Rais Magufuli atumbua mapapa wa Madawa ya Kulevya (unga)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,850
34,300
gari.jpg

Kasi ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu sasa imeanza kuvunja mtandao wa dawa za kulevya (unga) nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.

Rais Magufuli ametoa maelekezo mahsusi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akielekeza kuwa anataka kuiona Tanzania isiyokuwa na wauzaji na watumiaji ‘unga’.

Rais amenukuliwa akisema haiwezekani wauza unga wakawa na nguvu kuliko Serikali.

Tayari maofisi wa Serikali wameanza kulifanyia kazi agizo hilo kimyakimya na kwa kasi ya aina yake, ambako sasa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakihoji wafanyabiashara wenye ukwasi usioelezeka na katika kufanya hivyo wamekutana na ‘maajabu’.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imeanzisha operesheni ya kukamata wafanyabiashara wote wanaohusishwa na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

Katika operesheni hiyo, tayari polisi wamekamata ‘mapapa’ wawili wanaoelezwa kuwa miongoni mwa ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu nchini. Mapapa hao wanashikiliwa Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni.

Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni umeanza msako mkali wa kimyakimya kwa wafanyabiashara hao; operesheni inayoelezwa kuwa inahusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Usalama wa Taifa na kitengo maalum kutoka Ikulu.

JAMHURI limethibitishiwa kuwa Hemed Horohoro na Lwitiko Samson Adam, ni kati ya mapapa waliokuwa wakisakwa kwa udi na uvumba na sasa wametiwa nguvuni.

Lwikito ambaye anaelezwa kuwa na makazi nchini Afrika Kusini, alikamatwa nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam. ‘Papa’ huyo, amekutwa kwenye ‘nyumba ya ajabu’.

“Huwezi kuamini. Lwitiko aliishi maisha ya peponi. Ukiiona nyumba yake pale Magomeni, nje si nyumba ya maana, lakini ukiingia ndani utashangaa. Nyumba imejengwa chini ya ardhi (underground). Huko kuna maisha ya peponi.

“Kule chini ya ardhi ana bwawa kubwa la kuogelea huko huko, baa na magari yote ya kifahari yapatayo manane tuliyakuta huko chini ya ardhi, tulistaajabu,” anasema mmoja wa watu waliofanya kazi ya kumkamata.

Magari yaliyokuwa huko chini ya ardhi mengine yana thamani ya hadi Sh milioni 500. JAMHURI limefanikiwa kupiga picha sehemu ya magari hayo katika Kituo cha Polisi Oysterbay, ambayo yamo BMW X6, Lexus, Lumma CLR RS, Cooper na mengine ya kifahari.

Wakati Lwitiko akikamatwa na baadhi ya mali zake, Hemed alikamatwa na gari moja ambalo nalo pia linashikiliwa katika kituo hicho.

Watuhumiwa hao waliokamatwa wanatajwa kuwa wamekuwa wanauza dawa aina ya heroine kutoka Pakistan; cocaine kutoka Brazil, huku wakiishi maisha ya kifahari nchini Tanzania na Afrika Kusini.

Katika kinachohofiwa kuwa taarifa zimevuja ukamataji ulipoanza wiki iliyopita, kundi kubwa la wafanyabiashara waliolengwa lilikimbia nchi.

“Wengi wamekwenda Kenya na Afrika Kusini. Weengine wameikimbia Dar es Salaam, taarifa za kiintelijensia zinaonyesha wako mikoani, lakini kwa vyovyote vile chini ya Rais [John] Magufuli wanapoteza muda. Watakamatwa tu,” amesema mtoa habari wetu.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, ACP Christopher Fuime, anasema ukamataji huo ni endelevu, lakini hakutaka kuingia kwa undani zaidi akisema wananchi wasubiri kuona ‘wazungu wa unga’ wote wanapotea mtaani.

Anasema kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya si watu wadogo, bali wana uwezo na wanamiliki mtandao mkubwa, hivyo kukabiliana nao kunahitaji “muda na usiri mkubwa”.

