Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu na kumteua Anamringi Macha

Mkuu Nichumu Nibebike, ni kweli, nimesubiri sana, na nitaendelea kusubiri sana!, hivyo inaibidi sasa niongeze bidii, niongeze mapambio, sifia, tukuza na kujipendekeza kwa nguvu sana hadi anione!.

Hapa inahitajika bidii!, ila hata kama ningekuwa mimi, huyu Fadhili ningemtumbua tuu, kwanza ni bonge la HB, pili ni mtu wa pamba kali, unapiga suti kali, designers collection all the time na kutokelezea kuliko bosi wako?!, aende tuu!.

Kwa personal ratting yangu, huyu Jamaa ndio the best dressed DC!, anavishwa na Sheria Ngowi!, hivyo mimi katika Kipindi hiki cha kusubiria, suti zangu nitajishoneshea pale Mwenge, na kutokelezea kama Kangi Lugora!.

P.
Hapo ulipompandia jamaa kisha ukitumia kichwa chako vizuri na kushusha nondo zilizoshiba sidhani kama atakushauri tena. Comment yako inabidi tuiweke penye hansard kama bungeni.
 
Ukisoma hii taarifa ya Waziri Mkuu utajua kila kitu.

WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.



Ametoa onyo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.



“Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini tatizo kubwa kila mmoja anaenda kivyake, hakuna anayemsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri wala Mkuu wake wa idara,” amesema.



Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewaeleza watumishi na viongozi hao kwamba Serikali haitavumilia kuona watumishi wa aina hiyo wanaendelea kufanya kazi.



“Serikali haitavumilia kuona watumishi wakifanya mambo ya hovyo. Kahama ni wilaya yenye majaribu na Shinyanga nayo ni wilaya yenye majaribu makubwa. Kwa hiyo watumishi inabidi muwe makini, kuweni waangalifu msije mkaingia kichwakichwa kwenye majaribu haya.”



“Migogoro niliyoisikia ambayo iko hapa ni kwa sababu ninyi mmeingia kwenye biashara na kutake sides. Hapa Kahama, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya hamuelewani, Mkurugenzi na wakuu wa idara hamuelewani, wakuu wa idara na wasaidizi wao nao pia hawaelewani,” alisema.



“Napenda kusisitiza kwamba ninyio ni viongozi wa umma, kwa hiyo ni lazima mzingatie itifaki za kiuongozi, mzingatie mahusiano mema mahali pa kazi. Hatupendi viongozi muwe chanzo cha matatizo hapa Kahama,” aliwaasa.



Alisema Kahama ina fursa kubwa na nzuri kwenye kilimo, madini, mifugo na biashara na akawataka viongozi wanaoletwa kwenye wilaya hiyo wawe makini. “Kiongozi ukiletwa hapa inabidi uwe na kichwa kilichotulia. Inabidi uwe mwaminifu sana ili uweze kudumu kwenye wilaya kama hii,” alisisitiza.



“Kama kiongozi ulizoea kwenda disco inabidi uache, kama ulizoea kwenda baa inabidi ununue kreti uweke ndani kwako. Kama ulizoea kushabikia mpira kwa kujichora chaki, sasa basi. Kaa sebuleni kwako, angalia mpira kwenye luninga yako, ndiyo dhamana ya uongozi hiyo,” alisema.



Aliwataka watumishi wa umma wawasaidie wananchi kuboresha utendaji wao kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji ili kila kuleta tija kwenye kila sekta.



Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake wilayani Kahama kwa kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.



(mwisho)



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, JULAI 15, 2018
Hapa ndio nimepata mwanga kiasi kwa nini yanatokea hayo pana ukiukwaji mkubwa wa maadili mahala hapo.
 
Sasa kamchagua mchagga Bw.Macha naona wameibuka wanyiramba hawatakiwi!
Acheni hizo.
Kitila mkumbo ni kabila gani, mbona hukulalamika wakati anachaguliwa na wachaga wanaachwa?

