Rais Magufuli atengua uteuzi wa January Makamba kuwa Waziri wa Mazingira; yeye asema ameyapokea mabadiliko kwa moyo mweupe

Natabiri msimamo wa Mzee Mkapa ndiyo utaamua hatma ya nani mshindi kwenye mnyukano huu ndani ya CCM. Kumbukeni Mkapa ndiye alikabidhiwa nchi hii na Mwalimu.

Atakachosema Mkapa ndiyo kitakuwa hatma ya Taifa zima . Tunaisubiri kauli ya Mzee kwanza haya mengine ni mbwembwe tu.
Huyo hana lolote. Nchi hii kwa sasa haina mtu "Vanguard" kama Nyerere asiye mnafiki ambaye akinena watu wana-pay attention. Hakuna, woote waliobaki ni wanafiki wanaosumbuliwa na "Guilt Conscience".
 
Kuna mfumo wa familia flani hapa Tz huwa zinahisi zina hati miliki na nchi.
Makamba family, Nape Nnauye, Ritz family, Ile ya visiwani, na baadhi ya marafiki zao.

Muwe kama Rais Mwinyi na Mwanae Waziri wa Ulinzi (hawana makuu kabisa)
Mwanae makuu anayo sana na nahisi magufuri hajamshitukia picha ya January Yuko na mwinyi inaonyesha kitu kama unaurafiki na Baba mwanae ni kama mtto wake tu husein atashirikiana na january
 
Huu uteuzi wa Bashe umefanyika kiufundi sana...ni mwana ccm lakini alikuwa makini mno kukosoa...kwa uteuzi wake ndio njia ya kumfunga mdomo.
 
Mambo mengi muda mchache, sasa hivi bora ukose hela ya chai ununue bando.

Naona Bashe kafungwa mdomo rasmi, sasa hivi ni mwendo wa kuimba mapambio tu.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂😂😂
 
Mwinyi atabaki kuwa mwinyi mwanae alimulea katika misingi ya heshima na busara anachapa kazi hayupo mitandaoni na siyo mtu wa makundi huwezi muona na hao vijana wanaodhani bila wao ccm haiwezi kutawala ! Acheni kuwa na fikra potofu watanzania wapo wengi wenye uwezo mkubwa wa kuongoza
Kama hujui Hussein na junuary ni marafiki unajidanganya.
 
nimeona habari kukamilika kwa reli ya mizigo moshi to tanga.
hii itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi wetu

wacha wanyoshane kwa sababu maisha yetu sisi wakawaida ni kukimbizana tu haijalishi rais awe nani bora huyu kajenga barabara karibia wilaya. ukarabati wa sekondari kongwe bila ubaguzi kila kona ya nchi.
kuondoa ile service fee tanesco imenipa unafuu, bila kusahau bei ya umeme haipandishwi kila mwaka kama enzi za wale wanaoona wanatukanwa
 
Badala ya hiki kilichotendeka nahisi ingefaa sana kuziba ufa
Na ufa mkubwa kuiziba ni kuita kikao cha dharula cha wazee wastaafu maana palipo na wazee haliharibiki neno au angeita kikao cha kamati kujadili jambo hilo. Hii nadhani ingekuwa njia sahihi na bora zaidi kwa mtazamo wangu.
Kutengua dakika hizi ni hatari sana hasa kwa afya ya siasa. Mzee wetu amefanya mambo makubwa sana lazima vita awe nayo tu kwasababu amefanya mambo makubwa mazuri kwa watanzania lakini magumu kwa wale waliokuwa wamezoea kupiga fedha. Lakini karata lazima zichangwe kwa umakini zaidi.
Hakuna cha kikao wala nini mkuu. Hata ningekuwa mimi hakuna kuitisha kikao,ni kuwakamua tu wote wasariti,tena pamoja na kuwapiga chini aendelee kuwakamua hata kama hawana maziwa,watatoa mpaka damu. Kuitisha kikao ni kama kuwabembeleza. Dawa ya moto ni moto
 
Ni muda mrefu Bwana Mwezi wa kwanza alishaonekana akizugusha mikono sema tu Kocha alikuwa bize, labda alikuwa anaogopa maneno, maana mkifungwa tu Wabongo watakusakama "kwa nini ulimuacha fundi Ajibu".
 
Good, bad, or indifferent, leo Rais Magufuli kanifurahisha saaaana. Kanifurahisha mnooo.

Huwezi kuwa na wasaliti ndani ya timu yako. Watu wa dizaini hiyo fukuza, timua, butua kabisa.

We mtu umeteuliwa kumsaidia Rais halafu unaanza kumhujumu. Tabia gani sasa hiyo?

Kama hukubaliani naye si ujiuzulu tu ile umpinge ukiwa nje kiroho safi na kwa dhamiri safi.

Huna haja ya kuchukua mshahara na perks zote zinazokuja na wadhifa wako halafu kumbe ni msaliti.

Hiyo haikubaliki hata kidogo. Naamini hata wewe mwenyewe wewe msaliti ukiwa na timu ya wasaidizi wako halafu ubaini mmoja wao anakusaliti na kukuhujumu, hutosita kumfukuzia mbali.

Ngosha leo kanifurahisha sana. Hajachelewesha mtu.

Hata kama sikubaliani na Ngosha kwenye kila kitu lakini ikija kwenye hili la huyu msaliti, nipo naye kwa asilimia kama zote. Yaani kwa asilimia 800.

Tena huyo msaliti ana bahati sana. Manake ingekuwa Magufuli ndo mimi ningemuibukia huko huko aliko na kumshikisha adabu.

Mtu unakula pesa za walipa kodi ili ufanye kazi uliyopewa, kumbe mtu mwenyewe hufanyi lolote la maana.

Umekaa tu na wenzako mkipanga mbinu za kumhujumu Rais.

Hapana aisee. Hiyo haikubaliki hata kidogo na haivumiliki hata chembe.

Fukuzia mbali wasaliti na wahujumu wote.
Vipi umeipata wewe hiyo nafasi? nyie ndio wenye PHD alizosema Musiba.
 
Hakuna cha mpasuko wala nini. Huwezi kufunga ng'ombe na punda Halafu wakavuta tela pamoja kwani punda huwa anapiga mluzi akifika mlimani hivyo kumfanya ng'ombe asimame. Hakiwezekani kuongoza nchi ukawa na timu ya viongozi wanafiki wenye kutaka kukuharibia kazi zako ili wao wang'are. Dawa ni kuachana nao. Watanzania tuko nawewe mheshimiwa JPM mpaka mwisho wa dahari. Come what may
Amin
 
Back
Top Bottom