Alipoulizwa ni lini wanatarajia kuwafikisha mahakamani ‘mapapa wawili’ waliokamatwa, amesema hawezi kuzungumzia hilo kwani upelelezi bado unaendelea na kwamba unahusisha taasisi nyingi, hivyo ni vigumu kubainisha hilo.

Hata hivyo, amekiri kukamatwa kwa Horohoro na Lwitiko na anasema: “Hapa tunafuatilia mambo mengi. Tunavyopeleleza kesi za dawa za kulevya tunaangalia umiliki wa mali, utakatishaji wa fedha, na mambo mengine mengi. Ila kwa sasa tumeamua ingawa wengine wanakimbia baada ya kubonyezwa, lakini hiyo siyo tatizo,” anasema Kamanda Fuime.

Katika eneo la kutakatisha fedha za dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanamiliki mabasi yanayofanya kazi ya daladala jijini Dar es Salaam na mengine yanakwenda mikoani.

“Mabasi haya mengi yanatoka Mbagala kwenda Posta, yameandikwa jina la moja ya taasisi kubwa za uzalishaji mafuta duniani, na pembeni yameandikwa majina yao kwa kuongeza herufi mbili mwishoni tu zisomekazo ‘so’. Huyu anaingiza hadi kilo 500 ze heroine kutoka Pakistan, na fedha anazopata anazitakatisha kwa kuonyesha anafanya biashara ya daladala na mabasi ya mikoani,” amesema mtoa habari wetu.

“Wiki iliyopita, Wapakistani sita wameingiza kilo 500 za heroine, wakahifadhi robo Segerea jijini Dar es Salaam, nyingine zimehifadhiwa Pemba, nyingine Zanzibar na nyingine zipo kwenye boti majini hazijaingia nchini,” kiliongeza chanzo chetu.

Ukiacha magari, wanaouza dawa za kulevya wanajenga majengo makubwa katika miji ya Dar es salaam, Zanzibar, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya, kisha wanatumia majengo hayo kudanganya umma kuwa fedha zao zinatokana na kodi ya pango.

Kamanda Fuime, alipoulizwa mkakati wa kupambana na wauzaji waliotajwa kuikimbia nchi, amesema kuzungumzia hilo ni sawa na kuanika mipango ya polisi; jambo ambalo si sahihi.

Miezi miwili iliyopita polisi nchini walifanya uhamisho kwa askari wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na Tanga kuvunja mtandao wa uhalifu, hususan dawa za kulevya ndani ya Jeshi hilo.

Asilimia kubwa ya ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu wapo jijini Dar es Salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Magomeni na Mbezi Beach.

Waziri Kitwanga ameshakabidhiwa orodha ya polisi wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ambako majina hayo aliyakabidhi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Inspekta Jenerali Ernest Mangu.

Baada ya IGP Mangu kukabidhiwa majina hayo, aliwataka askari wa Oysterbay kumkabidhi orodha ya majina ya wauza ‘unga’ haraka.

Mpango huo ulienda sambamba na kuwapangua baadhi ya polisi walioonekana kushindwa kuukabili mtandao wa wauza ‘unga’.

Maofisa waliohamishwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kinondoni Camillius Wambura, aliyepelekwa Manyara na Mkuu wa Utawala Kinondoni, pamoja na baadhi ya askari wa kitengo cha upelelezi na wengine kutoka idara mbalimbali.

Kuhamishwa kwao kulitokana na kushindwa kwao kudhibiti mtandao wa dawa za kulevya nchini, kiasi cha kuifanya Tanzania kuwekwa kwenye orodha ya nchi zinazojihusisha na biashara hiyo kwa kiwango cha juu.

Awali, kabla ya matukio hayo, Tanzania ilikuwa ikitumiwa kama njia ya kupitishia dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini, Ulaya na Amerika, lakini kadri siku zinavyokwenda inakuwa soko la dawa hizo.

Kinachotokea vijana wengi mitaani wanaoitwa mateja, ndiyo wenye kufanya kazi ya kuiba na kupora vitu vya watu mbalimbali. Fedha wanazopata wanazitumia kununua ‘kete za dawa’ na kuzitumia.

