Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya 9 na Wakuu wa Mikoa, Thobias Andengenye awa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mwanri astaafu

isome tena kwa makini; usitoe mawazo yako tu. Katiba inayotumika leo Tanzania ni ile ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000. Soma vifungu hivi vya katiba uniambie wapi kuna neno CCM

View attachment 1497026
View attachment 1497027
View attachment 1497028
Hicho ulichoweka ni vifungu vya uwepo wa hivyo vyeo na watapatikanaje Basi, afu hicho ulichokiweka hapa ndo katiba ya ccm? Mie nilikuambia katiba ya ccm.

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977, tangu chama hicho kilipoanzishwa, wakuu wa wilaya wamekuwa wajumbe wa vikao vyote vikuu vya CCM katika ngazi ya wilaya.

Kwa mfano, ibara ya 76(1)(c) ya Katiba ya CCM toleo la 2010, mkuu wa wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa wilaya; ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya (ibara ya 78(1)(c); na ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya (ibara ya 80(1) (c).
 
Hawateuliwi kwa kufuata katiba ya CCM bali wanateuliwa kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata vifungu hivyo nilivyokuwekea.

CCM inawatatambua (courtesy) wakuu wa mikoa na wilaya kuwa wajumbe wa Kamati za Siasa za wilaya na mikoa yao iwapo tu wakuu hao ni wana CCM- soma vizuri vifungu hivyo usivisome kwa kukurupuka; kuna uwezekano kabisa kuwa wakuu hao siyo wana CCM kwa hiyo hawatakuwa wajumbe wa kamati hizo
1593846970721.png

1593846390406.png

Ni vivyo katiba ya CCM inamtambua spika wa bunge ambaye ni mwana CCM kuwa mjumbe mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya CCM iwapo Spika huyo anatoka CCM. Kuna uwezekana kabisa kuwa Spika akawa siyo mwana CCM kwa hiyo hawezi kuwemo kwenye kamati hiyo. Mwaka 2015 uchaguzi wa spika ulishindanisha wagombea wafuatao wamabo wengi hawakuwa wana CCM: Peter Leonard Sarungi (AFP), Hassan Kisabya Almas (NRA), Dkt. Godfrey Rafael Malisa(CCK), Job Yustino Ndugai (CCM), Goodluck Joseph Ole Medeye (CHADEMA), Richard Shedrack Lyimo (TLP), Hashim Spunda Rungwe (CHAUMMA) na Robert Alexander Kasinini (DP). Kama asingeshinda Ndungai, yaani spika angekuwa ametoka chama kingine, basi spika huyo asingekuwa kwenye Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM

1593846610485.png
 
Hawateuliwi kwa kufuata katiba ya CCM bali wanateuliwa kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata vifungu hivyo nilivyokuwekea.

CCM inawatatambua (courtesy) wakuu wa mikoa na wilaya kuwa wajumbe wa Kamati za Siasa za wilaya na mikoa yao iwapo tu wakuu hao ni wana CCM- soma vizuri vifungu hivyo usivisome kwa kukurupuka; kuna uwezekano kabisa kuwa wakuu hao siyo wana CCM kwa hiyo hawatakuwa wajumbe wa kamati hizo
View attachment 1497213
View attachment 1497209

Ni vivyo katiba ya CCM inamtambua spika wa bunge ambaye ni mwana CCM kuwa mjumbe mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya CCM iwapo Spika huyo anatoka CCM. Kuna uwezekana kabisa kuwa Spika akawa siyo mwana CCM kwa hiyo hawezi kuwemo kwenye kamati hiyo. Mwaka 2015 uchaguzi wa spika ulishindanisha wagombea wafuatao wamabo wengi hawakuwa wana CCM: Peter Leonard Sarungi (AFP), Hassan Kisabya Almas (NRA), Dkt. Godfrey Rafael Malisa(CCK), Job Yustino Ndugai (CCM), Goodluck Joseph Ole Medeye (CHADEMA), Richard Shedrack Lyimo (TLP), Hashim Spunda Rungwe (CHAUMMA) na Robert Alexander Kasinini (DP). Kama asingeshinda Ndungai, yaani spika angekuwa ametoka chama kingine, basi spika huyo asingekuwa kwenye Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM

View attachment 1497210
Kwan kuna mkuu wa wilaya ambaye ni chadema au ACT, wale wote ni CCM, wameweka 'anayetokana na ccm ili ikija tokea serikali haiko chini ya ccm ambapo moja kwa moja na maDC hawatokua ccm wasiingie kwenye vikao, ila kwa serikali hii ya ccm maDC wote ni CCM. Utambue tu DC na RC ni cheo cha kisiasa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mkoa 2 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Sengati alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na anachukua nafasi Bw. Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw.Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Bw.Andengenye anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 9 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, SACP Mlawa alikuwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na anachukua nafasi ya Bw. James Mugendi Ihunyo ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Jamila Yusuf kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Jamila Yusuf alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Bi. Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Ntemo alikuwa Mhandisi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na anachukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Salum A. Kali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kali alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Wilson Samwel Shimo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Shimo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Kanali Kahabi anachukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

Saba, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Abbas Kayanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kayanda alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu na anachukua nafasi ya Bi. Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

Nane, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Lazaro Jacob Twange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Bwana Twange anachukua nafasi ya Bi. Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.

