Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu na kumteua Anamringi Macha

MY FRIEND HAO WOTE WANATEULIWA NA RAIS!!
NA HAPA NDIPO NINAPOONA UBAYA WA KATIBA YETU!
DED na wakuu wa vitengo wako chini ya TAMISEMI; ni waajiriwa wa Wizara ya Nchi - Ofisi ya Rais; siyo wateule wa Rais! Wanasimaiwa na Waziri Mkuu
 
Historia ya huyu mheshimiwa ina UPS-and-DOWNS nyingi sana. Ukifuatilia historia yake tangu Mlimani(UDSM) hadi Minnessota hadi Dar, Arusha hadi Kahama katika kipindi cha miaka 22 iliyopita utaona kuwa ameshaanguka sehemu nyingi sana na kuamka tena. Alipoanguka UDSM aliibukia Minnesota State, na alipopoteza ajira yake 3M na maisha ya muziki hapo Minneapolis kukwama akaamua kurudi Tanzania akiahidi kuwa atakuwa mwanasiasa, ni kweli akafanikiwa mpaka kufikia ukuu wa Wilaya. Hapo katikati kuna mengi na ndiyo maana mimi nadhani ataamka tu, na huenda akawa waziri. Marehemu Swalehe Msuya aliwahi kuandika makala tatu kuhusu mheshimiwa Nkurlu enzi hizo, nimeweza kupata kopi za makala mbili; ile ya tatu siioni tena

Fadhili Nkurlu - A Music Legend in the Making - Mshale

MICHUZI BLOG: mdau arudi nyumbani kuendeleza libeneke
Kumbe ndiye aliyeboresha wimbo wa Malaika!!!!
 
Kumbe ndiye aliyeboresha wimbo wa Malaika!!!!

Hapana, huyu Fadhili Nkurlu hana uhusiano wowote na Fadhili Williams aliyerekodi kwa mara ya kwanza wimbo wa Malaika mwaka 1960; wimbo huo ulitungwa na Adam Salim mwaka 1945. Huyu Fadhili Nkurlu ambaye ana miaka kama 49 hivi, alizaliwa baada ya wimbo huo kuwa umesherakodiwa mara anyingi sana.
 
Huyu jamaa Fadhili ameingia kwenye Ugomvi mzito na Mkurugenzi wa Kahama Mji kisa wanagombania mwanamke mmoja Mtendaji Kata.


Ujio wa Magufuli mwezi wa 3 hapa Kahama aliwaambia wakae wamalize tofauti zao.. Lakini bado.


Hata hivyo huyu mkuu wa Wilaya ni mtu wa Starehe sana..... Gari la mkuu wa Wilaya linazurura hadi usiku wa manane.


Mkuu wa Wilaya yupo Mjini tu... Haendi Ushetu wala Msalala
Badooo wa ta........
MAANA hizo starehee zaooo zinawaaibishaa mjii mzimaaa kwakweli WANATIA AIBU kama awakujua MAANA ya UDC
 
Huyu jamaa Fadhili ameingia kwenye Ugomvi mzito na Mkurugenzi wa Kahama Mji kisa wanagombania mwanamke mmoja Mtendaji Kata.


Ujio wa Magufuli mwezi wa 3 hapa Kahama aliwaambia wakae wamalize tofauti zao.. Lakini bado.


Hata hivyo huyu mkuu wa Wilaya ni mtu wa Starehe sana..... Gari la mkuu wa Wilaya linazurura hadi usiku wa manane.


Mkuu wa Wilaya yupo Mjini tu... Haendi Ushetu wala Msalala
mkuu mbona tuliambiwa walipimwa sana utendaji wao na tabia kabla ya kuteuliwa?
 
Mbona yule mtangazaji wa Tbc Shabani Kissu alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya,alivyotolewa katika icho cheo mbona amerudi katika taasisi yake ya mwanzo ya Tbc,inakuwaje hapo
Mkuu, nina shaka na uelewa wako kuhusu masuala ya sheria.
 
Mkuu Nichumu Nibebike, ni kweli, nimesubiri sana, na nitaendelea kusubiri sana!, hivyo inaibidi sasa niongeze bidii, niongeze mapambio, sifia, tukuza na kujipendekeza kwa nguvu sana hadi anione!.

Hapa inahitajika bidii!, ila hata kama ningekuwa mimi, huyu Fadhili ningemtumbua tuu, kwanza ni bonge la HB, pili ni mtu wa pamba kali, unapiga suti kali, designers collection all the time na kutokelezea kuliko bosi wako?!, aende tuu!.

Kwa personal ratting yangu, huyu Jamaa ndio the best dressed DC!, anavishwa na Sheria Ngowi!, hivyo mimi katika Kipindi hiki cha kusubiria, suti zangu nitajishoneshea pale Mwenge, na kutokelezea kama Kangi Lugora!.

P.
Labda utakuwa na mahali kwingine kwa kutumbua pesa yako
 
Kama utaratibu huu ungekuwa unaleta tija inayokusudiwa,basi taarifa hizi za watu kuteuliwa na kutenguliwa kila kukicha zingekuwa zinapungua siku hadi siku lakini badala yake ndio kwanza zinaonekana kuongezeka na kwa tafsiri rahisi ni kuwa utaratibu huu haueleti tija iliyokusidiwa(mbinu imefeli).
Poor Assessment!
Kazi ya kusafisha nchi si ya siku moja,huyo DC nae aliingia kwenye biashara ya madini badala ya kuleta nafuu kwa wachimbaji wadogo akawa tatizo.Unamuachaje kazini mtu kama huyo
 
Poor Assessment!
Kazi ya kusafisha nchi si ya siku moja,huyo DC nae aliingia kwenye biashara ya madini badala ya kuleta nafuu kwa wachimbaji wadogo akawa tatizo.Unamuachaje kazini mtu kama huyo
Bora hata huyo DC kuliko mwenyekiti wako
 
Back
Top Bottom