Kundi hili limeongezeka, na inaelezwa kuwa wafanyabiashara vijana wa kundi la kati wengi sasa wanatumia dawa za kulevya na hilo ndilo linachangia magari mengi kuwekewa ‘tinted’, kwa nia ya kuficha maovu.

Serikali ya Awamu ya Nne, iliamua kupambana na dawa za kulevya kwa kubadili sheria na ikaelekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, lakini hadi leo chombo hicho hakijaundwa.

Ukiacha kutoundwa kwa chombo hicho, wafadhili walikuwa wakitoa fedha za kununulia dawa ya methodine kwa ajili ya vijana walioathirika na dawa za kulevya, lakini maofisa waliopo katika Tume ya Dawa za Kulevya wakaishia kuzifuja na hivyo mradi ukafutwa.

Matumaini makubwa ya Watanzania sasa yapo mikononi mwa Rais Magufuli, kwani inaelezwa kuwa yeye hana ushirika na wafanyabiashara ambao baadhi yao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

“Tunachosema, Rais sasa achunguze wanaomiliki mabasi, majumba makubwa na biashara zisizoelezeka mitaji yake ilipatikanaje, kisha kuanzia hapo atajua kina nani wanafanya biashara haramu na kina nani wanatumia biashara kutakatisha fedha za dawa za kulevya,” ameshauri mtoa habari wetu.

Gazeti la JAMHURI limekuwa miongoni mwa vyombo vya habari vilivyo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Mwezi uliopita lilichapisha orodha ya wauza unga 560 wanaofanya biashara hiyo nchini, na ambao wengi wao wapo mikononi mwa dola kwa sasa.

Hata hivyo, kumekuwapo madai kuwa wanaokamatwa wengi ni wachuuzi wa chini na wa kati, lakini wahusika wakuu wanaogharimia biashara hiyo, wakiwamo viongozi serikalini na katika vyombo vya dola, wakiwa hawajakamatwa.

Chanzo: Jamhuri
 
Nimependa hicho kipengele cha mateja kujihusisha na uporaji...

Kiukweli ingawa mtu anaweza kudhani kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanawahusu tu wauzaji na watumiaji lakini uhalisia ni kwamba kuna uhusiano chanya (positive correlation ) kati ya matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu kwa ujumla katika jamii...

Kama polisi wanataka kutekeleza wajibu wao wa kupunguza uhalifu katika jamii, basi biashara ya dawa za kulevya ni eneo ambalo wanatakiwa kulidhibiti kwa nguvu zao zote...
 
Du!
Hali ikiendelea hivi, watu tutakuwa tayari kuuwawa tukipambana na maovu kuitetea nchi yetu na raia wake hasa wanyonge. Mengi hayajafanyika bado lakini naona raha kuwa raia wa nchi hii kwa sasa!
Ewe Mungu Baba Mwenyezi Mlinde na kumbariki rais wetu mpendwa.
 
Samson Adam sauzi all maarufu kama tikotiko,mzee wa kugawa kifusi bure kwake ....
VP na yule ambaye anaishi karibu yake mwenye DCM za kumwaga....zmeandikwa T@ wamtumbue...
Na hiyo horohoro mzee wa tbt ktk ile barua kutoka kwa wafungwa gerezani china walimtaja!
 
Kweli chief Mimi nilikuwa nawaambia watu kuwa huyu mkwr akizidi kukaa madarakani tz itakuwa kama mexico,
 
hongera manyerere jackton na balile hivi ndivyo investigation journalism yapaswa kuwa, na mnaitendea haki taaluma yenu kwenye gazeti lenu la jamhuli, ILA! nikukumbushe tukio la kuwindwa na kutaka kuuwawa kwa investgation journalists wawili wa KTN KENYA, Mohamed ally na john allan namu, kupitia kipindi chao cha JICHO PEVU katika makala yao ya PARUWANJA LA MIHADARATI! hadi kupelekea kukimbia nchi na kuomba hifadhi norway, kuweni makini hili genge ni hatari mno! kuliko hata hilo neno lenyewe HATARI!.
 