Hii ndio sumu ya ukabila mnayopandikiza wakosoaji wa Dr.Magufuli.
KAMA HUWEZI KUONA UBAGUZI TUNAOFANYIWA SASA HIVI BASI PITA TU.
MPAKA AJALI MNASEMA VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA AU WAZIRI ANAUHUSIKA TENA WAKISEMA WANASEMA MIKOA AU WILAYA ZILE WALIPO WATU WA IRAMBA TU.
HUKO MBEYA MMEMWANDAMA MKUU WA MAASKARI KAMA VILE YEYE NDIO NATENGENEZA MIUNDOMBINU MIBOVU YA BARABARA
 
Enzi za Jk Swedi Mwinyi aliteuliwa kuwa DC Kondoa Magufur alivyokuja akatengua ,sahz kalud TBC kwenye nafac yake ya zamani
Swedi mwinyi hajawahi kuteuliwa kuwa DC,
Utakuwa umemfananisha na Mkamia!
 
Huyu jamaa Fadhili ameingia kwenye Ugomvi mzito na Mkurugenzi wa Kahama Mji kisa wanagombania mwanamke mmoja Mtendaji Kata.


Ujio wa Magufuli mwezi wa 3 hapa Kahama aliwaambia wakae wamalize tofauti zao.. Lakini bado.


Hata hivyo huyu mkuu wa Wilaya ni mtu wa Starehe sana..... Gari la mkuu wa Wilaya linazurura hadi usiku wa manane.


Mkuu wa Wilaya yupo Mjini tu... Haendi Ushetu wala Msalala
wanagombania mwanamke......?
wilaya nzima yuko pekee?
 
Huyu jamaa Fadhili ameingia kwenye Ugomvi mzito na Mkurugenzi wa Kahama Mji kisa wanagombania mwanamke mmoja Mtendaji Kata.


Ujio wa Magufuli mwezi wa 3 hapa Kahama aliwaambia wakae wamalize tofauti zao.. Lakini bado.


Hata hivyo huyu mkuu wa Wilaya ni mtu wa Starehe sana..... Gari la mkuu wa Wilaya linazurura hadi usiku wa manane.


Mkuu wa Wilaya yupo Mjini tu... Haendi Ushetu wala Msalala
Mzee Kama Ni mtendaji ndio tatizo... Asiii Kuna mwanasheria tena wilaya hapa pia lilikuwa koloni lililoleta mushkeri mji hapa.
Basii wazee watakuwa na visasi vyao Tangu idarani.,
 
UKIANGALIA TAARIFA ZINAONYESHA PM AKISEMA KUNA UHUSIANO MBAYA KATI YA DED NA DC NA WAKUU WA VITENGO, AJABU ANAONDOLEWA DC HAO WENGINE WAANCHWA.
 
KAMA HUWEZI KUONA UBAGUZI TUNAOFANYIWA SASA HIVI BASI PITA TU.
MPAKA AJALI MNASEMA VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA AU WAZIRI ANAUHUSIKA TENA WAKISEMA WANASEMA MIKOA AU WILAYA ZILE WALIPO WATU WA IRAMBA TU.
HUKO MBEYA MMEMWANDAMA MKUU WA MAASKARI KAMA VILE YEYE NDIO NATENGENEZA MIUNDOMBINU MIBOVU YA BARABARA
nyie singida si ndio ngome kuu ya chama dola? mnalalama nini
 
nyie singida si ndio ngome kuu ya chama dola? mnalalama nini
TATIZO SIO NGOME, SHIDA NI PALE WANAPOSHAMBULIWA WATU WA ENEO MOJA KILA LAWAMA UTUMBUAJI UNAWAHUSU.
KWA MFANO KAHAMA PM ANASEMA KUNA MGOGORO WA DED NA DC, LAKINI DC ANAONEKANA NDIO TATIZO NA SIO DED AU MWINGINE YEYOTE.
NIMEGUNDUA TUNASHAMBULIWA!
 
Back
Top Bottom