Rais Magufuli atengua uteuzi wa January Makamba kuwa Waziri wa Mazingira; yeye asema ameyapokea mabadiliko kwa moyo mweupe

Sodium

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
754
398
Kwaheri January Makamba, ila tutakukumbuka kwa kufanikisha suala la mifuko ya plastic.

76101980-EF1B-4C28-95D0-8046350B04EC.jpeg


Yeye asema ameyapokea Mabadiliko kwa moyo mweupe:

91E8435D-4953-442D-AE6D-886D1BC4AC0C.jpeg

Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa . Nitasema zaidi siku zijazo.

Zaidi...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanioa Dkt John Pombe Magufuli leo Julai 21, 2019 amemteua Mbunge wa Kibakwe George Simbachawene kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya January Makamba.


Uteuzi huo wa Rais Magufuli unamfanya Simbachawene kuweka rekodi ya kuwa Mbunge pekee ambaye alijiondoa kwenye Baraza la Mawaziri na kurejea tena baada ya miaka miwili.

Septemba 06. 2017 akiwa Waziri wa TAMISEMI, Simbachawene alitajwa kwenye ripoti ya Uchimbaji wa madini ya Tanzanite, na Almasi kupitia Kamati ya Bunge, ripoti ambayo iliwasilishwa kwa Spika Ndugai na yeye kumkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa ili aipeleke kwa Rais Magufuli.

Septemba 06. 2017 baada ya ripoti hiyo kukabidhishwa kwa Rais Magufuli, Simbachawene alitangaza kujiuzulu nafasi Uwaziri wa TAMISEMI ili kupisha tuhuma dhidi yake.

Agosti 28, 2018, Simbachawene alichaguliwa na Wabunge wenzake kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi Hawa Ghasia ambaye alitangaza kujizulu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI Ametengua Uteuzi wa January Makamba na kufanya Teuzi Kadhaa.

January alikuwa Ofisi ya Makamu wa Rais akishughulikia mambo ya mazingira na Muungano. Nafasi yake imechukuliwa na Mh. Simbachawene

Wakati huohuo Mh. JPM amemteua Mh. Hussein M. Bashe kuwa Naibu waziri wa Kilimo. Bashe ameziba pengo ambalo liliacha na Mh. Innocent Bashungwa ambaye sasa ni waziri wa viwanda na Biashara.

Mwisho, Mh. JPM amemteua Mh. Martin Lumbanga kuendelea kushika Uenyekiti wa Bodi ya wakurugeni Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma PPRA kwa Muhula mwingine

Ref. Attachment
IMG_20190721_071911.jpeg


Jpili njema
 
Hakuna cha mpasuko wala nini. Huwezi kufunga ng'ombe na punda Halafu wakavuta tela pamoja kwani punda huwa anapiga mluzi akifika mlimani hivyo kumfanya ng'ombe asimame. Hakiwezekani kuongoza nchi ukawa na timu ya viongozi wanafiki wenye kutaka kukuharibia kazi zako ili wao wang'are. Dawa ni kuachana nao. Watanzania tuko nawewe mheshimiwa JPM mpaka mwisho wa dahari. Come what may



Badala ya hiki kilichotendeka nahisi ingefaa sana kuziba ufa
Na ufa mkubwa kuiziba ni kuita kikao cha dharula cha wazee wastaafu maana palipo na wazee haliharibiki neno au angeita kikao cha kamati kujadili jambo hilo. Hii nadhani ingekuwa njia sahihi na bora zaidi kwa mtazamo wangu.
Kutengua dakika hizi ni hatari sana hasa kwa afya ya siasa. Mzee wetu amefanya mambo makubwa sana lazima vita awe nayo tu kwasababu amefanya mambo makubwa mazuri kwa watanzania lakini magumu kwa wale waliokuwa wamezoea kupiga fedha. Lakini karata lazima zichangwe kwa umakini zaidi.
 
Back
Top Bottom