma yake na busara zake kuwasamehe kwa kumuelekeza DPP (japo DPP hatakiwi kuelekezwa, siku hizi DPP anaelekezeka!), kutumia powers zake za Nolle kwa kuwatendea haki watu hawa waliobambikiwa kesi za uhujumu kwa kuzifuta kesi zao?.

Kama nilivyo sisitiza wakati wa kumpongeza rais Magufuli kwa uamuzi huu, naendelea kusisitiza rais Magufuli akitenda haki, yeye atabarikiwa na taifa litabarikiwa. Hawa watu waliobambikiwa kesi za uhujumu wakati kiukweli kabisa sio wahujumu, nao watendewe haki.

Hivyo tumuombe rais Magufuli, aombe kupewa majina ya wahusika wote wa kesi zote za uhujumu aangalie ni wangapi hawaja andika barua za kukiri na kuomba msamaha?, then hao wote ambao hawajaandika barua, ndio watakuwa wamebambikiwa, ili ikimpendeza, ndipo amuelekeze DPP, hao wote waachiwe kwa Nolle, watakuwa ni kweli wamesingiziwa na wakiachiwa watakuwa wametendewa haki.
Mungu mbariki rais Magufuli,
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
27,992
2,000
Amegoma kutoa majibu ya uvumi wa kumchoma kabendera, kwa hiyo kila mtu aamini kivyake
Ila uzi ambao umeweka kama nusu saa iliyopita, ni mwanajf analalamika kuwa watoto wa Pasco wa kiume wana tabia ya kuzalisha wanawake ovyo ovyo halafu wanakimbia kutoa matunzo. Sasa mleta uzi alikuwa analalamika kuwa Pasco anaweka mabandiko ya maana hapa JF lakini ameshindwa kudhibiti wanae wasiwatie mimba wenzao ovyo ovyo
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
28,804
2,000
Ila uzi ambao umeweka kama nusu saa iliyopita, ni mwanajf analalamika kuwa watoto wa Pasco wa kiume wana tabia ya kuzalisha wanawake ovyo ovyo halafu wanakimbia kutoa matunzo. Sasa mleta uzi alikuwa analalamika kuwa Pasco anaweka mabandiko ya maana hapa JF lakini ameshindwa kudhibiti wanae wasiwatie mimba wenzao ovyo ovyo
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
Kama wanawake wanajipeleka wenyewe na kijana wake ni mzima afanye nini sasa, hata ingekuwa mimi ningekaa kimya tu
 
koyola

koyola

JF-Expert Member
2,354
2,000
Amabaye hajaomba msamaha anauhakika kuwa ataahinda kesi....na huenda anaushahidi wa kutosha tutomkuta na hatia, waachwe na maamuzi Yao
 
O

Oumuamua

JF-Expert Member
843
1,000
Oh! Sasa nimeanza kuelewa, kumbe haikuwa Plea bargain kama sheria inavyotaka. Ilikuwa amnesty for economic saboteurs ila tofauti na amnesty nyingine hii inabidi ulipie. Kweli kama taifa tumesonga mbele, hii nchi lazima iende mbere.
 
M

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
1,494
2,000
Mkuu Pascal Mayalla nashukuru kwa bandiko lako. Naomba niulize maswali machache:-
1. Hivi hao watuhumiwa waliokiri makosa yao wakishindwa kulipa hizo pesa (By Installment) kama walivyokubaliana na ofisi ya DPP watarudishwa mahakamani

2. Hivi kumbukumbu za kimahakama baada ya watuhumiwa kukiri makosa ya mashitaka yao zitakuwa vipi? Je zitaonyesha kwamba wahusika walikuwa wanashitakiwa kwa mashitaka ya kuhujumu uchumi na kushindwa kesi?

Ahsante
 
Wamweru

Wamweru

JF-Expert Member
479
500
Bandiko zuri Sana Ila sio wote ambao watakataa kuandika barua ni kuwa hawajafanya hayo Kuna wengine wamefanya hayo na wakapokea Chao wakatumia vibaya sasa hata wakiandika barua watalipa nn?

Na Kuna wale kwa kutaka kujifanya wasafi ktk jamii wakati wamefanya hayo nao wamekataa kuandika barua na sio lazima kuandika barua na wamechangua njia Yao.

