Serikali ya kamata kilo Milion 2 za dawa za kulevya kuanzia Januari hadi Desemba 2024

Paul02

Member
Oct 25, 2024
30
66
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana Dawa za kulevya nchini, imefanikiwa kukamata Dawa za kulevya zenye uzito wa kilogramu milioni 2 katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2024.

“Hiki ni kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya kuwahi kukamatwa tangu mamlaka hii kuanzishwa, katika dawa zilizokamatwa bangi ilikuwa nyingi zaidi katika dawa zilizokamatwa kwa mwaka 2024 na bangi hizo ni aina ya skanka na hashishi kutoka nchi za nje”, Aretas Lyimo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya.

Aidha Lyimo anasema wamefanikiwa kukamata Jahazi lililokuwa limebeba shehena kubwa ya dawa za kulevya kutoka bara la Asia kuja kwenye nchi mbalimbali barani Afrika.

FB_IMG_1736417366602.jpg
 
Back
Top Bottom