Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya 9 na Wakuu wa Mikoa, Thobias Andengenye awa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mwanri astaafu

JPM ni noma, wenye karama ya kung'amua Mambo wataelewa,

It's a great strategy! Nadhani wakati anarudisha fomu Ali tu pre- empt.

Mawazo binafsi
 
Uteuzi mpya kila siku hizo kazi watazichapa saa ngapi!
Teuzi zingine zinafanyiak kwa sababu walikuwa katika nafasi hizo ni watia nia wa kugombea Ubunge. Kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma, mtumishi wa Umma anayatia nia lazima aachie nafasi aliyonayo. kwa mafano, Mwanri anawezakuwa anaenda kugobea ubunge katika Jimbo la Siha. Pia mara nyingine inatumika lugha nzuri kuwa amestaafu kumbe ameachwa kwa sababu fulani fulani
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mkoa 2 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Sengati alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na anachukua nafasi Bw. Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw.Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Bw.Andengenye anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 9 kama ifuatavyo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, SACP Mlawa alikuwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na anachukua nafasi ya Bw. James Mugendi Ihunyo ambaye amestaafu.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Jamila Yusuf kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Jamila Yusuf alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Bi. Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Ntemo alikuwa Mhandisi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na anachukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Salum A. Kali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kali alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Wilson Samwel Shimo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Shimo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Kanali Kahabi anachukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

Saba, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Abbas Kayanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kayanda alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu na anachukua nafasi ya Bi. Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

Nane, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Lazaro Jacob Twange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Bwana Twange anachukua nafasi ya Bi. Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.

Tisa, Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw.Toba Alnason Nguvila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nguvila alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha na anachukua nafasi ya Bw. Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Bw.Godwin Gondwe anachukua nafasi ya Bw. Felix Jackson Lyaniva ambaye amestaafu.

Kumi, Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Perla Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI). Amechukua nafasi ya Bw. Jumanne Sagini.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 03 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

Kanda inayopendeza GOLI zote. Sifuri wale wengine. Oyee!
 
Naona kuteua maafisa wa jeshi kwenye nafasi za kisiasa sasa limekuwa jambo la kawaida.

Katiba yetu haitaki Afisa wa jeshi awe mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni maofisa wa kiserikali siyo wa kisiasa. Ndiyo maana Mama Mghwira aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa akiwa ACT-Wazalendo; sijui kama baadaye alihama, lakini nafasi zile hazijali wewe ni mwanachama wa chama gani, unaweza usiwe na chama kabisa.
 
Hajatumbuliwa amestaafu

Ni maafisa kiserikali na chama. Ndiyo maana wengi huvaa nguo za chama na kuhudhuria vikao vyote vya chama.
 
Ni maafisa kiserikali na chama. Ndiyo maana wengi huvaa nguo za chama na kuhudhuria vikao vyote vya chama.
Soma katiba kuhusu nafasi hizo. Hawazuiwi kuwa wanachama wa chama chochote lakini majukumu yao siyo ya kisiasa.
 
Soma katiba kuhusu nafasi hizo. Hawazuiwi kuwa wanachama wa chama chochote lakini majukumu yao siyo ya kisiasa.
Katiba ya ccm inamtambua mkuu wa mkoa kama mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa, na DC ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya.
 
Katiba ya ccm inamtambua mkuu wa mkoa kama mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa, na DC ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya.
Hawateuliwi kwa kufuata Katiba ya CCM bali wanateuliwa kwa kufuata Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania; nadhani katiba ya CCM inawatambua wanachama wake ambao wana nafasi hizo. Kumbuka kuwa katiba ya CCM pia inawatambua wabunge ambao ni wana CCM kuwa kamati maalumu ya "CHAMA" lakini tambua kuwa kuna wabunge ambao siyo wana CCM na hivyo hawawezi kuwa wanakamati hiyo.
 
Hii katiba 1977 enzi za chama kimoja. DC yuko kichama na kiserikali.
 
Hii katiba 1977 enzi za chama kimoja. DC yuko kichama na kiserikali.
isome tena kwa makini; usitoe mawazo yako tu. Katiba inayotumika leo Tanzania ni ile ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000. Soma vifungu hivi vya katiba uniambie wapi kuna neno CCM

1593814345683.png

1593814366127.png

1593814381620.png
 
Naona kuteua maafisa wa jeshi kwenye nafasi za kisiasa sasa limekuwa jambo la kawaida.

Katiba yetu haitaki Afisa wa jeshi awe mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Hawaendi kuwa wenyeviti au makatibu wa chama. Bali wanaenda kuwa viongozi wa umma.
 
Kwa hiyo hutaki watu wasitasaafu? Mbona husemi kwa nini watu wanastaafu kila siku hilo huulizi? Kwa hiyo wakistaafu wasiwe replaced?
Tatizo upinzani siku hizi viazi vingi. Yaani watu wamestaafu eti nafasi zao zisizibwe! Ziro kabisa hawa watu.
 
Naona kuteua maafisa wa jeshi kwenye nafasi za kisiasa sasa limekuwa jambo la kawaida.

Katiba yetu haitaki Afisa wa jeshi awe mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Sio kwa Awamu hii na kwa nchi hii kwa kipindi hiki.
 
Mimi tangu Julius Mtatiro alipopewa nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Tunduru na akatulia tulii siamini tena SIASA ZA TANZANIA, hata Upinzani wenyewe ni wa kutilia mashaka sana.
 
Back
Top Bottom