Hivyo kwa wote ambao hawakuandika barua kesi zao zitaendelea vile vile na mahakama ndio mwamuzi wa mwisho kama wana makosa au la.
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
34,331
2,000
Kama utaratibu wa kukamata MTU kumshtaki ungekuwa ni baada ya upelelezi kukamilika. Au ile sheria kwamba DPP akimuweka mtu ndani upelelezi ukamilike ndani ya Siku sitini ingeheshimiwa basi ni wazi hata Leo hii hata waomba msamaha wangekuwa wachache sana.
Lakini haya mambo ya kusota miaka mitano eti uchunguzi bado hakuna anayekubali
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
βœ…
35,671
2,000
Ila uzi ambao umeweka kama nusu saa iliyopita, ni mwanajf analalamika kuwa watoto wa Pasco wa kiume wana tabia ya kuzalisha wanawake ovyo ovyo halafu wanakimbia kutoa matunzo. Sasa mleta uzi alikuwa analalamika kuwa Pasco anaweka mabandiko ya maana hapa JF lakini ameshindwa kudhibiti wanae wasiwatie mimba wenzao ovyo ovyo
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
Naomba link ya hilo bandiko, umri wa mtoto Kitanzania kwa maana ya minor ni under 14, the age of majority kwa Tanzania ni 18 years. Hao wanaoitwa watoto ni watu wazima wamemaliza vyuo vikuu, wanakaa makwao na wana maisha yao, they are adults na wako responsible kwa maisha yao.
P
 
M

mbongopopo

JF-Expert Member
1,481
1,500
Aliwapa siku 7, akaongeza 7 zingine kwa kuwahurumia. Unashangaza kutaka achukue atua zingine, kama vile hao wahusika hawakupewa nafasi ambayo alisema hatairudia tena. Kwa sasa wapambane na uamuzi wao tu. Kuna walioiba kuku na maziwa na vitu vidogo wapo jela na hata waliosingiziwa kesi. Bora awaangalie hao sasa kuliko hao walioiba pesa nyingi, na ambazo bado wanazo wanavizia mahakama itaamua nini.

Ushauri wako huu akiufata, atajishusha sana. Kuna mengi zaidi ya yeye kutoa nafasi kwa wananchi wengine na yanayowakabiri.
 
N

Nanye Go

JF-Expert Member
5,669
2,000
Kesi zimepungua sasa uchunguzi uharakishwe na mahakama itoe haki kwa watuhumiwa.

Vyombo vya uchunguzi vimerahisishiwa na kupunguziwa mzigo, sasa wachunguze zilizobaki na kesi ziungurume.
 
M

mulaga

JF-Expert Member
3,163
2,000
Ofisi ya DPP ingekuwa iko serious kutafuta ushahidi wasingemaliza hata mwezi mahabusu.Ila kesi za kubambikwa hata wakae miaka 60 ushahidi hautokamilika.
 
M

mulaga

JF-Expert Member
3,163
2,000
Kama utaratibu wa kukamata MTU kumshtaki ungekuwa ni baada ya upelelezi kukamilika. Au ile sheria kwamba DPP akimuweka mtu ndani upelelezi ukamilike ndani ya Siku sitini ingeheshimiwa basi ni wazi hata Leo hii hata waomba msamaha wangekuwa wachache sana.
Lakini haya mambo ya kusota miaka mitano eti uchunguzi bado hakuna anayekubali
Sheria zetu zinaupofu mwingi sijui kazi ya mwanasheria mkuu halioni hili.Jela ni nyumbani kwa kila mtu Leo kwao kesho kwake,sawa na dikteta bashir kulalamika ubovu Wa gereza alilopo hali angewezafanya kitu.Huu utaratibu wa kumkamata mtu mahabusu aoze ndani kwanza ndo ushahidi utafutwe ni Wa wapi huu ni sheria au ni mazoea kwa hali hii yafaa kweli kuwekwa kwenye kundi la jamii ya watu walioelimika na kustaarabika? Unamkamata vipi mtu kama ushahidi haujakamilika?
 

Forum statistics


Threads
1,424,956

Messages
35,077,075

Members
538,169
Top Bottom