Rais Magufuli atabiri anguko kuu la Chama Cha Mapinduzi

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
46,676
71,034
By Peter Saramba, Mwananchi

Mwanza. Onyo alilotoa Rais John Magufuli, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, kwa viongozi wa chama hicho tawala kuwa wasipoangalia kinaweza kuanguka, linaweza kuwa tahadhari mahsusi wakati huu, baadhi ya wasomi na wanasiasa wana mawazo wamekubaliana na mawazo hayo.

Rais Magufuli alisema hayo wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM jijini Mwanza Alhamisi iliyopita, akisema CCM inaweza kupoteza dola iwapo viongozi wake watajisahau na kuongoza kwa mazoea bila kukidhi mahitaji na matarajio ya wananchi.

Sehemu hiyo ya hotuba yake mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM--chombo cha pili kwa mamlaka baada ya Mkutano Mkuu imeibua mijadala, wengi wakihoji sababu za kutoa kauli hiyo wakati huu.

Wako wanaoona kuwa Rais ameona mbali baada ya kukiongoza chama hicho kwa miaka minne, wapo wanaoona ni tahadhari ya kawaida na wapo wanaoona nguvu ya upinzani ikiongezeka.

Rais ametoa tahadhari hiyo katika kipindi ambacho vyama vya siasa vinajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya uliopita kuwa na ushindani mkali kuliko wakati mwingine wowote tangu kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1992.

Katika uchaguzi huo, Magufuli alishinda kwa kupata kura milioni 8.8, sawa na asilimia 58, kiwango ambacho ni kidogo tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995.
 
Rais anajua CCM imeshaanguka muda mrefu tokea aliposhika kiti cha urais, kilichobakia ni kuvuta siku mbele ili CCM isife mikononi mwake; Hivo solution iliobakia ni;

1) Kutumia "DOLA" kwa kuwawekea vizuizi wapinzani wasifanye mihadhara na mikutano.

2) Kutumia "DOLA" kuwafunga na kuwapa kesi za kisiasa viongozi wa upinzani na wanachama wao.

3) Kutumia "DOLA" kufunga na kunyamazisha vyombo vya habari na mitandao.

4) Kutumia "DOLA" kuanzisha sheria kandamizi za vyama vya siasa, habari, mitandao ya simu na internet, mahesabu na matumizi ya serikali.

5) Kutumia "DOLA" kuwaminya na kuwaogopesha wafanyabiashara, wapinzani na raia.

6) Kutumia "DOLA" kufanya "CAMPAIGN" za kujinadi na kukinadi CCM kwa kugawa pesa na kuzunguka nchi nzima na jopo la mawaziri na watendaji wa serikali (Sio kwa nia ya kujua "SHIDA" za wananchi, bali kutangaza yanayofanyika).

7) Kutengeneza matukio ili kuwahamisha raia kifikra (KIKI).

8) Kutumia "DOLA" kupeleleza na kuhoji "PRIVACY" za raia, wafanyabiashara na wanasiasa kwa kupekua Account zao.

9) Kutumia "DOLA" kuachilia mazungumzo ya simu ya siri za wapinzani na wana CCM wenzao ili kuleta taharuki, chuki, mifarakano na sintofahamu kwa wanasiasa wa upinzani na ccm wenzao.

10) Kutumia "DOLA" kuwakata wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa mitaa na kukipa ushindi CCM kwa asilimia 100%.

NB Kama kungekua na "FAIR LEVEL PLAYING GROUND" kisiasa nchini. CCM sasa hivi ingekua imeshakufa na kuzikwa zamani sana. Ila hayo yanayotumika sasa hivi kukifanya chama kipumue (ICU) kwa siku chache zijazo sio kwamba yatakifanya kuongoza milele ndio maana ametoa "ANGALIZO" hilo.

Ila mgonjwa bado mahututi sana ICU, roho inamtoka halafu inarudi kwenye kiwiliwili chake. Pumzi zinakata na kurudi.
 
Tutafanya sherehe nchi nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
tenor.gif

Ni VIGELEGELE NCHI NZIMA!
 
Sijawahi kujisikia furaha namna hii tokea nizaliwe huko Iramba chini ya mbuyu takriban miaka sitini iliyopita.
 
Rais anajua CCM imeshaanguka muda mrefu tokea aliposhika kiti cha urais, kilichobakia ni kuvuta siku mbele ili CCM isife mikononi mwake; Hivo solution iliobakia ni;

1) Kutumia "DOLA" kwa kuwawekea vizuizi wapinzani wasifanye mihadhara na mikutano.

2) Kutumia "DOLA" kuwafunga na kuwapa kesi za kisiasa viongozi wa upinzani na wanachama wao.

3) Kutumia "DOLA" kufunga na kunyamazisha vyombo vya habari na mitandao.

4) Kutumia "DOLA" kuanzisha sheria kandamizi za vyama vya siasa, habari, mitandao ya simu na internet, mahesabu na matumizi ya serikali.

5) Kutumia "DOLA" kuwaminya na kuwaogopesha wafanyabiashara, wapinzani na raia.

6) Kutumia "DOLA" kufanya "CAMPAIGN" za kujinadi na kukinadi CCM kwa kugawa pesa na kuzunguka nchi nzima na jopo la mawaziri na watendaji wa serikali (Sio kwa nia ya kujua "SHIDA" za wananchi, bali kutangaza yanayofanyika).

7) Kutengeneza matukio ili kuwahamisha raia kifikra (KIKI).

8) Kutumia "DOLA" kupeleleza na kuhoji "PRIVACY" za raia, wafanyabiashara na wanasiasa kwa kupekua Account zao.

9) Kutumia "DOLA" kuachilia mazungumzo ya simu ya siri za wapinzani na wana CCM wenzao ili kuleta taharuki, chuki, mifarakano na sintofahamu kwa wanasiasa wa upinzani na ccm wenzao.

10) Kutumia "DOLA" kuwakata wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa mitaa na kukipa ushindi CCM kwa asilimia 100%.

NB Kama kungekua na "FAIR LEVEL PLAYING GROUND" kisiasa nchini. CCM sasa hivi ingekua imeshakufa na kuzikwa zamani sana. Ila hayo yanayotumika sasa hivi kukifanya chama kipumue (ICU) kwa siku chache zijazo sio kwamba yatakifanya kuongoza milele ndio maana ametoa "ANGALIZO" hilo.

Ila mgonjwa bado mahututi sana ICU, roho inamtoka halafu inarudi kwenye kiwiliwili chake. Pumzi zinakata na kurudi.
You are very right
 
Ni tahadhari kwa CCM. Uchaguzi wa serikali za mitaa imekuwa ni eye-opener ikizingatiwa ulisimamiwa na serikali yenyewe. Haki huzaa vitu vingi sana, utajiri, furaha, amani nk. Pamoja na mambo mengi yanayotajwa kama kuendeleza kwa miundombinu kama reli, ndege na bwawa la umeme - haki za watu zimepungua na kukandamizwa sana!!

Binafsi ninadhani kuondoka kwenye uchumi wa viwanda na kuja kwenye vipaumbele visivotoa ajira haraka, ndio kitu kilichokosesha wananchi muamko. Kipato cha mwananchi wa kawaida kimepungua kwa sababu hakuna ajira rasmi, ajira binafsi zimeathiriwa nk. Kwa ufupi hali ya kiuchumi au imeanguka au imebaki palepale!!
 
By Peter Saramba, Mwananchi
Rais ametoa tahadhari hiyo katika kipindi ambacho vyama vya siasa vinajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya uliopita kuwa na ushindani mkali kuliko wakati mwingine wowote tangu kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1992.
Katika uchaguzi huo, Magufuli alishinda kwa kupata kura milioni 8.8, sawa na asilimia 58, kiwango ambacho ni kidogo tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995.
P
 
Hakuna kitu kibaya Kama ukimfundisha mwanafunza halafu anachokiona ni tofauti na anachokiona nyumbani na katika mazingira yanayomzunguka.

Ndiyo kazi.ya wasaidizi wake. Kaika uongozi busara na hekima ni muhimu sana. Chuki ni kitu kibaya sana katika jamii. Nenda baba, nenda ufike salama. Acha watanzania wabaki na makovu yao. Kaendelee kula kuku kwa mirija.

Watanzania wataanza tena safari ya kutaguta maisha ya kujikomboa upya.

Yaani nikiwa usingizini nikaikumbuka cccm usingizi unakata na sipati tena usingizi.
 
Halafu Mohamed Shein anasema atajenga Daraja kutoka Unguja hadi Dar
Mimi nikajiuliza je litakuwa daraja la Minazi?
 
Back
Top Bottom