Samson Adam sauzi all maarufu kama tikotiko,mzee wa kugawa kifusi bure kwake ....
VP na yule ambaye anaishi karibu yake mwenye DCM za kumwaga....zmeandikwa T@ wamtumbue...
Na hiyo horohoro mzee wa tbt ktk ile barua kutoka kwa wafungwa gerezani china walimtaja!
Yule mwenye DCM kibao Kama 20 za Gongolamboto hajakamatwa kumbe? Nasikia Ana ubia na Rizmoko.
 
hongera manyerere jackton na balile hivi ndivyo investigation journalism yapaswa kuwa, na mnaitendea haki taaluma yenu kwenye gazeti lenu la jamhuli, ILA! nikukumbushe tukio la kuwindwa na kutaka kuuwawa kwa investgation journalists wawili wa KTN KENYA, Mohamed ally na john allan namu, kupitia kipindi chao cha JICHO PEVU katika makala yao ya PARUWANJA LA MIHADARATI! hadi kupelekea kukimbia nchi na kuomba hifadhi norway, kuweni makini hili genge ni hatari mno! kuliko hata hilo neno lenyewe HATARI!.
Mohamed Ally ni yule kama msomali ambaye walifanya kazi ya habari pelelezi juu ya mauaji ya wanaharakati wa kiislam akiwemo sheikh aboud rogo Mombasa?kama ni yeye basi sikuwa najua kama ameuawa..ila kwa kazi ya namna ile mimi niliamini kuwa hatokuwa salama...kumbe alitoa ripoti mpk ya wauza sembe?
 
View attachment 325353

Kasi ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu sasa imeanza kuvunja mtandao wa dawa za kulevya (unga) nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.

Rais Magufuli ametoa maelekezo mahsusi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akielekeza kuwa anataka kuiona Tanzania isiyokuwa na wauzaji na watumiaji ‘unga’.

Rais amenukuliwa akisema haiwezekani wauza unga wakawa na nguvu kuliko Serikali.

Tayari maofisi wa Serikali wameanza kulifanyia kazi agizo hilo kimyakimya na kwa kasi ya aina yake, ambako sasa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakihoji wafanyabiashara wenye ukwasi usioelezeka na katika kufanya hivyo wamekutana na ‘maajabu’.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imeanzisha operesheni ya kukamata wafanyabiashara wote wanaohusishwa na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

Katika operesheni hiyo, tayari polisi wamekamata ‘mapapa’ wawili wanaoelezwa kuwa miongoni mwa ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu nchini. Mapapa hao wanashikiliwa Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni.

Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni umeanza msako mkali wa kimyakimya kwa wafanyabiashara hao; operesheni inayoelezwa kuwa inahusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Usalama wa Taifa na kitengo maalum kutoka Ikulu.

JAMHURI limethibitishiwa kuwa Hemed Horohoro na Lwitiko Samson Adam, ni kati ya mapapa waliokuwa wakisakwa kwa udi na uvumba na sasa wametiwa nguvuni.

Lwikito ambaye anaelezwa kuwa na makazi nchini Afrika Kusini, alikamatwa nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam. ‘Papa’ huyo, amekutwa kwenye ‘nyumba ya ajabu’.

“Huwezi kuamini. Lwitiko aliishi maisha ya peponi. Ukiiona nyumba yake pale Magomeni, nje si nyumba ya maana, lakini ukiingia ndani utashangaa. Nyumba imejengwa chini ya ardhi (underground). Huko kuna maisha ya peponi.

“Kule chini ya ardhi ana bwawa kubwa la kuogelea huko huko, baa na magari yote ya kifahari yapatayo manane tuliyakuta huko chini ya ardhi, tulistaajabu,” anasema mmoja wa watu waliofanya kazi ya kumkamata.

Magari yaliyokuwa huko chini ya ardhi mengine yana thamani ya hadi Sh milioni 500. JAMHURI limefanikiwa kupiga picha sehemu ya magari hayo katika Kituo cha Polisi Oysterbay, ambayo yamo BMW X6, Lexus, Lumma CLR RS, Cooper na mengine ya kifahari.

Wakati Lwitiko akikamatwa na baadhi ya mali zake, Hemed alikamatwa na gari moja ambalo nalo pia linashikiliwa katika kituo hicho.