Tisa, Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw.Toba Alnason Nguvila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nguvila alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha na anachukua nafasi ya Bw. Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Bw.Godwin Gondwe anachukua nafasi ya Bw. Felix Jackson Lyaniva ambaye amestaafu.

Kumi, Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Perla Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI). Amechukua nafasi ya Bw. Jumanne Sagini.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 03 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

Wateule:
1. Dr. Philomena Sengati
2. Thobias Andengenye
3. Ismail Twahir Mlawa
4. Jamila Yusufu
5. Martine Ntemo
6. Salum Kali
7. Wilson Samuel Shimo
8. Mathias Kahabi
9. Abbas Kayanda
10. Lazaro Jacob Twange
11. Toba Alnason Nguvila
12. Godwin Gondwe (uhamisho)
13. Marian Perla Mbaga
Tanzania hakuna ukabila, na sote tunajua kuwa kamwe hauwezi kurudi.
Lakini kuna "Kabila yangu"!!
Are we reading from the same page?
 
Kwan kuna mkuu wa wilaya ambaye ni chadema au ACT, wale wote ni CCM, wameweka 'anayetokana na ccm ili ikija tokea serikali haiko chini ya ccm ambapo moja kwa moja na maDC hawatokua ccm wasiingie kwenye vikao, ila kwa serikali hii ya ccm maDC wote ni CCM. Utambue tu DC na RC ni cheo cha kisiasa
Unazungumza hisia zako tu bila kuangalia ukweli, na vile vile hujui tofautikati ya vyeo vya kisiasa na vyeo vya kiserikali. Vyeo vya kiserikali vinatokana na ama uteuzi wa Rais au ajir kupitia utumishi, wakati vyeo vya kisiasa vinatokana ama na uteuzi wa mwenyekiti au kwa kuchaguliwa na wanachama wa chama cha siasa au kwa kupigiwa kura kutokana na vyama- kama madiwani, wabunge, na rais. Unaongea kama vile hujui kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mama anna Mgwira aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wakati akiwa ACT.
 
Kuna kazi inaweza fanywa na mpumbavu yeyote hata umwamshe toka usingizini, lakini kuna kazi bila ujuzi nayo haifanyiki. Mafunzo na muda anaopitia daktari au mhandisi kuhitimu, kisha ukamteua kuwa mkuu wa wilaya ni matumizi mabaya ya maliasili watu. Hiyo ni likizo ya kitaaluma, ambayo baadae kumudu maisha ni kutegemea teuzi.
 
Hilo likitokea Wakristo waende Kanisani wakatoe Sadaka na Waislamu waende Msikitini wakatoe Zaka kwa Mungu kumshukuru kwa kuwakomboa Watanzania toka makucha ya Ibilisi aliyepakwa Mafuta kimakosa.
Kama Malawi limetokea wameweza sisi tushindwe tuna nini?
Na kama Watanzania mnaweka nadhiri ya kumtolea Mungu sadaka na zaka ya shukrani, Mungu ni mwaminifu atatimiza maombi yenu
IMG_20200703_111128.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mkoa 2 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Sengati alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na anachukua nafasi Bw. Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw.Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Bw.Andengenye anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 9 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, SACP Mlawa alikuwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na anachukua nafasi ya Bw. James Mugendi Ihunyo ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Jamila Yusuf kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Jamila Yusuf alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Bi. Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Ntemo alikuwa Mhandisi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na anachukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Salum A. Kali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kali alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Wilson Samwel Shimo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Shimo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Kanali Kahabi anachukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

Saba, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Abbas Kayanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kayanda alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu na anachukua nafasi ya Bi. Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

Nane, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Lazaro Jacob Twange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Bwana Twange anachukua nafasi ya Bi. Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.

Tisa, Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw.Toba Alnason Nguvila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nguvila alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha na anachukua nafasi ya Bw. Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Bw.Godwin Gondwe anachukua nafasi ya Bw. Felix Jackson Lyaniva ambaye amestaafu.

Kumi, Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Perla Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI). Amechukua nafasi ya Bw. Jumanne Sagini.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 03 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

Hao wa zamani si ni wateule wake? Wasingetangaza tu matokeo?
 
Back
Top Bottom