Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa afanya mazungumzo na katibu mkuu wizara ya ulinzi wa Burkina Faso

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
832
533
KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI WA BURKINA FASO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mei 16, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Burkina Faso Bw. Jean Baptiste Parkouda katika Ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Upanga jijini Dar-es-Salaam.

Katibu Mkuu Mnyepe kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alimfahamisha mgeni wake, utayari wa Wizara ya Ulinzi na JKT kushirikiana na Wizara ya Ulinzi ya Burkina Faso katika mambo ya Ulinzi na Usalama, Utawala na mafunzo, pamoja na kubadilishana wanafunzi katika vyuo vya kijeshi.

Kwa upande wake Jean Baptiste Parkouda, alimueleza Katibu Mkuu wa Ulinzi na JKT, utayari wa Wizara ya Ulinzi ya Burkina Faso kushirikiana na Wizara ya Ulinzi ya Tanzania katika masuala mbalimbali yahusuyo Mafunzo, Vita dhidi ya Ugaidi na kubadilishana utaalamu katika mambo mbalimbali yahusuyo ulinzi na usalama kati ya Tanzania na Burkina Faso.

Aidha, Makatibu hao walizungumzia ushirikiano katika masuala ya Afya, ambapo Dkt. Mnyepe alimfahamisha Katibu Mkuu mwenzake wa Burkina Faso fursa zilizopo Tanzania katika kubadilishana uzoefu katika masuala ya Afya kwa kupitia Taasisi za Afya za Kijeshi na Kiraia kama Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katibu Mkuu Jean Baptiste Parkouda aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT kwa kuandaa Mkutano Mkuu wa Michezo ya Majeshi Duniani - CISM na kusema kuwa kitendo cha Tanzania kukubali kuandaa Mkutano huo mkubwa duniani ni cha kupongezwa kutokana na gharama kubwa za uandaaji wa Mkutano Mkuu wa Dunia. Katibu Mkuu Parkouda akasema Burkina Faso inajisikia fahari kubwa kwa Tanzania kuwezesha mkutano huo kufanyika Tanzania, na akafikisha salamu za Waziri wa Ulinzi wa Burkina Faso kwa Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania.

Katika mazungumzo hayo ya Makatibu wakuu wa Wizara za Ulinzi za Tanzania na Burkina Faso pia zilihudhuriwa na Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini Rear Admiral Michael Mumanga na maafisa wengine toka Wizara ya Ulinzi na JKT.

20240517_080103_InSave_4.jpg
20240517_080103_InSave_6.jpg
20240517_080103_InSave_2.jpg
20240517_080103_InSave_5.jpg
 
Back
Top Bottom