Watuhumiwa hao waliokamatwa wanatajwa kuwa wamekuwa wanauza dawa aina ya heroine kutoka Pakistan; cocaine kutoka Brazil, huku wakiishi maisha ya kifahari nchini Tanzania na Afrika Kusini.

Katika kinachohofiwa kuwa taarifa zimevuja ukamataji ulipoanza wiki iliyopita, kundi kubwa la wafanyabiashara waliolengwa lilikimbia nchi.

“Wengi wamekwenda Kenya na Afrika Kusini. Weengine wameikimbia Dar es Salaam, taarifa za kiintelijensia zinaonyesha wako mikoani, lakini kwa vyovyote vile chini ya Rais [John] Magufuli wanapoteza muda. Watakamatwa tu,” amesema mtoa habari wetu.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, ACP Christopher Fuime, anasema ukamataji huo ni endelevu, lakini hakutaka kuingia kwa undani zaidi akisema wananchi wasubiri kuona ‘wazungu wa unga’ wote wanapotea mtaani.

Anasema kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya si watu wadogo, bali wana uwezo na wanamiliki mtandao mkubwa, hivyo kukabiliana nao kunahitaji “muda na usiri mkubwa”.

Alipoulizwa ni lini wanatarajia kuwafikisha mahakamani ‘mapapa wawili’ waliokamatwa, amesema hawezi kuzungumzia hilo kwani upelelezi bado unaendelea na kwamba unahusisha taasisi nyingi, hivyo ni vigumu kubainisha hilo.

Hata hivyo, amekiri kukamatwa kwa Horohoro na Lwitiko na anasema: “Hapa tunafuatilia mambo mengi. Tunavyopeleleza kesi za dawa za kulevya tunaangalia umiliki wa mali, utakatishaji wa fedha, na mambo mengine mengi. Ila kwa sasa tumeamua ingawa wengine wanakimbia baada ya kubonyezwa, lakini hiyo siyo tatizo,” anasema Kamanda Fuime.

Katika eneo la kutakatisha fedha za dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanamiliki mabasi yanayofanya kazi ya daladala jijini Dar es Salaam na mengine yanakwenda mikoani.

“Mabasi haya mengi yanatoka Mbagala kwenda Posta, yameandikwa jina la moja ya taasisi kubwa za uzalishaji mafuta duniani, na pembeni yameandikwa majina yao kwa kuongeza herufi mbili mwishoni tu zisomekazo ‘so’. Huyu anaingiza hadi kilo 500 ze heroine kutoka Pakistan, na fedha anazopata anazitakatisha kwa kuonyesha anafanya biashara ya daladala na mabasi ya mikoani,” amesema mtoa habari wetu.

“Wiki iliyopita, Wapakistani sita wameingiza kilo 500 za heroine, wakahifadhi robo Segerea jijini Dar es Salaam, nyingine zimehifadhiwa Pemba, nyingine Zanzibar na nyingine zipo kwenye boti majini hazijaingia nchini,” kiliongeza chanzo chetu.

Ukiacha magari, wanaouza dawa za kulevya wanajenga majengo makubwa katika miji ya Dar es salaam, Zanzibar, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya, kisha wanatumia majengo hayo kudanganya umma kuwa fedha zao zinatokana na kodi ya pango.

Kamanda Fuime, alipoulizwa mkakati wa kupambana na wauzaji waliotajwa kuikimbia nchi, amesema kuzungumzia hilo ni sawa na kuanika mipango ya polisi; jambo ambalo si sahihi.

Miezi miwili iliyopita polisi nchini walifanya uhamisho kwa askari wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na Tanga kuvunja mtandao wa uhalifu, hususan dawa za kulevya ndani ya Jeshi hilo.

Asilimia kubwa ya ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu wapo jijini Dar es Salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Magomeni na Mbezi Beach.

Waziri Kitwanga ameshakabidhiwa orodha ya polisi wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ambako majina hayo aliyakabidhi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Inspekta Jenerali Ernest Mangu.

