Rais Magufuli ataka Rais Museveni kuwa mkali kwa watendaji wake

Wewe unategea vyanzo vya Habari toka sehemu zisizo aminika mwenzio Jiwe ana vyanzo vyake hadi pale Ikulu so pengine anajua huo mradi unakwama kwa sababu gani

Hivyo vyombo vya rais sasa hivi kazi yake kubwa ni kuwafuatilia vyama vya upinzani, na kudukua mawasiliano ya watu ili kumpa rais taarifa.
 
Mambo kama hayo nadhani yalistahili kuzungumzwa faragha. Kumkosoa Rais mwenzako hadharani namna hiyo, nadhani haikuwa poa.
Faragha ndio yanachelewesha mambo,faragha kwani wanauza cocaine mkuu?

Kamchana live ili tujue kikwazo kipo wapi, asingeeleza ukweli wewe ulijua mradi umekwama wapi?

Msema kweli ni mpenzi wa mungu(Mheshimiwa Magufuli's voice)
 
Nimemsikia pia.

Ila hili swala la kuingilia nchi nyingine na kuonyesha kana kwamba hawafanyi kazi vizuri kwa kweli siyo uungwana. Tanzania bado ina mapungufu mengi sana katika utendaji chini ya awamu hii. Kubadilisha Commissioners wa TRA haina maana kwmba utendaji umekuwa mzuri. Mfano haukuwa sahihi hata kama ulikuwa ni utani tu haukuwa mahali pake!!
Sawa Mr. Zero
 
Faragha ndio yanachelewesha mambo,faragha kwani wanauza cocaine mkuu?

Kamchana live ili tujue kikwazo kipo wapi, asingeeleza ukweli wewe ulijua mradi umekwama wapi?

Msema kweli ni mpenzi wa mungu(Mheshimiwa Magufuli's voice)
Kwa mfano M7 angemwambia mzee baba hadharani(mimi ningekua na rc kama konda boy ningemtumbua chap sijui kwanini unamchelewesha),hapo Magu angechukuliaje?
 
Rais wetu hua anasema mara kwa mara kua hafundishwi na wala hakuna mtu wa kumpangia au kumshauri amuweke nani mahala gani na amtoe nani na akasisitiza kua ukitaka kuharibu kabisa mshauri cha kufanya.

Hii ni baada ya watu kitaka kumshinikiza amuondoe Makonda baada ya kuvamia ofisi ya utangazaji ya CMG.

Kilichonishangaza yeye mheshimiwa rais wetu anapangia wengine na kuwashauri cha kufanya nani akae wapi nani akae kule.

Hii naiona ni kituko kwa sababu iwapo yeye alisema hakuna mtu wa kumpangia kumuondoa Makomda, iweje yeye ampangie M7 amuondoe makonda wake wa kule?
 
Kuna sehemu niliandika hapa kwamba jamaa ni mshamba bwege (country bumpkin).

Hajui diplomasia, hana ujanja (tact), mwingi wa kukurupuka halafu mwepesi wa kusahau.

Alichokifanya kwa Museveni ni kama anampangia rais mwenzake cha kufanya hadharani, wakati yeye kasema hataki kupangiwa.

Babu jinga!
 
Ona sasa ulivyo mjinga! Wenzio wameongelea suala la utendaji ili hilo Bomba likamilike wananchi wapate ajira, wewe unaleta Habari za majenerali?
Unafikiri pale alikuwa ni ccm na chadema au Magufuli na Membe pale?
Mjinga mwenyewe, kwamba Waganda hawaelewi kuwa wanahitaji kuuza hayo mafuta ama? Kwani hayo mafuta si ya kwao, unafikiri ni ya Magufuli? Complete idiot, go hang!
 
Kwa mfano M7 angemwambia mzee baba hadharani(mimi ningekua na rc kama konda boy ningemtumbua chap sijui kwanini unamchelewesha),hapo Magu angechukuliaje?
🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️
 
mpingani at work.... wazee wa Nongwa ....
Pinga kila kitu... i mean kila kitu....
hata angesalimia tu asiseme kingine mngepinga tu...
Dammit pinga hadi kufa....
huyu mtu muwe mnamuandikia hotuba,,,,anapayuka sana aise....anamfundisha mu7 kuendesha nchi wakati mu7 kaingia madarakani ilihali yeye akiwa mwalimu.....anamfundisha dereva kukata kona..
 
tuandamane kupinga JPM kumshauri Museveni.... yani kafanya kosa kubwa sana..

Nafanya mazoezi ya kuwa mpinzani/ mpingani....

Ila nadhani has something to do na matatizo ya akili ama ushirikina ama roho mbaya ama hate ya kuzaliwa. ..

Hakuna jema...... nyambafuz
Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtaka Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.

Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika leo Ijumaa Septemba 6, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania, Magufuli amesema Serikali yake ilifanya mabadiliko ya sheria ili kupunguza sehemu ya kodi kwa ajili ya mradi huo.

Amemtaka pia Rais Museven kuchukua hatua nchini kwake kwa kuwa tayari kupoteza kidogo kama Tanzania ilivyofanya ili apate kikubwa zaidi.

Pia, amemshauri kama watendaji wake ndiyo kikwazo asisite kuwaondoa na kuweka wengine.

“I wish (ninatamani) hawa watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ni-deal (nishughulike) nao angalau kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli huku washiriki wa mkutano huo wakicheka.

Amewataka watendaji katika nchi za Uganda na Tanzania wahakikishe wanafanikisha miradi mikubwa ambayo inatengeneza ajira nyingi. Amesema watendaji wengi hawajali kwa sababu wanapata mishahara.

Kwa upande wake, Rais Museven amewataka wafanyabiashara kujadiliana kwa kina na kujibu swali linalouliza “utajiri wa mataifa unatoka wapi?” kama lilivyoulizwa na Adam Smith kwenye kitabu chake cha Wealth of Nations (Utajiri wa Mataifa).

Museven amesema suala la miundombinu ni muhimu katika kurahisisha biashara baina ya mataifa hayo kwa sababu gharama za usafirishaji wa kontena kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Port Berry itakuwa Dola za Marekani 1600 badala ya Dola 4500 za sasa.

Kiongozi huyo alimhakikishia Rais Magufuli kwamba serikali yake itahakikisha bomba la mafuta linajengwa na mafuta ambayo yamekuwepo kwa miaka milioni mbili iliyopita yanapatikana kwa maendeleo ya wananchi.

View attachment 1199967

Chanzo: Mwananchi
 
Watanzania wajiandae kuanza kufurushwa (na/au kunyanyaswa) Uganda. Huwezi kuwatukana watu kutokana na kutekeleza majukumu yako kwa mujibu wa taratibu zao.
Acha uoga ww labda kama ww ndio unataka kuanzisha ili wakuanze na ww.
 
huyu mtu muwe mnamuandikia hotuba,,,,anapayuka sana aise....anamfundisha mu7 kuendesha nchi wakati mu7 kaingia madarakani ilihali yeye akiwa mwalimu.....anamfundisha dereva kukata kona..
Unatakiwa wakuanze kukuandikia ww maana unatuwekea hivyo,,,,,, na ..... vinamaanisha nn.
 
Kwa mfano M7 angemwambia mzee baba hadharani(mimi ningekua na rc kama konda boy ningemtumbua chap sijui kwanini unamchelewesha),hapo Magu angechukuliaje?
Mkuu ungejibu kwanza nikichouliza, kumbuka kaweka kila kitu hadharani ili wananchi tujue kikwazo cha mradi wa bomba mafuta kipo wapi maana ndio kabeba dhamana ya watanzania wote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom