Primitive
JF-Expert Member
- Nov 7, 2011
- 222
- 45
Ndo huyo huyo! Yuko Wizara ya Nishati na Madini, kuna mijitu inaongea isivyovijua ili mradi tuu!!Mume wa Mh. si Andilile Mwainyekule?
Ndo huyo huyo! Yuko Wizara ya Nishati na Madini, kuna mijitu inaongea isivyovijua ili mradi tuu!!Mume wa Mh. si Andilile Mwainyekule?
Nahisi harakati ndo kwisha maana nani atakayekubali kutia kitumbua mchanga!?Tuone Rioba kama ataendelea na uanaharakati wake, ni mtego mbaya sana kwake
Ni kweli mkuu..ila aliye juu yake si unamjua? hapo ndipo mtihani kwa dr unaponzia...pili tunamjua rioba kwa muda wake wote amekuwa ni "mtu wa harakati" vp sasa na mofump yetu tunayoifahamu huyu bwana ataachwa aonyenye utaalamu ili kuleta tija au ndo yaleyale yaliyonpata mzee wetu "Doti"..Dr Rioba ni mpiganaji ,Ilboru boy #HAPA KAZI TU
Mkuu naomba pia ukumbuke yaliyompata mzee wetu yule aliyeletwa kutoka bbc..vp mwisho wake unambuka ushuhuda ulikua upi?Kwa TBC ....! yaani mimi roho kwatu. Nadhani Dr. Rioba hataniangusha.
Hii nchi sasa naona kila post kubwa ni prof. au dk. Kazi ipo.
Yule mama wa NSSF alikaa masaa 5. Dr. RYOBA atakaa siku tano...natabiri Mh. Fulani kwa wadhifa wake atataka kumkalia kichwani lakini Daktari atagoma....hapo itakuwa kusuka au kunyowa....pia inawezakuwa mwisho wa Mh.Fulani
Mumewe si Andilile Mwainyekule ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ?
mkatoliki ameteua watu wake?! ye acha awajaze cc hatuna elimu, elimu yetu madrasa
RiobaKuna mteule Fulani anafahamika kwa uanaharakati wa Uhuru wa vyombo vya habari, si mwingine Bali ni Dr. Rioba!
Wasiwasi wangu ni kuwa boss wake mheshimiwa Fulani atamwambia " Uanaharakati mwisho chalinze" mjini ni chama tawala tu! Tusubiri tuone!
Ingekuwa jambo la msingi kama hizi nafasi zingetangazwa watu wakaomba na usaili ukafanyika tungepata watu makini zaidi kuliko marafiki kuvutana, naona prof Godius kama vile kuna mtu kamshika mkono, hainyeshi kama anayo taaluma au uzoefu katika investment au social security.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.
Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.
TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).
Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.
Lizaboni, ulikuwako kwenye bodi ya kumsaidia rais kuteua, especially kumteua huyo Dr. Ryoba?? Unachekesha saana mkuu!!Riona hajateuliwa kwa saabu ya uanaharakati wake bali kutokana na utendaji wake
kama mwenyewe ameridhia kwa moyo mweupe basi hakuna shida.hivi inawezekana kwa mteule kukataa uteuzi ama labda kuomba marekebisho yafanyike wizarani ndio akubali ? maana kiukweli si haki duniani hadi ahera kwa Ryoba kuwa chini ya Nape , tuwe wakweli jamani .