Rais Magufuli atembelea Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili, Amjulia hali Mufti Mkuu Tanzania

incorruptible

Member
Apr 19, 2014
62
46
Akitokea Dodoma leo, Magufuli amepita kumjulia hali Mufti mkuu wa Tanzania Zuberi . Katika hali ya kushangaza kwa mara nyingine tena amekuta wodi ya kina mama wanalala chini na hata wengine katika vitanda wanalala watano watano.
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    126.9 KB · Views: 134
  • image.jpeg
    image.jpeg
    166.2 KB · Views: 171
hi kuanzia mkurugenzi wa muhimbili, katibu mkuu wizara ya afya waziri naibu waziri hawajui akina mama wajawazito wanalala chini? ina maana huyo mkurugenzi hatembelei eneo lake la kazi na kuona matatizo yaliyopo? kweli ma prof tuna
 
Nadhani sasa ataelewa pale tunapomwambia kuwa awe anaangalia msingi wa jambo zaidi ya juujuu! Asibweteke kufukuza watumishi kama kawaida yake akadhani ametatua tatizo! Aangalie msingi wa tatizo! Hakuna anayependa kupoteza kazi yake!
 
Hivi mapato yanayoingia hayawezi kununua hata kitanda kimoja kila siku na kwa mwaka walau vitanda 150 hadi 300?
Maprofesa wetu na wasomi wetu wa leo ni wa posho tu si wabunifu hata kidogo.
 
Hapo ndipo tujiulize, wana mipango wa Kitanzania wanajua vipaumbele kweli ? Tatizo ni vitanda na magodoro au ni kupanua wodi?? Kipi kwanza?? Wagonjwa wanaongezeka Muhumbili kwa sababu ya upungufu ulioko hospitali nyingine, sasa hata kama stoo kuna vitanda, je wavifunge juu ya vingine?? Naomba tu mwana mipango mmoja anijibu.
Raisi wangu, wamekudanganya hao??
 
Amfukuze Mseru basi...
Tatizo la Muhimbili siyo vitanda.. bali ni hospital imeshakuwa ndogo.. miaka iliyopita kina mama walikuwa wanalala chini kusema kweli hospital imezidiwa tena mno.
Mseru hawezi kuiondoshwa kwani zile makurupuko yote ilikuwa inatafutwa sababu ya kuwekwa yeye. kwani yule kaimu mkurugenzi aliyekuwepo aliyarithi yale matatizo ya CT scan kutoka kwa Marina Njelekela na jamaa alikaimu hata miezi 3 haijafika.Na ilipogundulika ya kuwa wizara ya fedha ndiyo tatizo kwa kushindwa kutoa pesa za ukarabati na Muhimbili haiwezi kutafuta fundi mwengine kutokana na mikataba iliyokwisha kutiwa na mizara ya afya... lakini baada ya jamaa kuondoshwa tu pesa za ukarabati zikatoka. Huo utaona ni mpango wa kisanii na PR wa ikulu akaiaminisha jamii ya kuwa kaimu mkurugenzi ndiyo lilikuwa tatizo.... Sasa miezi mitatu imeshapita je Mseru atawajibishwa? kwani ameshakaa muda sawa sawa na alokaa Dr Hussein Kidanto. Tuangalie usanii utaleta habari gani na utatuaminisha vp?
 
Hivi huyo magu hajui kama muhimbili ni ndogo kulinganishwa na mahitaji ??
 
Asikilize ushauri wa wataalamu la sivyo atajikuta amekuwa kichaa..

Tengeneza mfumo mzuri ambao kila mtu ataufuata, tunga sheria ambazo zitawabana wazembe na nk, toa elimu kwa raia wafahamu haki zao na pale zinapopindishwa waelekezwe jinsi na wapi pa
kuzidai, jenga uzalendo kwa watanzania ondoa dhana ya uvyama, Jenga mapenzi kwa wananchi wako maana mpaka sasa Mh.Mangu haeleweki ni kitu gani anachosimamia..Na mwisho akumbuke Tanzania si Dar peke yake wala Hospital si Muhimbili tu
 
Back
Top Bottom