imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 46,676
- 71,057
By Peter Saramba, Mwananchi
Mwanza. Onyo alilotoa Rais John Magufuli, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, kwa viongozi wa chama hicho tawala kuwa wasipoangalia kinaweza kuanguka, linaweza kuwa tahadhari mahsusi wakati huu, baadhi ya wasomi na wanasiasa wana mawazo wamekubaliana na mawazo hayo.
Rais Magufuli alisema hayo wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM jijini Mwanza Alhamisi iliyopita, akisema CCM inaweza kupoteza dola iwapo viongozi wake watajisahau na kuongoza kwa mazoea bila kukidhi mahitaji na matarajio ya wananchi.
Sehemu hiyo ya hotuba yake mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM--chombo cha pili kwa mamlaka baada ya Mkutano Mkuu imeibua mijadala, wengi wakihoji sababu za kutoa kauli hiyo wakati huu.
Wako wanaoona kuwa Rais ameona mbali baada ya kukiongoza chama hicho kwa miaka minne, wapo wanaoona ni tahadhari ya kawaida na wapo wanaoona nguvu ya upinzani ikiongezeka.
Rais ametoa tahadhari hiyo katika kipindi ambacho vyama vya siasa vinajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya uliopita kuwa na ushindani mkali kuliko wakati mwingine wowote tangu kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1992.
Katika uchaguzi huo, Magufuli alishinda kwa kupata kura milioni 8.8, sawa na asilimia 58, kiwango ambacho ni kidogo tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995.