Baada ya IGP Mangu kukabidhiwa majina hayo, aliwataka askari wa Oysterbay kumkabidhi orodha ya majina ya wauza ‘unga’ haraka.

Mpango huo ulienda sambamba na kuwapangua baadhi ya polisi walioonekana kushindwa kuukabili mtandao wa wauza ‘unga’.

Maofisa waliohamishwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kinondoni Camillius Wambura, aliyepelekwa Manyara na Mkuu wa Utawala Kinondoni, pamoja na baadhi ya askari wa kitengo cha upelelezi na wengine kutoka idara mbalimbali.

Kuhamishwa kwao kulitokana na kushindwa kwao kudhibiti mtandao wa dawa za kulevya nchini, kiasi cha kuifanya Tanzania kuwekwa kwenye orodha ya nchi zinazojihusisha na biashara hiyo kwa kiwango cha juu.

Awali, kabla ya matukio hayo, Tanzania ilikuwa ikitumiwa kama njia ya kupitishia dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini, Ulaya na Amerika, lakini kadri siku zinavyokwenda inakuwa soko la dawa hizo.

Kinachotokea vijana wengi mitaani wanaoitwa mateja, ndiyo wenye kufanya kazi ya kuiba na kupora vitu vya watu mbalimbali. Fedha wanazopata wanazitumia kununua ‘kete za dawa’ na kuzitumia.

Kundi hili limeongezeka, na inaelezwa kuwa wafanyabiashara vijana wa kundi la kati wengi sasa wanatumia dawa za kulevya na hilo ndilo linachangia magari mengi kuwekewa ‘tinted’, kwa nia ya kuficha maovu.

Serikali ya Awamu ya Nne, iliamua kupambana na dawa za kulevya kwa kubadili sheria na ikaelekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, lakini hadi leo chombo hicho hakijaundwa.

Ukiacha kutoundwa kwa chombo hicho, wafadhili walikuwa wakitoa fedha za kununulia dawa ya methodine kwa ajili ya vijana walioathirika na dawa za kulevya, lakini maofisa waliopo katika Tume ya Dawa za Kulevya wakaishia kuzifuja na hivyo mradi ukafutwa.

Matumaini makubwa ya Watanzania sasa yapo mikononi mwa Rais Magufuli, kwani inaelezwa kuwa yeye hana ushirika na wafanyabiashara ambao baadhi yao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

“Tunachosema, Rais sasa achunguze wanaomiliki mabasi, majumba makubwa na biashara zisizoelezeka mitaji yake ilipatikanaje, kisha kuanzia hapo atajua kina nani wanafanya biashara haramu na kina nani wanatumia biashara kutakatisha fedha za dawa za kulevya,” ameshauri mtoa habari wetu.

Gazeti la JAMHURI limekuwa miongoni mwa vyombo vya habari vilivyo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Mwezi uliopita lilichapisha orodha ya wauza unga 560 wanaofanya biashara hiyo nchini, na ambao wengi wao wapo mikononi mwa dola kwa sasa.

Hata hivyo, kumekuwapo madai kuwa wanaokamatwa wengi ni wachuuzi wa chini na wa kati, lakini wahusika wakuu wanaogharimia biashara hiyo, wakiwamo viongozi serikalini na katika vyombo vya dola, wakiwa hawajakamatwa.

chanzo.Magufuli atumbua mapapa wa ‘unga’ | Gazeti la Jamhuri

Hapa pana Kazi ngumu kweli lkn tunaimaani na Amiri Jeshi wetu Mkuu, hakuna kurudi nyuma, kinachotakiwa sasa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, vyombo vya habari pamoja na wananchi wote wenye mapenzi mema na nchi yetu tushiriki kuwafichua wote!
 
Sasa tuone kama rais wangu JPM ataweza kuingilia "Capo Di Tutti Capi" na kumkamata Moko au yule jamaa Kinje. Wenzetu wenye nia thabiti waliwezi kuwasambaratisha ma Capo di Tutti Capi wa ukweli kama akina Salvatore Riina au Salvatore Lo Piccolo sijui hawa wetu wenye ushawishi mkubwa kisiasa na wanaingia bungeni kututungia sheria. Hadi namhurumia Magufuli
 
Samson Adam sauzi all maarufu kama tikotiko,mzee wa kugawa kifusi bure kwake ....
VP na yule ambaye anaishi karibu yake mwenye DCM za kumwaga....zmeandikwa T@ wamtumbue...
Na hiyo horohoro mzee wa tbt ktk ile barua kutoka kwa wafungwa gerezani china walimtaja!
Anayemiliki daladala za Posta Mbagala nadhan zile zilizoandikwa [HASHTAG]#OpecTeam[/HASHTAG]
 
Mohamed Ally ni yule kama msomali ambaye walifanya kazi ya habari pelelezi juu ya mauaji ya wanaharakati wa kiislam akiwemo sheikh aboud rogo Mombasa?kama ni yeye basi sikuwa najua kama ameuawa..ila kwa kazi ya namna ile mimi niliamini kuwa hatokuwa salama...kumbe alitoa ripoti mpk ya wauza sembe?
Ndie huyo mkuu, ILA HAJAUAWA BADO YUPO! alionyesha hadi mahala alipokuwa amepangiwa auawe!, google JICHO PEVU youtube ana makala nyingi, pia GURULI YA SAITOTI aliwapa wauza unga siku saba kuwa atawataja bungeni, matokeo yake siku moja kabla ya kuwataja akapangiwa safari na helcopter, ikawa imepuliziwa sumu muda mfupi tu baada ya helcopter kuruka ikapoteza mwelekeo ikiwa angani, ikadondoka na kuua watu wote wa4 waliokuwamo wakiwemo maafisa wakubwa wa polisi na jeshi! HAWA WATU NI HATARI MNO! PINDI WANAPOTAKA KUKUONDOA KWA GHARAMA YOYOTE ILE.
 
Muandishi Wa Gazeti La Jamhuri, Kwanini Haukumuuliza Huyo Kamanda ( MTOA HBR) , Hivi Hao Waliokamatwa Ndio Miongoni Mwa Wale "VIGOGO " Wa Dawa Za Kulevya, Ambao Majina Yao Yako Ktk Ripoti Ya Tume Ya RAIS Mstaafu Wa Awamu Ya 4!!!!??? Alafu Kama Sheria Zimebadilishwa, Ili Kuunda Mamlaka Ya Kudhibiti Dawa Za Kulevya, Na Mamlaka Hiyo Haijaundwa Hadi Leo Na Haijulikani Sababu Za Kupelekea Kushindwa Kwao, Je, Huo Ukamataji Unaendeshwaji!!!?? Na Je, Kukamata Magari, Pesa, Majumba Ni Vielelezo Thabiti Mbele Ya Sheria Za Dawa Za Kulevya Mahakamani!!!?? Kwa Mtazamo Lazima Wale Wanaokamatwa Ni Budi Wakutwe Na "VIELELEZO "Visivyo Acha Shaka Mbele Ya MAHAKAMA!!! SASA Idara Husika Waliokabidhiwa Kazi Hiyo Wasiifanye Kwa Kukurupuka Tu, Ili Kumridhisha "BOSI "Wao Tu, Mwisho Wa Siku Kule Mahakamani Ushaidi Wa Kuwatia HATIANI Ukakosekana!!! Nakumbuka Mno Lile Tukio La MELI Ya Samaki Ya Wachina, Maarufu Kama MELI Ya Samaki Wa MAGUFULI, Tukio Au Kesi Ambayo Imelitia Taifa Hasara Kubwa!!! KAMA Kweli Tuna Nia Thabiti Ya Kupambana Na Biashara Hii, Basi Tuanze Na Ile ORODHA Aliyopewa Mzee Kikwete, Maana Tuliambiwa Na Yeye Mwenyewe Kuwa Ktk ORODHA Hiyo, Kuna Viongozi Wa Dini, Wafanyabiashara Wakubwa, Wanasiasa Na Wananchi Wengine!! SASA Tuanzie Hapo Na Tuunde Hiyo Mamlaka, Na Zoezi Hilo Lifanywe Kimya Kimya Kweli, Sio Kama Hivi Ilivyo Sasa!!!
 
Back
Top Bottom